Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na wakulima na Wadau wa zao la Mpunga katika uzinduzi wa shirikisho la MTAYArF lillioundwa na makampuni matatu ya Mtenda Kyela Rice Supply,Tanseed International Ltd na YARA Tanzania Ltd katika ukumbi wa Mtenda jijini Mbeya.
Timu nzima ya shirikisho la MTAYArF wa kwanza ni mkurugenzi wa kampuni ya Mbegu ya Tanseed Mashauri,wa pili ni Mwenyekiti wa Bodi wa shirikisho hilo Stella Mutagwaba,Mkurugenzi wa Mtenda Kyela Rice Supply company Ltd George Mtenda na mwakilishi wa kampuni ya M,bolea ya YARA Tanzania
Mchele ukiwa tayari kwenye vifungashio tayari kwenda sokoni unaoandaliwa na kampuni ya Mtenda Kyela Rice Company Ltd
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mtenda Kyela Rice Company Ltd George Mtenda akizungumza katika uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Kampuni ya mbegu ya Tanseed,Mashauri
Baadhi ya Wakulima na wadau wa zao la mpunga wakiwa katika uzinduzi wa shirikisho hilo katika ukumbi wa mtenda jijini Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika picha pamoja na wadau na wakulima wa zao la mpunga kutoka Wilaya Tatu za Kyela,Mbarali na Momba Mkoani Mbeya
Mwenyekiti wa Bodi ya MTAYArF Stella Mutagwaba akitoa taarifa ya shirikisho hilo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akibadilishana mawazo na wenyeji wake
Baadhi ya wadau na wakulima wakifuatilia uzindiuzi wa shirikisho hilo
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameyataka makampuni yanayojishughulisha na
masuala ya kilimo ,yasijitengenezee
faida kubwa kwa mgongo wa wakulima kwa kuweka mikataba ambayo itamuumizi na
kumyonya Mkulima.
Kandoro alitoa kauli hiyo jana katika uzinduzi wa shirikisho
la makampuni matatu ya Mtenda Kyela
Rice Supply Company Ltd,Tanseed International Ltd na Kampuni ya Mbolea ya YARA Tanzania Ltd ambayo yameungana kwa lengo la kumpunguzia
gharama za uzalishaji na kumtengenezea faida mkulima wa zao la Mpunga.
Alisema kuwa
kumekuwepo na makamapuni mengi yanayofanya shughuli za kilimo katika mazao
mbali mbali lakini yamekuwa yakitengenezea faida kubwa kwa mgongo wa wakulima
na kumuacha mkulima kuendelea kuwa masikini.
“Ili kilimo
kweli kiwe na manufaa kwa mkulima ni lazima mikataba yenu na wakulima iwe
mizuri ambayo itamasidia na kumlinda
mkulima ili anaye aweze kupata faida
katika zao analozalisha na kuondokana na umasikini”alisema
Awali akitoa
taarifa ya shirikisho hilo
linaloitwa MTAYArF Mwenyekiti wa bodi Stella Mutagwaba alisema kuwa linatarajia kuwafikia wakulima
6000 wa zao la mpuga katika Wilaya ya Kyela,Mbarali na Momba ambapo
washirika watafanya kazi kwa pamoja katika myororo wa thamani wa zao la
Mpunga.
Alisema kuwa
pia shirikisho hilo litakuwa na jukumu la kukabiliana na changamoto za
masoko,uzalishaji mdogo na ubora usioridhisha wa zao la mpunga ambapo kila
mshirika atakuwa na jukumu maalum la kulingana na uzoefu wake kwenye mnyororo
wa thamani katika zao la mpunga.
Mutagabwa
alisema kuwa kamapuni ya Mtenda Kyela Rice Supply itakuwa na majukumu ya
kuingia mkataba na wakulima wa mpunga na
kununua , kukoboa na kuuza mchele na Tanseed International itakuwa na jukumu la kuzalisha na kusambaza
mbegu bora kwa wakulima kwa bei nafuu huku YARA Tanzania ikiwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa wakulima
kuhusu matumizi bora ya Mbolea kwa wakati sahihi na kiwango sahihi.
Kwa upande wake mwakilishi wa wakulima wa zao la mpunga katika wilaya hizo tatu, Oden Simkwai alisema kuwa wanakabaliwa na changamoto mbali mbali
ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya
kilimo bora , kukosa soko la uhakika,ubovu wa miundombinu ya barabara na uchakachuaji
wa pembejeo za kilimo.
Simkwai
alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto
hizo wakulima wa zao la Mpunga
wataendelea kutumia nguvu nyingi na gharama kubwa katika uzalishaji wa
zao hilo bila ya kupata faida yoyote na kuendelea kuwa masikini.
0 comments:
Post a Comment