Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kununua kahawa Mkoani Mbeya (CMS)Yogesh Modhwadia akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya
Mwakilishi wa kampuni ya kunuanua kahawa Mkoani Mbeya CMS Ephrahimu Kasanga akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari Wilayani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kununua kahawa Mkoani Mbeya (CMS)Yogesh Modhwadia akielezea kazi zinazofanywa na kampuni yake katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe wakati kampuni hiyo ikikabidhi msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa maabara
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crisipin Meela akifurahia jambo baada ya kupokea taarifa ya Kampuni ya CMS ya kukabidhiwa mifuko 60 ya Saruji
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mwenye shati nyeupe akiwa ameshikana mkono na mwakilishi wa kampuni ya CMS baada ya kukabidhiwa mifuko 60 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari
RUNGWE.Wananchi
Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wametakiwa kuwapuuza wanasiasa ambao wanawashinikiza
kugoma kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari ili kuepuka watoto wao kufanya vibaya katika
masomo ya sayansi.
Kauli hiyo
imetolewa jana na mkuu wa Wilaya ya
Rungwe Crispin Meela alipokuwa akipokea mifuko 60 ya Saruji yenye thamani ya
Sh1.2milioni kutoka kwa Kampuni ya ununuzi wa kahawa mkoani Mbeya (CMS )ikiwa ni mchango wa ujenzi
wa maabara katika shule za Sekondari Wilayani humo.
Meela
alisema kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipita kwa wananchi na
kuwashinikiza wagome kuchangia ujenzi wa maabara na kusababisha baadhi ya
maeneo utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa maabara kwa kila shule
kusuasua.
“Katika suala
hili la ujenzi wa maabara siyo ni la
Serikali pekee bali linahitaji nguvu za wananchi hivyo wananchi wanatakiwa kuwapuuza hawa
wanasiasa wetu ili kuweza kukamilisha agizo la Rais,hivyo sioni sababu ya
wanasiasa kutaka kutuharibia utaratibu tuliojiwekea na wananchi katika ujenzi
wa maabara zetu”alisema
Meela alisema kuwa kuhusu ujenzi wa maabara umefikia asilimia
90 na kwamba wilaya hiyo ina jumla ya
shule za sekondari 43 na halmashauri ya Rungwe imechangia Sh.90milioni na
Busokelo imechangia Sh101milioni katika ujenzi huo ikiwa ni pamoja na ununuzi
wa samani.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi Saruji hiyo
mwakilishi wa kampuni ya CMS Ephraim Mwakabaja alisema kuwa mbali ya kampuni hiyo kununua kahawa kwa wakulima wa
Wilaya ya Ileje,Mbeya vijijini,Mbozi na Rungwe pia inajihusisha katika kuchangia maendeleo ya
wananchi katika maeneo hayo.
Alisema
kuwa kama kampuni wanafahamu umuhimu wa maabara katika shule za
Sekondari hivyo wameamua kuchangia saruji hiyo ili kuwasaidia watoto wa wakulima wa kahawa
kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
Aidha
alisema kuwa mbali ya mchango huo wa
Saruji kwa Wilaya ,kampuni hiyo imeweza kuchangia ujenzi wa maabara katika
shule ya sekondari Bujinga kwa kutoa fedha tasilimi Sh200,000 .
0 comments:
Post a Comment