Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho akiondoa magogo kwa ajili ya kupisha gari la wagonjwa mahututi likiwa limebeba mgonjwa kutoka Mbozi na kupelekwa hospoitali ya rufaa Mbeya,lakini baada ya kupita gari hilo magogo yalirudishwa tena barabarani.
Mbozi.Wananchi
wa kijiji cha luanda Wilaya ya Mbozi jana walifunga barabara kuu ya Mbeya Tunduma kwa saaa matatu, kwa
kupanga mawe na magogo mara baada ya mwenzao kugongwa na gari na kufa papo hapo.
Kutokana na
tukio hilo la kuziba barabara kuanzia saa 10:00 hadi saa 12:45 jioni kulisababidha kuwepo kwa foreni kubwa ya
magari na kuleta adha na kero kwa
wasafiri na magari yanayotoka na kuingia ndani ya nchi.
Barabara
hiyo hutumiwa na nchi za
Zambia,Kongo,Zimbabwe Botswana na
Afrka Kusini kupitia mpaka wa Tunduma
Wilayani Momba ambapo kuna magari
ya aina mbali ikiwa ni pamoja na maroli ambayo yalikuwa yamekwama katika eneo
hilo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti katika eneo hilo la tukio baadhi ya wananchi hao walisema
kuwa matukio ya ajali ya watu kugongwa yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika
eneo hilo kutokana na magari kuwa na na mwendo kasi.
“Hivi juzi
Oktoba 28 mwaka huu aligongwa mama yetu hapa na alifariki dunia papo hapo lakini
alipita mkuu wa wilaya ya Mbozi Michael
Kadege na kutuahidi kuwa baada ya siku tatu yatajengwa matuta katika eneo hili
lakini hakuna kilich ofanyika na leo amegongwa mtu mwingine hili halikubaliki”alisema
mkazi mmoja wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina Elias Simbeye
Simbeye
alisema kuwa wameamua kuziba barabara ili kuikumbusha serikali kuwa matuta
yanayatakiwa haraka katika eneo hilo ili kuweza kuokoa maisha ya watu kutokana
na kugongwa na magari mara kwa mara katika eneo hilo.
Alisema kuwa
eneo hilo lina miteremko mkari kwa pande zote mbili lakini magari yamekuwa
yakitumia mwendo kasi bila ya tahadhari kutokana na kijiji hicho kuwa na watu
wengi ambao wamekua wakivuka ng`ambo ya pili kwa ajili yakufuata mahitaji
Sokoni.
Kwa upande
wake Afisa mtendaji wa kata ya Luanda Blaya Msongole alisema kuwa wananchi
wamepatwa na hasira kutokana na ahadi aliyokuwa ameitoa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi
hivi karibuni ilipotokea ajali ambapo pia walitaka kufanya tukio kama hili.
“Mkuu wa
Wilaya alipita hapa na kuwaomba wananchi watulie huku serikali Wilaya ikifanya
jitihada za kuhakikisha matuta yanawekwa hapa baada ya siku tatu kitendo
ambacho hakijafanyika hivyo ili ndilo linatupa shida hapa”alisema
Jeshi la
polisi Mkoa wa Mbeya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo askari wake walifungua barabara hiyo bila kutumia nguvu na kufanikiwa magari hayo
kuanza kupita majira ya saa 12:45 jioni.
0 comments:
Post a Comment