Pages

Thursday, December 17, 2015

WACHINA JELA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA FARU




MAHAKAMA ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Mbeya imewahukumu kwenda jela miaka 20 watalii  wanne raia wa  nchini China ambao wamekutwa na nyara za serikali pembe za Faru 11 zenye thamani ya dola za kimarekani 418,000 zenye uzito wa kgm 53.3 kinyume cha sheria.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua takribani saa 4 kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 9:45 alasiri Hakimu wa mahakama ya hakimu mfawidhi mkoa wa Mbeya Michael Mtaite alisema kuwa adhabu hiyo ya kifungo cha miaka 20 inakwenda pamoja na kulipa faini zaidi ya dola 800.
Hakimu Mtaite amesema kuwa washitakiwa hao  Song Lei(32)Xiao Shaodan(29)Chen Jianlian(33)na Hu Liang kwa pamoja walikutwa na nyara hizo pembe za Faru Novemba 6 kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi, Kasumulu wilayani Kyela wakati wakijaribu kuvuka mpaka kuingia nazo nchini.
Amesema washitakiwa hao ambao walikuwa na gari aina ya Toyota Hilux Surf yenye namba za usajili T 103 DER ambapo katika gari hilo walitengeneza sanduku maalumu la chuma chenye kufuri na bawaba na kuhifadhi pembe hizo kwa nia ya kuziingiza nchini.
Hakimu Mtaite ambaye alikuwa akisoma hukumu hiyo kwa Kiswahili huku ikitafsiriwa kwa lugha ya Kichina na mkalimani Mtanzania Manifred Lyoto amesema kuwa raia hao wa China wanatiwa hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Aidha amesema kuwa mahakama imezingatia kiini cha kosa na kujiridhisha kuwa washatikiwa walipanga kutekeleza kosa la jinai kwa kuingiza nchini nyara za serikali pembe 11 za Faru bila kibali,kutekeleza kuingiza pembe hizo nchini na kukutwa nazo wakizimiliki bila kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyama pori.
Awali kabla ya kutoa hukumu hiyo wakili wa serikali Wankyo Simon ameitaka mahakama hiyo kutoan adhabu kali dhidi ya washtakiwa kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu na ujangiri dhidi ya wanyama pori walio hatarini kutoweka.
Wakili Simon amesema kuwa kitendo cha washtakiwa hao pia kinakiuka mkataba wa Kimataifa unaolinda na kuhifadhi wanyama walio mbioni kutoweka ikiwa ni pamoja na  sheria za Uhujumu uchumi na kuitaka mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa raia wengine wanaosingizia kuingia nchini kwa ajili ya utalii.
Amesema raia hao waliingia nchini kwa nia ya kufanya utalii na kuwa badala yake wamekuja kufanya uhalifu jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa kuwa ni mfano kwa adhabu kali ambayo mahakama inapaswa kutoa dhidi ya washtakiwa.
Naye Wakili wa upande wa utetezi Ladslaus Rwekaza amesema kuwa mahakama iangalie uwezekano wa kuwapunguzia adhabu hasa ikiangaliwa mahusiano ya urafiki baina ya Tanzania na China na kuwa kutokana na kosa hilo kuwa ni la kwanza na kutokuwa na historia ya makosa ya aina hiyo kwa washtakiwa, mahakama itoe adhabu kwa jicho la huruma.
Hata hivyo Hakimu Mtaite ambaye aliahirisha hukumu hiyo kwa saa nzima amesema mahakama inawahukumu jumla ya miaka 38 jela kwa makosa matatu ambapo adhabu hiyo itakwenda kwa pamoja na kutumikia jumla ya miaka 20 jela huku wakitakiwa kulipa faini ya dola zaidi ya 800,000.

Thursday, December 10, 2015

MAGUFULI ATEUA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam jana Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Jana Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli anatangaza baraza la mawaziri wa Jamhuri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tuwe pamoja kulifahamu baraza letu.
Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua baraza la mawaziri, baada ya kusubiri kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.
Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri.
Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.
BARAZA LA MAWAZIRI
WIZARA OFISI YA RAIS,TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA.
Mawaziri - George Simbachawene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.
WIZARA  OFISI YA MAKAMU WA RAIS MUUNGANO NA MAZINGIRA
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina



OFISI YA WAZIRI MKUU SERA,BUNGE,KAZI VIJANA, AJIRA NA WALEMAVU
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.
WIZATA KILIMO MIFUGO NA UVUVI
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha
WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO
(waziri Bado hajapatikana).
Naibu Waziri – Inj. Edwin Amandusi Ngonyani



WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
(Waziri Bado hajapatikana).
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi


WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
Waziri - Prof. Mwijarubi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.



WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Waziri - Harrison Mwakyembe
WAZIRI WA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,KIKANDA NA KIMATAIFA.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.



WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Waziri - Dk. Hussein Mwinyi


WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Waziri - Charles Kitwanga.



WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula



WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
(Waziri Bado hajapatikana).
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani



WIZARA YA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI.
Waziri Charles Mwijage.



WIZARA YA ELIMU,SAYANSI TEKNOLOJIA NA UFUNDI
(Waziri Bado hajapatikana).
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya
WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Waziri - Ummy Mwalimu
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala



WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,WASANII NA MICHEZO
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.
WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela
( KWA HISANI YA JOSEPHAT LUKAZA BLOG)


Sunday, December 6, 2015

WCS & USAID ILIVYOWAWEZESHA WANA TAJATI KUTEMBELEA HIFADHI YA KITULO

WCS chini ya Ufadhili wa USAID iliwawezesha chama cha wanahabari za Utalii na Uwekezaji Tanzania TAJATI kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo



Mbunge wa Makete Dkt Norman Sigalla alipata firsa ya kuzungumza na wana TAJATI walipotembelea kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Makere

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Francis Namaumbo akizungumza na wanahabari wana TAJATI(pichani chini)waliotembelea ofisini kwake

Baadhi ya wanahabari wana TAJATI wakifuatilia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmshaudri ya wilaya ya Makete(picha juu) walipotembelea ofisini kwake miwshoni mwa wiki.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Makete Francis Namaumbo akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari wana TAJATI walipotembelea halmashauri ya Makete mwishoni mwa wiki.

Mmiliki wa Blogu hii Brandy Nelson akizungumza jambo kwenye kikao kilichowakutanisha wanahabari wana TAJATI na mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Kitulo

Wanahabari wakifuatilia jambo kutoka kwa mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Taaifa Kitulo

Wanahabari wana TAJATI wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Hifadhi ya Taifa Kitulo


Wanahabari wana TAJATI wakiwa mbele ya bango linalotambulisha Hifadhi ya Taifa ya Kitulo

Faraja Dembe Ofisa kutoka WCS akiwaonesha wanahabari maeneo na mipaka ya Hifadhi ya Kitulo


Wanahabari wakivinjari katika uwanda wa maua kwenye Hifadhi ya Taifa ya Kitulo walipotembelea mwishoni mwa wiki

Wanahabari Brandy Nelson na Esther Macha wakijiselfisha walipotembelea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wilayani Makete mkoani Njombe


Wanahabari wakiwa kwenye mpaka wa Mkoa wa Mbeya na Njombe walipokuwa wakirejea kutokea wilayani Makete mkoani Njombe