IZZO B akiimba kwa hisia wimbo wake wa tumoghele huku akishangiliwa maelfu ya watu waliojitokeza kumshudia katika banda la Cocacola kwanza katika viwanja vya maonyesho ya nanenane jijini Mbeya
Meneja mauzo kanda yanda za juu kusini Rashidi Mgonja akimkabidhi pikipiki kiongozi wa timu ya Uyole baada ya kutwaa kombe la mashindano ya bodaboda Cup yaliyoandaliwa City Sign Ptomotion ya jiji mbeya
Watoto wakitoa burudani kabla ya kupanda IZZO B jukwaani na kuanza kutumbuiza
Maelfu
ya watu kutoka mikoa ya kanda ya nyanda
za juu kusini walijitokeza jana kumshuhudia Msanii wa tasinia ya muziki wa bongo
fleva Izzo B viwanja vya maonyesho ya nanenane jijini
Mbeya.
Msanii
huyo ambaye yupo mbeya kwa ajili ya onyesho
la Kilimanjari music tour linatotarjiwa kufanyika jijini Mbeya ,jana aliibuka ghafla jukwaani katika
banda la maonyesho la kampuni yaCocacola
na kuanza kuimba.
Baada ya
msanii huyo kupanda jukwaani na kuanza kuimba mashabiki na wapenzi wa muziki
huo waliokuwa katika mabanda mbali mbali katika viwanja hivyo walisogea kwa
kasi kubwa katika banda hilo na kuanza kusukumana huku wengine wakiwa na shauku
ya kutaka kumshika mkono.
Furaha ya
watu iliyoongezeka pale tu msanii huyo alipoimba wimbo wake unaoitwa “Tumoghele”
ambao ni wa lugha ya kabila la Wanyakyusa na “Naongea na Ridhiwani” kulazimika kushangilia kwa kupiga kelele ambazo zilivuta watu wengine
zaidi waliokuwepo katika viwanja hivyo vya maonyesho.
Akizungumza
mara baada ya kumaliza kuimba Izzo B alisema kuwa kutokana na kuwa ni mzawa wa Mbeya aliguswa
kufika katika viwanja hivyo mara baada ya kampuni ya Cocacola kumu mara tu baada ya kutua katika uwanja wa
ndege wa Songwe akitoa jijini Dar Salaam.
“Mimi ni mtoto
wa hapa Mbeya nawapenda watu wote wa mbeya hivyo nasikia furaha kuwa nyumbani
na daima siwezi kuwazarau kwani napenda amani na ninawaombea muendelee kuishi
kwa amani na upendo”alisema
Mwisho
0 comments:
Post a Comment