Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Nice Catering ya Jijini Dar es salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya kituo cha kulelea watoto yatima cha Mehayo mjini Morogoro |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nice Catering Yona Sonero akizungumza na mmoja wa watu wenye ulemavu Jabir Mwaipaya mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. |
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Nice Catering wakiwa kwenye kituo cha Mehayo ambako walitoa msaada mbalimbali ya vyakula,mafuta na sabuni vyenye thamani ya sh 750,000 |
MC maarufu Charles Mwakipesile akifanya maombi katika kituo cha kulelea watoto cha Mehayo. |
Watoto yatima na wenye ulemavu wa akili na viungo wa kituo cha Mehayo Mkoani Morogoro,mwishoni mwa wiki wamekabidhiwa msaada wa vyakula mbali mbali na fedha tasilimu Sh750,000 kutoka kwa Kampuni ya Nice Catering.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhi msaada huo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Nice Catering,Yona Sonero alisema sadaka kubwa inayomgusa mungu ni ya
kusaidia watoto yatima kwa kuwawezesha kuishi maisha kama walivyo watoto
wengine.
“Kuna wafanyabiashara
wengi ambao wamejaliwa kuwa na kipato kikubwa ni vema wakatumia sehemu ya fedha
zao kuwasaidia watoto hawa ili na wao waweze kuishi kama binadamu wengine.
Aidha Sonero alisema
pamoja na msaada huo wa chakula anajitolea kununua baiskeli mbili za miguu
mitatu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa miguu.
Alisema kampuni hiyo
imekuwa ikifanya hivyo kila mwaka ambao ilitanguliwa na semina elekezi kwa
watumishi wake zaidi 1000 na kwamba sadaka kuu ambayo anaitoa kwa mungu ni
kuwasaidia watoto hao ,ambao wanamahitaji mengi na maisha yao ni magumu
kutokana na uwezo mdogo walionao watu waliojitolea kuwalea.
Kwa upande wake mlezi wa
kituo cha Mehayo kilichopo mjini Morogoro Linda Ngido alisema kituo hicho kina jumla ya watoto 65 wenye umri wa kuanzia miaka
saba hadi 42 ambao ni yatima na ulemavu wa akili na viungo ,lakini
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya afya kutokana na kituo hicho
kushindwa kumudu gharama za matibabu mara wanapokwenda hospitalini.
“Tunaomba serikali
ikitambue hiki kituo kuwa ni kazi ya kujitolea hivyo hawa watoto wapewe msamaha
wa matibabu ili waweze kupata matibabu kama ilivyo kwa watu wenye uwezo na
kuondokana na usumbufu ambao tunaupata katika vituo vya afya”alisema Ngido.
Alisema anashukuru
kupata msaada huo kwani utawasaidia watoto hao kupata chakula cha uhakika kwani
kwa mlo mmoja anatumia sh100,000 kutokana na idadi kubwa ya watoto alionao
katika kituo hicho.
Aidha alisema changamoto
nyingine ni ukosefu wa maji
kutokana kushindwa kulipia gharama za maji safi na taka za Moruwasa na
kusababisha kutumia maji ya visima ambayo ladha yake ni ya chumvi.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo Mkuu wa wilaya ya Mvomero Betty Mkwassa aliwataka wamiliki wa makampuni mbalimbali nchini kuwa na nidhamu ya kulipa kodi serikalini.
Mkwassa alisema iwapo makampuni yatajitokeza kulipa kodi bila kusukumwa na mamlaka ya mapato nchini uwezekano wa makadirio ya ukusanyaji mapato serikalini utaongezeka mara dufu.
Alisema Kampuni ya Nice Catering ni mfano wa kuigwa kutokana na kufanya shughuli zake kwa uwazi.
''Kufanya vizuri kwa kampuni hii kunatokana na uwazi wake wa shughuli mbalimbali, hii ni dalili kwamba ni walipaji kodi wazuri,''alisema Mkwassa.
Nice Catering ni kampuni tanzu inayomiliki kampuni ya mabasi ya Rungwe Express na Rungwe Hotel ya Jijini Dar es salaam

Hotel ya kisasa ya Rungwe Palace iliyopo jijini Dar es salaam |
Nice Catering ni kampuni tanzu inayomiliki kampuni ya mabasi ya Rungwe Express na Rungwe Hotel ya Jijini Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment