MBEYA.Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema) amesema kuwa dhamira iliyopo kwa chama hicho ni kuhakikisha kinatengeneza historia ya kukalia kiti cha
Umeya ndani ya halmashauri ya jiji la
Mbeya.
Sugu alitoa kauli hiyo juzi kwa nyakati
tofauti wakati akiwahutubia wakazi wa mitaa mbalimbali ya jiji
alipofanya mikutano ya hadhara ya kampeni za chama hicho na kuwanadi
wagombea nafasi za uenyekiti wa mitaa hiyo kupitia chadema.
“Hivyo uchaguzi huu wa serikali za
mitaa ni muhimu kwa chama chetu kufanya vizuri ili kuweza kutimiza lengo la
kuliongoza jiji la Mbeya”
Alisema kuwa ili waweze kuchukua kiti cha umeya chadema wanahitaji kuchukua mitaa isiyopungua
140 hadi 150, na kwamba cha hicho kikifanikiwa kuchukua idadi hiyo kitakuwa kimejiwekea
mazingira ya kushinda nafasi ya umeya
katika halmashauri ya jiji hilo.
“Msingi wowote wa uongozi bora unatoka
ngazi ya Serikali za mitaa, na wenyeviti wa mitaa ndio dira ya kuleta maendeleo
au kudumaza katika eneo husika hivyo wananchi wasijefanya makosa
wala kupuuzia uchaguzi huo na wahakikishe wanawachagua viongozi wenye uchu wa
maendeleo”alisema
Aidha alisema kuwa amekuwa akikumbana na changamoto mbali mbali
ikiwa ni pamoja na uwepo wa vikwazo kutoka kwa wenyeviti wa CCM, katika utekelezaji
wa ahadi zake kwa wapiga kura wake.
“Mfano mzuri ni huu, kuna fedha za
wananchi wa kata ya Nsalaga ambazo nilizilielekeza kwa ajili ya ujenzi wa
mradi wa mabwawa ya kufugia samaki lakini wenyekiti wa mitaa
ya kata hiyo wanapinga kupokea fedha hizo kwa sababu ambazo hazina msingi
wowote”alisema .
0 comments:
Post a Comment