Pages

Sunday, February 28, 2016

WANATAJATI WALIPOTEMBELEA SURPRISE BEACH MAKAMBAKO

Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) wakiwa wamebarizi kwenye ufukwe wa Kigamboni uliopo mjini Makambako mkoani Njombe walipoenda kutembelea eneo hilo la kipekee la utalii nchini

Wanatajati wakiangalia mandhari ya Surprise Beach iliyopo Makambako

Wanahabari Christopher NYENYEMBE na Brandy Nelson wakiwa ndani ya Bahari wakivuka na boti kutokea Kigamboni Jijini Dar es Salaam mandhari hii iko Makambako mkoani Njombe katika Beach maarufu ijulikanayo kwa jina la Surprise




Mkurugenzi wa Star Intergrated ya Makambako mkoani Njombe inayomiliki Surprise Beach Mr Kyando akizungumza na na waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI) waliotembelea Ufukwe wa Surprise mwishoni mwa wiki (kulia)Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe
,
Waandishi wa habari za Utalii na uwekezaji Tanzania(TAJATI)wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Star Intergrated Mr Kyando, kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mahusiano wa TAJATI Felix Mwakyembe,Katibu Mkuu wa TAJATI Venance Matinya,Mweka hazina wa TAJATI Brandy Nelson,Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe na Mratibu wa TAJATI mkoa wa Njombe Mercy Sekabogo

Mfano wa Mlima Kilimanjaro uliopo kwenye kivutio cha Utalii cha Surprise Beach Makambo mkoani Njombe

Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji wakiendelea kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii ndani ya Surprise Beach iliyopo Makambako mkoani Njombe






WanaTAJATI wakiwa kwenye UFUKWE wa Suprise Makambako mkoani Njombe




Tuesday, February 16, 2016

NICE CATERING ILIVYOWAPONGEZA WAFANYAKAZI WAKE MJINI MOROGORO


Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Betty Mkwasa akimvisha mgolole wa heshima Mkurugenzi wa kampuni ya Nice Catering Yona Sonero  wakati wa sherehe ya kila mwaka ya kuwapongeza wafanyakazi wa kampuni hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nashera Hotel mjini Morogoro mwishoni mwa wiki

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Nice Catering ya Jijini Dar es salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya kituo cha kulelea watoto yatima cha Mehayo mjini Morogoro




Mkurugenzi wa Kampuni ya Nice Catering Yona Sonero akizungumza na mmoja wa watu wenye ulemavu Jabir Mwaipaya mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.



Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Nice Catering wakiwa kwenye kituo cha Mehayo ambako walitoa msaada mbalimbali ya vyakula,mafuta na sabuni vyenye thamani ya sh 750,000



Mkurugenzi wa kampuni ya Nice Catering Yona Sonero na MENEJA  wa kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Rungwe Express Bonny Mbamba yanayofanya safari kati ya Mbeya na Dar es salaam kila siku wakisikiliza ibada baada ya kutoa msaada wa vyakula kwenye kituo cha Mehayo mjini Morogoro


MC maarufu Charles Mwakipesile akifanya maombi katika kituo cha kulelea watoto cha Mehayo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Nice Catering Yona Sonero akifuatana na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Betty Mkwasa wakiwasili kwenye ukumbi wa Nashera Hotel mjini Morogoro wakati wa sherehe ya kuwapongeza wafanyakazi wa kampuni ya Nice Catering mwishoni mwa wiki.

Watoto  yatima na wenye ulemavu wa akili na viungo wa kituo cha Mehayo Mkoani Morogoro,mwishoni mwa wiki wamekabidhiwa  msaada wa vyakula mbali mbali na fedha tasilimu Sh750,000 kutoka kwa  Kampuni ya Nice Catering.
 Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Mkurugenzi wa Kampuni ya  Nice Catering,Yona Sonero alisema  sadaka kubwa inayomgusa mungu ni ya kusaidia watoto yatima kwa kuwawezesha kuishi maisha kama walivyo watoto wengine.
“Kuna wafanyabiashara wengi ambao wamejaliwa kuwa na kipato kikubwa ni vema wakatumia sehemu ya fedha zao kuwasaidia watoto hawa ili na wao waweze kuishi kama binadamu wengine.
Aidha Sonero alisema pamoja na msaada huo wa chakula anajitolea kununua baiskeli mbili za miguu mitatu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa miguu.
Alisema kampuni hiyo imekuwa ikifanya hivyo kila mwaka ambao ilitanguliwa na semina elekezi kwa watumishi wake zaidi 1000 na kwamba sadaka kuu ambayo anaitoa kwa mungu ni kuwasaidia watoto hao ,ambao wanamahitaji mengi na maisha yao ni magumu kutokana na uwezo mdogo walionao watu waliojitolea kuwalea.
Kwa upande wake mlezi wa kituo cha Mehayo kilichopo mjini Morogoro Linda Ngido alisema  kituo  hicho kina jumla ya watoto 65 wenye umri wa kuanzia miaka saba hadi 42 ambao ni yatima na ulemavu wa akili na viungo ,lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya afya kutokana na kituo hicho kushindwa kumudu gharama za matibabu mara wanapokwenda hospitalini.
“Tunaomba serikali ikitambue hiki kituo kuwa ni kazi ya kujitolea hivyo hawa watoto wapewe msamaha wa matibabu ili waweze kupata matibabu kama ilivyo kwa watu wenye uwezo na kuondokana na usumbufu ambao tunaupata katika vituo vya afya”alisema Ngido.
Alisema anashukuru kupata msaada huo kwani utawasaidia watoto hao kupata chakula cha uhakika kwani kwa mlo mmoja anatumia sh100,000 kutokana na idadi kubwa ya watoto alionao katika kituo hicho.
Aidha alisema changamoto nyingine ni  ukosefu wa maji kutokana kushindwa kulipia gharama za maji safi na taka za Moruwasa na kusababisha kutumia maji ya visima ambayo ladha yake ni ya chumvi.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo Mkuu wa wilaya ya Mvomero Betty Mkwassa aliwataka wamiliki wa makampuni mbalimbali nchini kuwa na nidhamu ya kulipa kodi serikalini.
Mkwassa alisema iwapo makampuni yatajitokeza kulipa kodi bila kusukumwa na mamlaka ya mapato nchini uwezekano wa makadirio ya ukusanyaji mapato serikalini utaongezeka mara dufu.
Alisema Kampuni ya Nice Catering ni mfano wa kuigwa kutokana na kufanya shughuli zake kwa uwazi.
''Kufanya vizuri kwa kampuni hii kunatokana na uwazi wake wa shughuli mbalimbali, hii ni dalili kwamba ni walipaji kodi wazuri,''alisema Mkwassa.
Hotel ya kisasa ya Rungwe Palace iliyopo jijini Dar es salaam


Nice Catering ni kampuni tanzu inayomiliki kampuni ya mabasi ya Rungwe Express na Rungwe Hotel ya Jijini Dar es salaam



Monday, February 8, 2016

SAFARI YA WANATAJATI KUMSAKA KIPUNJI MLIMA RUNGWE


Wanahabari wa Chama Cha waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji wakioneshana Nyani adimu aina ya Kipunji kwenye msitu wa hifadhi ya mlima Rungwe walipotembelea hivi karibuni

Mzee Mazao Fungo ambaye ndiye muongoza njia kuelekea kwenye msitu wa Mlima Rungwe akiwasisitiza wanahabari kukaa kimya ili kuweza kumuona Nyani Kipunji kwa kuwa Nyani huyo ana aibu huogopa kelele za watu




Nyani Kipunji akiwa juu ya mti

Safari ya kumsaka Nyani Kipunji iliendelea


Geti kuu la kuingilia kuanza kupandisha mlima Rungwe


Baadhi ya miti ya asili iliyopo kwenye Hifadhi ya Mlima Rungwe


Hii ni Camping Site  ambayo ilipewa heshima ya jina la Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye alifika hadi hapo na kuzungumza na wahifadhi wa mlima Rungwe

Ndani ya msitu huo kulikuwa na miti mikubwa na mikongwe



Maeneo mengi iliwalazimu wanahabari kutafutiza njia kwa kujipenyeza katikati ya miti ili kumsaka Nyani Kipunji


Mwisho wa safari kila mtu alichoka kiu na njaa ilikatwa kwa kunywa juice na mikate ya asili maarufu kama mabumunda ambayo kiuhakika yalikata njaa ya kurejesha nguvu kama awali


Kila mtu alichoka na kukalia mgongo ha;pa ni katika Hotyeli moja iliyopo katika kijiji cha Kyimo ambako wanatajati walipata fursa ya kupata vinywaji kupooza makoo yao kabla ya kuanza safari ya kurejea Jijini Mbeya



NI safari ya ndani ya msitu mnene uliosheheni miti mikubwa ya asili inayokadiriwa kuwa na umri wa maelfu ya miaka, yenye majani ya rangi ya kijani kibichi kitokanacho na uoto wa asili uliopo chini ya hifadhi ya Mazingira asilia ya Mlima  Rungwe, ukimya uliotawala ndani ya msitu huo, ubaridi na giza lililotokana na msitu huo kutanda  eneo lote la mlima huo uliogopesha na kutia hofu.
Wanyama ndege na wadudu wa kila aina walianza kuonekana kuanzia mwanzo wa safari kupitia geti kuu la Syukula hadi eneo la kilele cha mlima wa hifadhi ya mlima wa msitu wa Rungwe
wapekee ndio waliojivunia makazi hayo ambapo milio yao ilionesha aina ya furaha waliyonayo kuishi katika msitu wa aina hiyo ambao umeendelea kutunzwa na kuhifadhiwa vyema na serikali.
Hali hiyo iliwashawishi wanahabari wa chama cha waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania, (TAJATI)wamefanya ziara ya kiutalii kwenye Msitu wa Hifadhi Mazingira Asilia wa mlima Rungwe wenye ukubwa wa hekta 13,652.1  kwa nia ya kumsaka mnyama adimu duniani Nyani Kipunji.
Kwa mujibu wa mhifadhi mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Innocent Lupembe alisema kuwa Nyani Kipunji ni moja kati ya vivutio pekee vya utalii duniani ambaye hapatikani kokote zaidi ya msitu huo.
Alisema kuwa msitu huo umefanywa kuwa ni msitu wa hifadhi wa mazingira asili wa mlima Rungwe ambako ndani yake kuna baadhi ya wanyama kama vile Mbega,Ngedere. Tumbili na Nyani aina ya Kipunji ambaye ana asili ya aibu na kupatikana kwake
Alisema lengo la serikali  kuhifadhi msitu huo ni kulinda Bionuai na rasilimali zilizopo katika msitu huo ambao awali ulikuwa chini ya usimamiziwa Idara ya Misitu na Nyuki ambapo hata hivyo ulikuwa unaharibiwa na  kuvamiwa na  wananchi wanaolizunguka eneo hilo.
Lupembe alisema kuwa mbali ya kuhifadhi uoto wa asili uliogawanyika kwa sehemu 5 hadi 6 msitu huo una wanyama mbalimbali akiwemo Nyani aina ya Kipunji ambaye aligunduliwa na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya mazingira na viumbe hai(WCS) mwaka 2003.
Alibainisha kuwa hata hivyo ni asilimia 30 tu ya watalii kutoka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo huku asilimia 70 ni watalii kutoka ndani ya nchi wanaokadiriwa kufikia watalii 200 hadi 250 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mhifadhi Biolojia wa (WCS) Sophy Machage alisema kuwa msitu huo wa mlima Rungwe ambao uko juu km 2,981 kutoka usawa wa bahari ni moja kati ya hifadhi za asili ambayo rasilimali pekee ya Taifa inayohitaji kutunzwa mazingira yake.
Alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna msitu mnene na miti mikubwa ya asili ambaapo chini yake kuna chemichemi za maji yanayotiririka cjhini kwa chini kuelekea kwenye mito ya jirani inayopeleka maji Ziwa Nyasa.
Naye muongoza njia wa mlima huo Mzee Mazao Fungo alisema kuwa eneo la mlima huo halina njia halisi bali njia zilizopo ni za kubuni kutokana na mazingira ya msitu na mlima ulivyo.
Alimtaja Nyani Kipunji kuwa ni mnyama mwenye aibu ambaye kumuona kwake kunahitaji tahadhari na inawezekana kwa siku mbili au tatu asionekane ingawa kuna wakati hutembea kwa makundi.
‘’Akisikia kelele za watu hukimbia kila kundi linakuwa na kiongozi wao mwanaume na mlinzi wakisikia kelele au mchakacho wa miguu hukaa kimya hata kwa siku nzima hupendelea kuruka kwenye miti mirefu na huko ndiko makazi yao yalipo’’alisema Mzee Fungo.