Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Malenga akipokea mifuko ya saruji 950 yenye thamani ya Shilingi milioni 18 kutoka kwa mwakirishi wa mbunge wa jimbo la Kyela Dr Harrison Mwakyembe,Richard Kilumbo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za Sekonsari za Wilaya Kyela ambapo kila shule itakabidhiwa mifuko 50
Mwakilishi wa mbunge akitoa taarifa ya mchango huo kutoka kwa mbunge na kusema kuwa ni kuunga juhudi zinazofanywa na wananchi wa wilaya hiyo katika kuchangia maendeleo
KYELA .Mbunge
wa jimbo la Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ametoa mifuko ya Saruji 950 yenye
thamani ya Sh18milioni kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za
Sekondari Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi saruji hiyo mwakilishi wa mbunge Mwakyembe,Richard Kilumbo alisema kuwa lengo
la kutoa msaada huo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi wa Kyela
katika kujenga maabara katika shule za Sekondari.
“Rais
Kikwete alitoa agizo kwa kila shule ya
sekondari kuwa na maabara ambapo asilimia kubwa ya ujenzi wake unafanywa kwa
nguvu za wananchi hivyo mbunge ameona kuna umhimu wa kuungana mkono jitihada
zinazofanywa na wananchi wake kwa kuchangia saruji hiyo ili kuasidia
kukamilisha ujenzi huu”alisema
Aidha Kilumbo amewataka wananchi wa Kyela wanaoishi ndani na nje ya Wilaya hiyo
kuacha siasa za makundi na badala yake kushiriki kwa pamoja katika shughuli za
maendeleo ili kufanikisha zoezi hilo ambalo ni agizo la Rais.
“Tunapokuwa
katika shughuli za maendeleo siasa tuziweke pembeni na tuungane
kwa pamoja wanakyela wote katika shughuli
za maendeleo na uhakikisha Wilaya yetu inasonga mbele katika maendeleo,Kyela
kwanza Siasa baadae”alisema
Akizungumza
mara baada ya kupokea Saruji hiyo mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Malenga
aliipongeza hatua hiyo ya Mbunge Mwakyembe kujitolea saruji ambapo alisema kuwa
itasaidia kukamilisha ujenzi wa maabara
katika shule 19 ambapo kila shule itapata mifuko 50 ya saruji.
Alisema
kuwa wananchi wameonyesha juhudi za
ambapo hadi sasa wamefikia asilimia 80 bila
ya halmashauri kuchangia chochote
kwani ilikuwa na bajeti ya ujenzi
wa maabara mbili pekee hivyo nguvu kubwa imetumika ni ya wananchi wa Kyela.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya
Kyela alisema kuwa kyela ina
jumla ya shule za sekondari 22 ambapo
tatu ujenzi wake umekamilika na 19
ujenzi wake wamefikia silimia 80 uliofanywa nguvu za wananchi.
Alisema
kuwa ujenzi huo waa maabara hizo gharama yake ni Sh250milioni
ambapo wananchi wamechangia Sh100milioni,halmashauri Sh50milioni na
wadau watachangia Sh50milioni.
0 comments:
Post a Comment