Pages

Monday, February 8, 2016

SAFARI YA WANATAJATI KUMSAKA KIPUNJI MLIMA RUNGWE


Wanahabari wa Chama Cha waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji wakioneshana Nyani adimu aina ya Kipunji kwenye msitu wa hifadhi ya mlima Rungwe walipotembelea hivi karibuni

Mzee Mazao Fungo ambaye ndiye muongoza njia kuelekea kwenye msitu wa Mlima Rungwe akiwasisitiza wanahabari kukaa kimya ili kuweza kumuona Nyani Kipunji kwa kuwa Nyani huyo ana aibu huogopa kelele za watu




Nyani Kipunji akiwa juu ya mti

Safari ya kumsaka Nyani Kipunji iliendelea


Geti kuu la kuingilia kuanza kupandisha mlima Rungwe


Baadhi ya miti ya asili iliyopo kwenye Hifadhi ya Mlima Rungwe


Hii ni Camping Site  ambayo ilipewa heshima ya jina la Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye alifika hadi hapo na kuzungumza na wahifadhi wa mlima Rungwe

Ndani ya msitu huo kulikuwa na miti mikubwa na mikongwe



Maeneo mengi iliwalazimu wanahabari kutafutiza njia kwa kujipenyeza katikati ya miti ili kumsaka Nyani Kipunji


Mwisho wa safari kila mtu alichoka kiu na njaa ilikatwa kwa kunywa juice na mikate ya asili maarufu kama mabumunda ambayo kiuhakika yalikata njaa ya kurejesha nguvu kama awali


Kila mtu alichoka na kukalia mgongo ha;pa ni katika Hotyeli moja iliyopo katika kijiji cha Kyimo ambako wanatajati walipata fursa ya kupata vinywaji kupooza makoo yao kabla ya kuanza safari ya kurejea Jijini Mbeya



NI safari ya ndani ya msitu mnene uliosheheni miti mikubwa ya asili inayokadiriwa kuwa na umri wa maelfu ya miaka, yenye majani ya rangi ya kijani kibichi kitokanacho na uoto wa asili uliopo chini ya hifadhi ya Mazingira asilia ya Mlima  Rungwe, ukimya uliotawala ndani ya msitu huo, ubaridi na giza lililotokana na msitu huo kutanda  eneo lote la mlima huo uliogopesha na kutia hofu.
Wanyama ndege na wadudu wa kila aina walianza kuonekana kuanzia mwanzo wa safari kupitia geti kuu la Syukula hadi eneo la kilele cha mlima wa hifadhi ya mlima wa msitu wa Rungwe
wapekee ndio waliojivunia makazi hayo ambapo milio yao ilionesha aina ya furaha waliyonayo kuishi katika msitu wa aina hiyo ambao umeendelea kutunzwa na kuhifadhiwa vyema na serikali.
Hali hiyo iliwashawishi wanahabari wa chama cha waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania, (TAJATI)wamefanya ziara ya kiutalii kwenye Msitu wa Hifadhi Mazingira Asilia wa mlima Rungwe wenye ukubwa wa hekta 13,652.1  kwa nia ya kumsaka mnyama adimu duniani Nyani Kipunji.
Kwa mujibu wa mhifadhi mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Innocent Lupembe alisema kuwa Nyani Kipunji ni moja kati ya vivutio pekee vya utalii duniani ambaye hapatikani kokote zaidi ya msitu huo.
Alisema kuwa msitu huo umefanywa kuwa ni msitu wa hifadhi wa mazingira asili wa mlima Rungwe ambako ndani yake kuna baadhi ya wanyama kama vile Mbega,Ngedere. Tumbili na Nyani aina ya Kipunji ambaye ana asili ya aibu na kupatikana kwake
Alisema lengo la serikali  kuhifadhi msitu huo ni kulinda Bionuai na rasilimali zilizopo katika msitu huo ambao awali ulikuwa chini ya usimamiziwa Idara ya Misitu na Nyuki ambapo hata hivyo ulikuwa unaharibiwa na  kuvamiwa na  wananchi wanaolizunguka eneo hilo.
Lupembe alisema kuwa mbali ya kuhifadhi uoto wa asili uliogawanyika kwa sehemu 5 hadi 6 msitu huo una wanyama mbalimbali akiwemo Nyani aina ya Kipunji ambaye aligunduliwa na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya mazingira na viumbe hai(WCS) mwaka 2003.
Alibainisha kuwa hata hivyo ni asilimia 30 tu ya watalii kutoka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo huku asilimia 70 ni watalii kutoka ndani ya nchi wanaokadiriwa kufikia watalii 200 hadi 250 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mhifadhi Biolojia wa (WCS) Sophy Machage alisema kuwa msitu huo wa mlima Rungwe ambao uko juu km 2,981 kutoka usawa wa bahari ni moja kati ya hifadhi za asili ambayo rasilimali pekee ya Taifa inayohitaji kutunzwa mazingira yake.
Alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna msitu mnene na miti mikubwa ya asili ambaapo chini yake kuna chemichemi za maji yanayotiririka cjhini kwa chini kuelekea kwenye mito ya jirani inayopeleka maji Ziwa Nyasa.
Naye muongoza njia wa mlima huo Mzee Mazao Fungo alisema kuwa eneo la mlima huo halina njia halisi bali njia zilizopo ni za kubuni kutokana na mazingira ya msitu na mlima ulivyo.
Alimtaja Nyani Kipunji kuwa ni mnyama mwenye aibu ambaye kumuona kwake kunahitaji tahadhari na inawezekana kwa siku mbili au tatu asionekane ingawa kuna wakati hutembea kwa makundi.
‘’Akisikia kelele za watu hukimbia kila kundi linakuwa na kiongozi wao mwanaume na mlinzi wakisikia kelele au mchakacho wa miguu hukaa kimya hata kwa siku nzima hupendelea kuruka kwenye miti mirefu na huko ndiko makazi yao yalipo’’alisema Mzee Fungo.




0 comments: