Pages

Tuesday, October 21, 2014

CHANJO YA SURUA NA RUBELLA YAZINDULIWA WILAYANI ILEJE KIMKOA OKTOBA 18,2014

 Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Sinyamule  akitoa chanjo kwa mtoto wa miezi sita Chrisina Haonga katika uzinduzi wa chanjo ya Surua na Rubella kimkoa katika kijiji cha Chitete Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya

 Mwanafunzi wa darasa la Sita  Said Mgwenge katika shule ya msingi Chitete akiruka sarakasi katika uzinduziu wa chano ya Surua na Rubella katika kijiji cha Chitete Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya





 Mwakilishi wa Wizara ya Afya na maendeleo ya jamii akitoa salam katika uzinduzi huo

 Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mbeya Japhet Mhaye akitoa taarifa ya Chanjo ya Surua na Rubella katika uxzinduzi wa chanjo hiyo kimkoa katika kijiji cha Chitete Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk Seif Mhina akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chitete katika uzinduzi wa chanjo ya Surua Rubella katika kijiji cha Chitete Wilaya ya Ileje
 Mwakilishi wa katibu tawala Mkoa wa Mbeya (RAS) Akitoa salama katika uzinduzi huo
 Mwakilishi wa shirika la Afya Duniani (WHO) akitoa salam katika uzinduzi wa chanjo  ya Surua  na Rubella kimkoa  katika kijiji cha Chitete Wilayani Ileje
 Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya  Rosemary Sinyamule akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika Uzinduzi wa Chanjo ya Surua na Rubella Kimkoa  iliyofanyika katika kijiji cha Chitete Wilayani humo.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Chitete wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Rosemary  Sinyamule katika uzinduzi wa Chanjo ya Surua na Rubella katika kijiji ca Chitete Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya



ILEJE.  Mkoa wa  Mbeya  katika miaka miwili iliyopita umeweza kufikia lengo laTaifa la asilimia 90 ya kiwango cha utoaji  chanjo kwa  watoto wenye umri wa mwaka mmoja.Imeelezwa


Hayo yalisemwa na Mratibu wa  chanjo  Mkoa wa Mbeya Japhet Mhaye wakati wa uzinduzi wa  Chanjo ya Surua-Rubella na magonjwa yasiyopewa kipaumbele
 kimkoa, uliofanyika katika kijiji cha Ikumbilo, kata ya  Chitete wilayani  ya Ilej.


Alisema kuwa  mwaka 2012, lengo lilikuwa kuwachanja watoto 116,857, waliochanjwa walikuwa ni 111,658 sawa na asilimia 96 na mwaka 2013 lengo lilikuwa ni watoto 118,874 waliochanjwa walikuwa 110,782 sawa na asilimia 93.

 Mhaye alisema kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu, mkoa ulikuwa na lengo la kuchanja watoto 76,149  ambapo waliochanjwa ni 78,025, sawa na asilimia 102 ya lengo lililokuwa limewekwa kimkoa
.


 Mhaye alisema kampeni ya chanjo ni mkakati unaolenga
kudhibiti maradhi na kutokomeza ugonjwa wa Surua na Rubella
 ifikapo mwaka 2020 ambapo  tangu kampeni hizo zianze mwaka 1999, Tanzania
imeweza kudhibiti milipuko ya Surua.

Awalia akitoa taarifa ,Mratibu wa Huduma ya Afya ya Mzazi na Watoto wilayani Ileje, Anna Mwakipesile, alisema kuwa  Ileje, imepeleka maabara Kuu Dar es
Salaam mwezi septemba mwaka huu , sampuli za watoto watano wanaoshukiwa kuwa na Surua ambao   bado haijapata majibu ya matokeo ya kimaabara.


  Anna alisema wilaya hiyo iliwahi kukumbwa na ugonjwa wa
 Surua miaka ya 2003, ambapo kulikuwa na wagonjwa 15 wenye
 umri wa miaka mitano na watu wazima wapatao 126 na kuwa
mwaka 2007/2008,kulikuwa na wagonjwa wawili wa Surua wenye
umri wa chini ya mwaka mmoja.

Alisema kuwa Takwimu zinaonyesha kuwa Surua ilijitokeza kwa wingi katika
 kata za Mbebe na Chitete, hivyo kutokana na tatizo hilo
 wilaya imeendelea kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huo pamoja
na kupooza ghafla.


 Aidha alisema kuwa katika Wilaya hiyo,  wanatarajia
kuwachanja watoto chini ya miaka mitano wapatao 50,540,
 watoto wenye umri wa miezi 6-59 wapatao 20,968 watapatiwa
 Vitamin A, watoto 17,934 watapatiwa dawa za Mabendazole,
 wakati watu takribani 100,000 watapata dawa za Usubi na
 Minyoo ya tumboni kuanzia umri wa miaka mitano na
 kuendelea.

 




0 comments: