MTOTO Justa Mwasomola akiwa na baba yake mzazi Ephrahimu Mwasomola
RUNGWE .Mtoto Justa Mwasomola
mwenye umri wa miaka tisa mkazi wa kijiji cha Masebe wilaya ya Rungwe
Mkoani Mbeya anaomba msaada wa fedha kwa ajii ya kupatiwa matibabu ya
uvimbe uliopo juu ya pua nakusababisha kushindwa kuendelea na masomo.
Akizungumza kwa uchungu baba
mzazi wa mtoto Ephrahimu Mwasomola alisema kuwa tatizo hilo lilianza mara
baada ya kuzaliwa mtoto huyo mwaka 2005 ambapo kilikuwa kama
kiupele kidogo katikati ya jicho na jicho.
“Kijiupele hicho kianza
kuongezeka kadri anavyoendelea kukua ambapo baadae baada ya kufikisha miezi
sita ndipo nilipompeleka katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe ya
Makandana kwa ajili ya kupatiwa matibabu”alisema
Alisema kuwa mara baada ya kufika
katika hospitali hiyo ya Wilaya Daktari alimwambia kuwa hospitali hiyo haina
uwezo wa kuondoa huo uvimbe na ndipo walipomuandikia barua ya
kwenda katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
“Mwaka huo huo 2005 tulipelekwa
rufaa mbeya na muuguzi wa wa hospitali ya makandana na baada ya kufika
huko mtoto akafanyiwa uchunguzi ambapo madaktari wa rufaa nao wakasema
hawanauwezo wa kuondoa huu uvimbe hivyo natakiwa kwenda hospitali kubwa ya
Muhimbili”alisema
Baba huyo alieleza kuwa alikatishwa
tamaa na hatua hiyo ya madktari wa rufaa mbeya kumwambia aende muhimbili
kutokana na hali yake ya kifedha kuwa duni kwani hata ndugu zake
alipowashirikisha suala hilo walidai kuwa pia nao hawana uwezo kifedha za
kumsaidia mtoto wake kwenda Muhimbili kupatiwa matibabu.
Alisema kuwa aliamua kurudi
kijijini kwake na kuendelea na maisha mengine huku akimuacha mtoto huyo
na uvimbe huo ukiendelea kuongezeka hadi hapo mwaka jana alipokutwa
na mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela njiani akielekea shule.
“Baada ya mkuu wa Wilaya kumuona
nilifikishiwa taarifa na Mwalimu wa shule ya msingi mapambano kuwa nahitajika
kwa mkuu wa wilaya ndipo nilipofanya hivyo na kufika ofisini kwake lakini
sikumkuta na nikaamua kurudi nyumbani hadi hivi juzi aliponitafuta
tena na kunitaka nifike ofisini kwake na mtoto”alisema
Akizungumzia tatizo lake huku
akitoa machozi Mtoto Justa alisema kuwa anajisikia uchungu sana kwa kuwa
na hali hiyo kwani kwa sasa hajawezi hata kwenda shule kutokana na wanafunzi
wenzake kumcheka na kujiona ni tofauti na wenzake.
“Wenzangu kwa sasa wanaendelea na
masomo wapo darasa la kwanza lakini mimi siwezi kwenda shule tena kwani mwaka
jana nilipokuwa chekechea wenzangu walikuwa wananicheka na wengine kunishangaa
wananizunguka wengi mimi nakuwa katikati naomba mnisaidie kuondoa
hiki kitu usoni kwangu”alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Rungwe Crispin Meela alisema kuwa alishitushwa na hali ya mtoto
huyo baada ya kumuona njiani akiwa anaenda shule na ndipo alipoamua kumfuatilia
ili kujua kama kuna matibabu yoyote ambayo amewahi kupata.
Meela alisema kuwa mtoto huyo
ameendelea kukaa na uvimbe huo nyumbani kwa muda wa mika tisa bila kupata
matiabu yoyote na kwa kadri unavyoonyesha unaendelea kuongezeka hivyo
inawezekana tatizo hilo likawa kubwa hivyo ni vema serikali na wasamalia
wema wakajitokeza kumsaidia mtoto huyo aweze kufika muhimbili kwa ajili ya
kupatiwa matibabu .
Alisema kuwa tangu alipoambiawa
anatakiwa kwenda muhimbili ni muda wa miaka tisa sasa hivyo anahitaji kuanza
kufuata taratibu upya kuanzia hodspitali ya Wilaya hadi Rufaa ili aweze
kupatiwa barua ya kwenda muhimbili.
0 comments:
Post a Comment