TAASISI ya
FaidaMali kwa ufadhili wa Shirika la
Mapinduzi ya Kijani (AGRA), imetoa msaada wa baiskeli kwa vikundi 60 vya wakulima zenye thamani ya Sh11.4 kwa ajili ya
kurahisisha mawasiliano katika shughuli za kilimo kwa Wilaya tatu za Morogoro
na Mbeya.
Akizungumza na vikundi vya wakulima Igurusi Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa Mkurugenzi wa FaidaMali Tom Sillayo alisema taasisi hiyo pia imetoa msaada wa komputa tano
kwa vikundi vya akiba na mikopo(SACCOS)zenye thamani ya Sh5.6milioni katika
Wilaya hizo tatu.
Alisema kuwa taasisi hiyo ya Faida Mali alizitaja wilaya
zilizokabidhiwa msaada huo wa baiskeli
na komputa kuwa ni pamoja na Kilosa Mkoani Morogoro na Mbarali na Mbeya vijijini ambapo imekuwa
ikijishughulisha na kazi ya kutoa mafunzo kwa wakulima kwa kupitia vikundi
kuhusinana na kilimo bora na cha kisasa.
“Wakulima wamekuwa wakipatiwa mafunzo juu ya mbinu mbali
mbali za kilimo bora,namna ya kutumia vizuri mbolea na mbegu bora za kisasa
ikiwa ni pamoja na kujifunza namna ya
kuongeza uzalishaji wa mazao ili kuweza
kupata mavuno mengi “alisema
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzake Abia Mwasuta
kutoka kijiji cha Chamoto Wilaya ya Mbarali alisema wanakabiliwa na changamoto
mbali mbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mtaji,elimu ya ujasiliamali,vitendea
kazi na ubovu wa miundombinu ya barabara.
Alisema pamoja na kupewa mafunzo na msaada wa baiskeli,
wakulima wengi hawana mtaji kwa ajili
ya kumudu gharama za pembejeo ili
kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga na kuweza kupata mavuno mengi yatakayo
wasaidia kuboresha maisha yao.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka AGRA ,Valentino Miheso
alisema mradi huo ni wa miaka mitatu
ambapo wakulima watapata mafunzo ya utalaam wa kilimo cha biashara,vitendea
kazi na jinsi ya kuanzisha miradi midogomidogo ya ufugaji kupitia vikundi ili
kuondokana na umasikini.
Alisema kuhusu komputa zinatolewa kwenye Saccos zilizopo
maeneo ya vijijini ambazo vikundi vya wakulima ni wanachama na wananufaika
katika kupata mikopo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kupata fedha
kwa ajili ya pembejeo za kilimo.
Na Brandy Nelson,Mbeya
0 comments:
Post a Comment