Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Prof..Norman Sigallah King akimkaribisha mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi waliohudhulia hafla hiyo
Mkuu wa Mmoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa ameshika Boksi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kufanyia ukakarabati wa madarasa mengine manne katika shule hiyo ambapo zilipatikana jumla ya Sh 2.3milioni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi waliohudhulia hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu akizungumza katika hafla hiyo
Mwalimu Neema Sanga akisoma taarifa ya shule ya msingi ya Hassanga
Wanafunzi wa shule ya msingi Hassanga wakiimba kwaya katika hafla hiyo
Mmoja wa Wanafunzi wa shule ya msingi hassanga akiimba Ngonjera
Mkuu wa Mmoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa ameshika Boksi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kufanyia ukakarabati wa madarasa mengine manne katika shule hiyo ambapo zilipatikana jumla ya Sh 2.3milioni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi waliohudhulia hafla hiyo.
Mbeya.Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) jana limekabidhi vyumba vya madarasa vinne na jengo la
utawala kwa shule ya msingi Hassanga jijini Mbeya baada ya kuyafanyia ukarabati
uliogharimu Sh 31.5 milioni.
Akitoa
taarifa ya matengenezo ya shule hiyo
mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Mkurugenzi wa
mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu alisema
kuwa uwamuzi wa
kufanya ukarabati huo ulitokana
na maombi yaliyofanywa na kamti ya uongozi wa shule kwa kupitia afisa elimu
Wilaya yaliyopelekwa ofisi za NHC Mbeya
Februari mwaka huu.
Alisema kuwa kazi hiyo ilianza Aprili 19 na
kumalizika Agosti 20 mwaka huu ambapo jumla ya Sh. 22.7 milioni zitumika
katika ukarabati wa jingo la utawala
na Sh.8.8 zilitumika katika kukarabati
wa maradasa manne.
Mchechu alisema
kuwa baada ya kufika shuleni hapo na
kujionea ubovu wa vyumba vingine vya
madarasa hivyo shirika hilo pia lipo
tayari kumalizia madarasa mengine manne ambappo ujenziu huo utaanza rasmi
kesho.
Akizungumza
wakati wa kupokea madarasa hayo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema
kuwa wananchi na serikali wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na shirika
hilo katika shughuli za maendeleo.
“Ni lazima
tuwashukuru hawa ndugu zetu lakini pia tunakila sanbabu ya kuwaunga mkono hivyo
naanzisha harambee ndogo hapa ambapo kila mmoja achangia alichonacho ili tuweze
kuzikabidhi kwa mkurugenzi wa NHC kwa
ajioli ya kutumalizia madarasa yetu mengine
manne yaliyobaki”alisema
Akitoa
taarifa kwa niaba ya uongozi wa shule Mwalimu Neema Sanga alisema
kuwa shule hiyo inajumla ya vyumba vya madarasa 14 ambapo vine vipo katika hali nzuri
baada ya kukarabatiwa NHC huku vilivyobaki vikiwa na hali mbaya.
Alisema bado
shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa
madawati 150 na ukosefu wa uzio kwa ajioli ya ulinzi na usalama wa mali za
shule.
0 comments:
Post a Comment