Mratibu wa miradi wa kampuni ya Mtenda Kyela Rice ya Mkoani Mbeya Idd Kinyaga akitoa maelezo mbele wakulima wa zao la mpunga Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya katika kikao cha pamoja na kupitia mkataba .
Ofisa kilimo,ushirika na umwagiliaji Wilaya ya Kyela Joseph Njau akitoa maelezo kwa wakulima wa zao la mpunga wilayani humo
Wakulima wa zao la Mpunga wilaya ya Kyela wakiwa katika picha pamoja na maofisa kutoka Kampuni ya Mtenda Kyela Rice baada ya kukubaliana kuingia mkataba wa kukopeshwa pembejeo
Moses Mwamaso akizungumza kwa niaba ya wakulima wa zao la Mpunga Wilaya ya Kyela wakati wa kupitia mkataba wa kukopeshwa pembejeo za kilimo kutoka kwa kampuni ya Mtenda Kyela Rice
Kyela.Wakulima 1200 wa zao la Mpunga Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya
wameingia mkataba na Kampuni ya mtenda kyela Rice Supply kwa ajili ya
kukopeshwa pembejeo za kilimo ikiwa ni pamoja na mafunzo ya kitaalam ya kuboresha kilimo cha zao hilo.
Akizungumzia mkataba huo kwa niaba ya wakulima hao Moses
Mwamaso alisema kuwa utawawezesha kupata
mbegu bora na mbolea ziatakazowasaidia kuongeza uzalishaji na kupata mavuno mengi na yenye ubora utakaoleta ushindani sokoni.
“Mpunga wa kyela unapendwa na watu kutoka maeneo mbali mbali
lakii tatizso kubwa lililopo ni kuwa tumekuwa tukillima zao hili bila ya mbolea
na hivyo kuambulia mavuno kidogo ambayo hayamsaidia mkulima kubalisha maisha
yake”alisema
Alisema kuwa wakuima
wengi wamekuwa wakitegemea mbolea ya ruzuku kutoka serikalini ambayo
haitoshelezi kwa wakulima wote,hivyo mkopo huo utaweza kuwasaidia kuongeza uzalishaji kutokana na malipo yake kufanyika
baada ya mavuno.
Awali Mkurugenzi wa kampuni
hiyo George Mtenda alisema kuwa wakulima hao watapata mkopo kupitia vikundi
vyao na kwamba liba yake itakuwa ni
asilimia tatu ambayo watarejesha pamoja na mkopo huo baada ya mavuno.
“Katika mkataba
huu tumekubaliana kuwa tutatoa mafunzo kwa wakulima wahusika wa
mkopo huo, ya kuwazesha kulima mpunga wenye ubora, kwani katika marejesho ya
mkopo wao yatakuwa ni mpunga ambao unaubora,ambapo tutapigiana hesabu kwa Zaidi
ya bei iliyopo sokoni kwa wakati huo ”alisema
Mtenda alisema kuwa
ni lazima itumike Zaidi ya bei iliyopo sokoni ili kumsaidia mkulima
kupata faida na kumwezesha kuinua kipato chake na kuboresha maisha yake
kwa kuweza kumudu mahitaji yake ya kila siku ikiwa ni pamoja na kupeleka shule
watoto wake
Kwa upande wake afisa
kilimo,ushirika na umwagiliaji Wilaya ya
Kyela, Joseph Njau alisema kuwa kwa sasa uwezo wa uzalishaji wa zao la mpunga katika wilaya hiyo ni tani 3.8 kwa hekta moja kwa kilimo cha kutegemea mvua pekee huku kilimo cha umwagiliaji ni tani 4.5 kwa
hekta moja.
Njau alisema kuwa kama wakulima hao watafuata maelekezo ya mafunzo hayo na
kuboresha kilimo cha zao hilo wataweza kuongeza uzalishaji na kufikia tani 4.5
hadi 5.5 kwa hekta na mazao yao kuwa na ubora ambao unakubalika sokoni.
0 comments:
Post a Comment