Pages

Thursday, August 28, 2014

KANDORO AIOMBA SERIKALI KUU KUMALIZA MGOGORO WA KAPUNGANA


 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro  akizungumza ofisini kwake na Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika  Mhandisi Christopher Chiza mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jana
.




Mbeya.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, ameipigia magoti Serikali kuu kuona uwezekano wa kumaliza mgogoro baina ya wananchi wa Kijiji cha Kapunga na Mwekezaji wa Shamba la Kapunga Project Wilayani Mbarali Mbeya.

Mgogoro huo umedumu zaidi ya miaka 10 ambapo inadaiwa mwekezaji wa shamba la Kapunga(Kapunga Rice Project) kuuziwa na serikali eneo lenye ukubwa wa hekta 7370 badala ya hekta  5500 ambazo ndizo wanakijiji walitoa kwa Nafco kwa ajili mradi maalum wa kuendeleza kilimo cha mpunga.

Akizungumza ofisini kwa mbele ya Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza,Kandoro alisema kuwa katika mgogoro huo
 wananchi ndio wanaoumia zaidi, hivyo ni lazima Serikali  kuhakikisha inaumaliza mgogoro kama ilivyo amuliwa.

“Ni muda mrefu sasa wale wakulima na wananchi wa kapunga wamekuwa katika mgogoro na mwekezaji na kuwa na matokeo mabaya ya mahusiano  baina yao, na kuwepo kwa  matukio ya kutoweka kwa amani yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara, hivyo ni vyema Serikali kupitia  wizara husika iliangalie  tatizo hili na kulimaza,” alisema Kandoro.

Ajibu hoja hiyo Waziri Chiza alisema kuwa anatambua kuwa eneo hilo la kijiji lilitolewa kimakosa na kwamba wananchi wanapaswa kupata haki yao kwa kuhakikisha mgogolo huo unamalizika.

“Ni kweli wakulima  ndiyo wanaoumia na suala hilo lilishaamliwa ni lazima fidia itolewe wahusika wanaolishughulikia kuangalia uwezekano wa kulimaliza,tufike mwisho huu mgogoro uishe”alisema

Alisema kuwa suala hili lilishatolewa uwamuzi lakini namana ya ulipaji wa fidia ndiyo changamoto kwani kuna jinsi utaratibu utaratibu unaotakiwa kufanyika katika kurudisha eneo la wananchi ambao ni pamoja na Mwekezaji kulipwa fidia ya eneo mbadala au kulipwa fidia ya fedha yasilimu.

0 comments: