Mbeya.Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya, limezuia maandamano ya waumini zaidi ya 500 wa Kanisa
la Moravian jimbo la kusini
Magharibi, yaliyotakiwa kufanyika leo, ya kushinikiza kufanyika mkutano
wa dharula wa Sinodi kwa lengo la kumaliza mgogoro wao uliodumu kwa
mwaka mmoja na nusu.
Kanisa la
Moraviani jimbo lakusini magharaibi limekuwa na mgogoro uliodumu zaidi ya mwaka
mmoja . mara baada kumvua madaraka Mwenyekiti wa jimbo hilo Nosigwe Buya na
kusimamishwa kazi wachungaji watano waliodaiwa kuhusika kumtetea
mwenyekiti huyo.
Akizungumza
na gazeti hili Mwenyekiti wa waumini hao
Frank Phiri alisema kuwa leo walipanga kufanya maandamano ya amani kwa lengo la
kushinikiza kufanyika kuitishwa mkutano wa Sinodi baada ya kuona viongozi wa
kanisa hilo hawafuati maamuzi na maagizo ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Mbeya.
“ Tulifiata
taratibu zote za kuomba kibali cha kufanya maandamano na tayari waumini
kutoka Wilaya zingine walishaingia tangu lakini cha kushangaza polisiwamtuzuia kufanya
hivyo kwa madai kuwa wanahofu vurugu zinaweza kutokea kitu ambacho tunaamini sisi kuwa siyo cha ukweli”alisema
Alisema
kuwa juzi siku ya ijumaa waliwasilisha
barua ya kuomba kibali katika ofisi wa
mkuu wa polisi wa Wilaya ya Mbeya (OCD ) ambaye alikiri kuipokea na kuwataka
warudi jumamosi ambapo walipofika
ofisini kwake walimkuta OCD huyo akiwa na katibu mkuu wa jimbo hilo.
“Hali hii inatufanya tukose imani na serikali yetu
kwani kama viongozi
wa kanisa wameshindwa kufuata maaagizo na maamuzi ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya kumrudisha
Mwenyekiti katika nafasi yake na
badala yake wanachukua uwamuzi mwingine wa kuwafukuza wachungaji watano sasa sisi waumini wanataka tuwe upande gani”alisema
Alisema kuwa
kama waumini wanaamini kuwa mkutano wa dharula wa Sinodi ndiyo unaweza kumaliza mgogoro huo na kuliweka kanisa pamoja kama katiba inavyoeleza ‘lakini hawa wenzetu viongozi hawataki
kuitisha Sinodi wakatgi ndiyo
iliyowaweka madarakani kufanya hivyo ni kuliua kanisa kwani mgogoro huu hauwezi kuisha bila ya
kuitishwa kwa mkutano huu.”alisema
Akieleza
sababu za kuzuia maandamano hayo kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa wamefanya hivyo
baada ya uchunguzi wao kubaini kuwa maandamano hayo yanaweza kuleta machafuko
kutokana na mgopgolo ulivyo.
“Kweli
tumezuia kufanyika kwa maandamano hayo
kwani kila upande kuna mambo wanataka kufanya mara huyu anataka hili,huyo
mwingine anataka hili hivyo tumeona ni vema tuwakatilie wote ili kuepusha machafuko ambayo yangeweza
kutokea”alisema
0 comments:
Post a Comment