Meneja wa GEFP Mkoa wa Mbeya Ramadhan Sossora akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Mwandishi wa habari wa Bomba FM na mratibu wa hafla hiyo akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mfuko GEFP
Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo
Meneja Masoko wa GEFP,Aloyce Ntukamanzina akitoa taarifa ya uetekeleza katika hafla hiyo
Meneja Masoko Aloyce Ntukamanzina akisikiliza kwa makini maswali ya waandishi wa habari katika hafla hiyo
MBEYA .Mfuko
wa mafao ya kustaafu (GEPF) umefanikiwa kukusanya Sh37.29bilioni kutoka kwa
wanawachama wake 76,000 katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2004 hadi Juni
2014.
Hayo yalisemwa jana na meneja masoko wa GEP, Aloyce
Ntukamanzina katika uzinduzi wa ofisi ya
tisa ya nyanda za juu kusini katika eneo
la uhindini jijini Mbeya.
Ntukamanzina alisema kuwa mfuko huo umekuwa
ukifanikiwa mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2004 ilikuwa na wanachama 16,131 na kufanikiwa
kukusanya Sh5.1bilioni.
Alisema kuwa
katika kipindi hicho cha miaka 10 mfuko
huo pia umeweza kulipa mafao kwa wanachama wake 76,000 zaidi ya Sh12.73bilioni wakati
mwaka 2004 walilipa mafao Sh67.1milioni kwa wanachama 16,131.
Aidha alisema
kuwa mfuko huo pia umeweza kupata
mafanikio makubwa katika mpango wa hiari
wa kujiwekea akiba katika kipindi cha
miaka mine tangu ulipoanzishwa mwaka 2010.
Alisema
kuwa katika kipindi hicho wameweza
kukusanya zaidi ya Sh5bilioni kwa wanachama 35,481 waliosajiliwa na kwamba
mpango huo unawahusu wanachama walioajiriwa,wasioajiliwa na wafanyabishara.
Meneja huo
alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzisha mpango huo maalum ni kuwawezesha
watanzania wengi kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kwani uwiano wa mifuko ya
pensheni iliyopo nchini idadi ya wanachama wanaohudumiwa na mifuko hiyo
haiendani.
“Tanzania
tuna watu zaidi ya 48milioni na tunamifuko ya sita lakini wanaopata huduma
katika mifuko hii ni watanzania 1.8milioni pekee,kwa hiyo tunaona jinsi kunachangamoto kubwa kwa mifuko hii ya
pensheni kuwafikia watanzania walio wengi”alisema
0 comments:
Post a Comment