Mmoja wa viongozi wa kikundi cha ulinzi na usalama cha UVCCM (GREEN GADI)akitoa ishara ya heshima wakati wa mgeni rasmni alipokuwa akiingia ukumbini
Baraza hilo lilipata mgeni kutoka nchi ya CROATIA aliyejitambulisha kwa jina la Leta aliyekuwa ameongozana na mgeni rasmi mjumbe wa baraza kuu la UVCCM Taifa Neema Mwandabila
Katibu msaidizi wa UVCCM Wilaya ya Liwale Mkoa wa Lindi Timoth Mzava akizungumza katika ufunguzi wa baraza hilo na kuwataka vijana kusimamia na kudhibiti maadili ya viongozi na wanachama wake badala ya kubaki kutumika na watu wanaotaka madaraka kwa masilahi yao binafsi na familia zao.
CHUNYA. Mjumbe wa baraza kuu la Taifa Neema Mwandabila amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni badala ya kubaki kuwabebea mabango wazee.
Akizungumza
jana katika mkutano wa baraza la UVCCM
Wilaya ya Chunya uliofanyika katika
ukumbi wa chama hicho alisema kuwa ni wakati wa vijana kutumia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na uchaguzi huo kwa
kushiriki chaguzi mbali mbali na kugombea na nafasi mbali mbali za
uongozi.
“Msimamo wa chama cheti na kuhakikisha tunashiriki
kikamilifu katika chaguzi mbali mbali huku tukiwa na lengo moja la kushinda na kushika dola hivyo kama vijana tunanafasi pia kuhakikisha
tunagombea na kushinda badala ya kubaki kuwabebea mabango wazee”alisema
Aidha Mwandabila alisema kuwa ni kazi ya kuhamasisha jamii kwenda kujiandikisha katika dafatari la
wapiga kura mara utaratibu ukapoanza ili
kuweza kuwa na wapiga kura wengi ambao wamejiandikisha na kitambulisho cha
mpiga kura.
Alisema kuwa
marekebisho ya dafatari hilo yanatarajia kuanza hivi karibu hivyo ni vema
vijana wakajiandaa kwa kuhamsisha
familia zao na jamii inayowazunguka kwani kutoka kufanya hivyo uwepo wa Uvccm utakuwa hauna maana.
Kuhusu
Katiba Mpya mjumbe huyo alisema kuwa
vijana wanapaswa kuzingatia msimo wa chama hicho wa kuwepo kwa serikali
mbili kwani hakuna nafasi ya kuhoji kuhusiana mfumo huo wa serikali mbili.
“Nilazima kama vijana tushiriki katika kuhamasisha
wananchi kuikubali serikali mbili kwani huo ni msimo wa chama chetu kwa la
kuulinda muungano wetu hakuna sababu kwa sisi vijana kuendelea kuhoji suala hili kwani tayari linaeleweka kwamba ni
lazima katiba yetu ielekeze uwepo wa serikali mbili”alisema
Mwandabila
alisema kuwa kuna muda utafika kwa
katiba hiyo kwenda kwa wananchi kwa ajili ya kuipigia kura ya ndiyo au hapana
hivyo ni wajibu wa vijana kushiriki kikamilifu katika kufanya kampeni ya kuhakikisha wananchi wanaikubali kwa kuwa
na serikali mbili.
0 comments:
Post a Comment