Waziri Chiza akimuuliza maswali mhandisi Elibariki Mwendo kutoka ofisi ya umwagiliaji kanda ya Mbeya ambao ndiyo wasimizi wakuu wa miradi hiyo baada ya kushuhudia mradi huo kubomoka kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Mbarali.Waziri wa kilimo,chakula na ushirika Mhandisi Christopher Chiza jana alikelwa na madudu katika ujenzi wa mradi
wa bwawa la Lwanyo Igurusi Wilayani mbarali
uliogharimu kiasi cha Sh3.077bilioni kujengwa kiwango cha chini na kuagiza
kuundwa kwa tume maalum itakayochunguza hali hiyo atimaye hatua kali kuchukuliwa
dhidi ya wahusika
Mradi wa ujenzi wa bwawa hilo ulianza kutekelezwa Machi
2010 chini ya ofisi ya umwagiliaji kanda
kwa kupata fedha kupitia mfuko wa
kuendeleza kilimo cha umwagiliaji Taifa (NIDF)na kujengwa na kampuni ya
Boimanda Modern Construction na kukamilisha kazi hiyo kwa mujibu wa mkataba
Desemba 2013 ambapo zaidi ya wananchi 6000 walitarajia kunufaika na mradai huo.
Akizungumza baada ya kufika katika bwawa hilo alisema
kuwa kutokana na hali hiyo mbaya serikali imepata hasara kubwa kwani mradi huo hauwezi kutumika na kwamba itachukua
hatua ya kutuma timu ya wataalam kuja
kufanya uchunguzi na ukaguzi wa kitaalam(Technical Oditing) na kuchukua hatua
kali za kisheria dhidi ya wahusika.
“Hii hali ni mbaya inaumiza kila mtu atakayefika hapa na
kuona kilichofanyika nilazima aumie hivyo hakuna atakayekubaliana na hili kwani fedha nyingi zimeteketea hapa na bwawa
hili haliwezi kutumika hivyo ni lazima
watu wawajibike hapa hata kama waliohusika wamestaafu lakini serikali haistaafu
hivyo itawafuata huko huko walipo”alisema
Alisema kuwa kazi itakayofanywa na timu hiyo ni
kuhakikisha wanaangalia michoro ya ujenzi wa mradi huo, utaratibu uliotumika
kumpata mkandarasi,jinsi malipo yalivyofanyika na kukagua uwezo wa mkandarasi.
“Nilazima huyu mkandarasi akaguliwe hivyo kwani sina
imani na uwezo wake hivyo naagiza wataalam kutoka bodi ya wakandarasi (CRB)
kuhakikisha wanamkagua mkandarasi huyu kwani alichotufanyia hapa ni hasara
kubwa kwa serikali lakini pia nikuwanyika wananchi wetu haki ya kupata maji kwa
ajili ya kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya nyumbani”alisema
Akijibu maswali ya
Waziri mkurugenzi wa kampuni hiyo ya ukanadarasi ya Boimanda, Nicholaus Mgaya
alisema kuwa kampuni yake ipo daraja la tatu
na kwamba mkataba wake umekwisha na alipoomba kuongezewa fedha zingine
kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo alikataliwa na wahusika.
Naye Mhandisi
kutoka ofisi ya umwagiliaji kanda Elibariki Mwendo alisema kuwa waligundua tatizo hilo la ujenzi chini ya
kiwango baada ya ujezi huo kubomoka
wakati tayari mkandarasi ameshamaliza mkataba wake na fedha zote ameshalipwa.
Alisema kuwa tatizo lililopo hapo ni maji kupita
sehemu siyo sahihi na kusababisha ujenzi wa tuta hilo kubomoka
na kwamba suala la kumtafuta mkandarasi lilifanywa na halmashauri ya Wilaya ya
Mbarali.
Awali akitoa taarifa kwa Waziri, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Abbas Kandoro alisema kinachomsikitisha
ni namna miradi inayosimamiwa na
ofisi ya umwagiliaji kanada kujengwa
chini ya kiwango.
”Hali hii ni mbaya sana kwa serikali yetu kwani wananchi
hawawezi kutuelewa fedha nyingi mabilioni ya shilingi kupotea bure na ujenzi wake unasikitisha kwani utaalam unanipa mashaka “alisema
0 comments:
Post a Comment