Wanachama na wajumbe wa baraza la UVCCM Wilaya ya Chunya wakisikiliza kwa makini
Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Liawale Mkpoani Lindi Timoth Mzava akiwa katika picha ya pamoja na makada wenzake akiwemo mjumbe wa baraza la UVCCM Mkoa wa Mbeya akiwakilisha Wilaya ya Ileje Mary Mwanisongole katika mnara wa miaka 50 ya Uhuru Wilayani Chunya
Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Chunya Saul Mwaisenye akizungumza wakati wa ufunguzi wa baraza la vijana Wilayani humo
Mjumbe wa baraza kuu ya UVCCM Taifa Neema Mwandabila akizungumza katika ufunguzi wa baraza hilo Wilaya ya Chunya
Chunya .Vijana na wanachama
wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Mbeya wametakiwa
kusimamia na kudhibiti maadili ya viongozi na wananchama badala ya kutumika na
wanasiasa wanaotaka madaraka kwa lengo la kujinufaisha wao na familia zao.
Kauli hiyo imetolewa na
Katibu msaidizi wa umoja wa vijana wa CCM Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi Timoth
Msava katika mkutano wa baraza la vijana la Wilaya ya Chunya
lililofanyika jana katika ukumbi wa
chama hicho.
Alisema kuwa kazi ya vijana ni
kuhakikisha wanachama na viongozi wanakuwa na maadili mazuri kwa mujibu
wa kanuni na katiba ya chama kwa lengo la kujenga chama na kurudisha imani ya
chama kwa jamii nzima.
“Vijana tunapaswa kubadilika
na kufanya kazi kwa kufuata kanuni za chama chetu kwani maadili ya baadhi
ya wanachama na viongozi wetu siyo mazuri na badala tumegeuzwa na kuwekwa
mifukoni mwa wagombea na kufanywa madaraja ya kupatia madaraka kwa
masilahi yao binafsi”alisema
Akitoa taarifa ya Jumuia
hiyo Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Chunya Saul Mwaisenye alisema
kuwa kuna kero ambazo zisipopatiwa ufumbuzi haraka vijana wengi
ambao ni wakulima na wafugaji watakata tamaa na kuichukia serikali yao
Mwaisenye alizitaja kero
hizo kuwa ni pamoja na vojana kutotengewa maeneo ya kuchimba dhahabu ili
kuondoa mzozo unoajitokeza mara kwamar kati yao na wawekezaji na kusababisha
kuijengea chuki serikali yao.
Alizitaja kero nyingine kuwa
ni pembejeo za kilimo zinazotolewa kama ruzuku na serikali kutofika kwa wakati
na asilimia 10 zinazotakiwa kutolewa na halmashauri ya Wilaya kwa ajili
kukopeshwa vikundi vya vijana na akinamama hazitolewi.
0 comments:
Post a Comment