Pages

Saturday, August 8, 2015

MIZENGWE YAIBUKA BAADA YA KURA ZA MAONI CCM MBEYA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya kwenye kura za maoni Fatuma Kasenga akijinadi mbele ya wananchi  kuomba ridhaa ya chama hicho kwenye moja ya kampeni za chama hicho hivi karibuni

Sambwee Shitambala mmoja wa wabunge 16 wa CCM aliongoza katika kura za maoni kwenye kinyang'anyiro ndani ya chama.

Mgombea wa CCM kwenye kura za maoni za ubunge wa jimbo la Mbeya Amani Kajuna akijiorodhesha katika daftari maalumu la wagombea kwenye ofisi za CCM wilaya Mbeya hivi karibuni
Ulimboka Benjamin Mwakilili mmoja wa wagombea waliojitosa kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kati ya wagombea 16 waliojitokeza 



Charles Mwakipesile akizungumza na wanachama wa chama hicho siku alipochukua na kurejesha fomu za kuwania kinyang'anyiro hicho jijini Mbeya.

Jackson Numbi mmoja kati ya wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hiyo jijini Mbeya.

Na Ripota Wetu, Mbeya
SIKU chache baada ya CCM kumaliza zoezi la upigaji wa kura za maoni ndani ya chama hicho jimbo la Mbeya mjini zimeibuka tuhuma kwamba mmoja wa wagombea Ubunge wa chama hicho amewanunua viongozi wa chama wilaya kwa nia ya kutoa maoni ya kukubalika kwake ndani na nje ya chama.
Taarifa za ndani kutoka kwa baadhi ya wanachama hicho ambao hawakupenda kutajwa majina yao walisema kuwa vikao vya chama vinaendelea ili kutoa upendeleo kwa mmoja wa wagombea kwa madai ya kukubalika kwake ndani na nje ya chama.
Jumla ya wagombea 16 wa CCM walijitokeza katika kuwania nafasi ya Ubunge wa jimbo hilo ambapo walitembea katika kata 36 na kujinadi mbele ya wanachama na Agosti Mosi wanachama walipiga kura na kuwapitisha wagombea wanaowahitaji.
Akizungumza kwa njia ya simu juu ya kuwepo kwa madai hayo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya Ephraim Mwaitenda ambaye kwa muda huo alidai yupo katika kikao alisema kuwa kikao hicho kimeketi ili kutathmini wagombea wote walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho.
‘’Ni kweli tupo kwenye kikao cha tathmini baada ya kura za maoni, tunaangalia kukubalika kwa mgombea ndani na nje ya chama, hatupendi kurudia makosa ya mwaka 2010, mwaka ule tulimpitisha mgombea Benson Mpesya aliyeongoza kwa kura lakini matokeo yake tukashindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu,’’alisema.
Alisema wanafanya tathmini ya kina kuangalia mgombea anayekubalika kwa vijana na kwenye chama hatimaye watatoa maoni na mapendekezo yao na kuyapeleka kwenye vikao vya juu vya chama.
‘’Kura zilizopigwa hazitabadilishwa kila mgombea atabaki na kura zake kama zilivyopigwa kwenye kura za maoni, hapa tunapitia uwezo wa mgombea mmoja mmoja ndani ya chama na nje ya chama,’’alisema.
Hata hivyo Mwaitenda baadaye alikata simu na kusema kuwa bado anaendelea na kikao na hivyo atafutwe baadaye baada ya kumalizika kwa kikao.
Wagombea watatu walioongoza katika kura hizo dhidi ya wenzao 16 ni Sambwee Shitambala(4,633), Amani Kajuna(4,409),Charles Mwakipesile(2,316).

0 comments: