Diwani wa kata ya Chiwezi (CCM) Emmanuel Punte Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya aliyenyosha mkono akirushiana maneno na Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka na kusababisha kutaka kurushiana ngumi katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo.
Diwani wa kata ya Mkulwe wa (CCM) ,Mathew Chikoti akimsihi Diwani wa kata ya Chiwezi (CCM) Emmanuel Punte kuacha malumbano ndani ya kikao cha baraza la madiwani
Momba:Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Momba jana nusurawarushiane makonde ndani ya kikao cha baraza la madiwani baada yakutokea malumbano makali ya kutaka kuvunjwa kamati mbali mbali nakuteua wajumbe wapya.
Vurugu hizo zilianza mara baada ya kutolewa hoja na Diwani wa kataya Mkulwe wa CCM ,Mathew Chikoti ya kuwa utaratibu uliotumikakatika kuteua wajumbe hao haukufuata kanuni za baraza hilo kutokanana maelekezo ya serikali.
“Kutokana na elimu tuliyopewa na maboresho ya kuzijua kanuni mbalimbali yaliyofanyika hivi karibuni tumebaini kuwa ni mambo mengi ambayo meza mmekuwa mkituficha hivyo hata utaratibu uliotumika katika kuteua
wajumbe wa kamati haukuwa sahihi kwani haukufuata kanuni za barazaletu”alisema diwani Chikoti
Hoja hiyo ilipingwa na Mwenyekiti wa halmashauri Bernad Sicholongwealiyekuwa akiongoza kikao hicho hali iliyosababisha kutokea kwa mvutano mkali na kufikia madiwani kurushiana lugha chafu ndani ya kikao hicho
Hali iliendelea kuwa mbaya mara baada ya Diwani wa kata ya
Tunduma(CHADEMA) Frank Mwakajoka ambaye aliomba mwongozo kutoka kwa mwenyekiti ambapo hoja hiyo ilipingwa vikali na diwani wa kata yaChiwezi(CCM) Emmnuel Punte ambapo alisema kuwa diwani huyo hanauwezo wa kutoa mwongozo huo hivyo na Mwenyekiti hawezi kumsikiliza.
Diwani huyo wa Chiwezi alimtaka Mwenyekiti kutovunja kamati hizo nakuendelea na baraza”kwani mimi tangu nimechaguliwa sijawahi kuingiakatika kamati ya fedha hivyo tuacheni tuendelee kuwepo katika kamatihii”alisema
Baada ya kauli hiyo ndipo madiwani hao wakaanza kurushiana maneno na
hata kufikia kutaka kurushiana makonde hadi hapo mwenyekiti alipoamua kumtoa nje diwani huyo wa kata ya Chiwezi
Pamoja na kumtoa diwani huyo nje bado hali iliendelea kuwa si shwari ndani ya baraza hilo ambapo madiwani wengine wa CCM waliendelea kumtuhumu mwenyekiti wao kuendesha kikao hicho kibabe ambapowaliendelea kumsisitiza kuwa aendeshe kikao hicho kwa kufuata kanuni.
“Mwenyerkiti unachokifanya hapa ni kutuburuza hatuwezi kuendelea nakikao hicho hadi hapo utakapotoa majibu ya kuvunja kwa kamatitunaomba utusomee kanuni na uendeshe kikao kwa kufuata kanunihizo”alisema diwani wa Nkangamo (CCM)Winston Simwelu
Hali hiyo ilianza kuwa tulivu mara baada ya afisa utumishi wa
halmashauri ya wilaya hiyo Ameliye Mfugale kusoma kanuni kuwa kama wajumbe watakuwa hawajaridhika na uteuzi wa wajumbe wakamati halmashauri ianweza kuvunja kamati hizo na kufanya uteuzi upya wakati wowote endapo kama wasioridhika watafikia theruthi mbili.
Baada ya afisa utumishi huyo kueleza kanuni hiyo ndipo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo Anton Mwantona aliposimama na kueleza kuwa ataitisha kikao maalumu kwa ajili ya kuvunja kamati hizo na kuteua wajumbe wapya endapo kama theluthi mbili za wajumbe zitafikiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Momba Abihudi Saidea alisema kuwaanashangazwa na hatua ya madiwani kulumbana katika kikao cha baraza lamadiwani na kuwataka kuimarisha ushirikiano katika kuleta maendeleo.
Alisema kuwa kikao hicho kinapaswa kuendeshwa kwa kufuata kanuni nasheria za baraza la madiwani ili kuondoa migongano mbayo inawezakutokea wakati kikao hicho kinaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment