Pichani ni Mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) na
Wakakili wa kujitegemea Sambwee Shitambala(wa kwanza kulia) akifurahia jambo na wakili anayemtetea Tasco Luambano mara baada ya kufikishwa katika mahakama ya
hakimu mkazi Wilaya ya Mbeya kwa shitaka la kuingia kwa jinai na kujenga nyumba katika viwanja viwili eneo la Gombe Uyole jijini Mbeya mali ya Jaswinder Palsigh.
Mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) na
Wakakili wa kujitegemea Sambwee Shitambala jana amefikishwa katika mahakama ya
hakimu mkazi Wilaya ya Mbeya kwa shitaka la kuingia kwa jinai na kujenga nyumba.
Mwendesha mashitaka
wakili wa serikali Ahmed Stambuli alieleza mbele ya hakimu mkazi Wilaya ya
Mbeya Gilbert Ndeuruo alisema kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati Juni 18,2012 na Novemba 28,2013 katika eneo la Gombe Wilaya ya Mbeya mjini.
Alisema kuwa
mshitakiwa aliingia kwa jinai katika viwanja viwili namba 27 na 28 block
BB na kujenga nyumba kinyume na kanuni kifungu cha kanuni ya adhamu sura ya 16 ,mali ya Jaswinder Palsigh na
kumsababishia mlalamikaji maudhi.
Mshitakiwa
alikana shitaka hilo na mwendesha mashitaka
alieleza mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na
kwamba upande wa mashitaka hauna kipingamizi cha dhamana dhidi ya
mshitakiwa.
Ndeuruo alieleza mahakamani hapo kuwa dhamana
ipo wazi kwa mshitakiwa kuwa na mdhamini mmoja na kusaini bondi ya Sh1milioni
ambapo mshitakiwa alitimiza masharti hayo ya dhamana na kesi itakuwa Septemba
10,mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya awali.
Akizungumza
nje ya mahakama Wakiri anayemtetea
mshitakiwa huyo Tasco Luambano alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha kesi ya mteja wake kusikilizwa
katika mahakama ya Wilaya badala ya ardhi .
Aidha
alisema kuwa kesi hiyo inawahusu watu zaidi ya 400 “lakini cha kushangaza ni
mteja wangu pekee ndiye aliyefikishwa mahakamni hapa lazima kuna kitu ndani
yake kwani eneo analodaiwa mteja wangu kuingia kwa jinai lina nyumba za watu
zaidi ya 400 ambao wanaishi katika eneo hilo la viwanja vyote viwili”alisema
“Mteja wangu
alikamatwa jana na jeshi la polisi akiwa na watu wengine wanne ambapo wote kwa
pamoja walipewa dhamana na kutakiwa
kufika hapa mahakamani kwa ajili
kusomewa mashitaka yao lakini cha ajabu
wote wamefika lakini kasomewa
peke yake”
0 comments:
Post a Comment