MKUU wa mkoa
wa Mbeya Amos Makalla ameunda kikosi kazi cha watu 14 kilichogawanyika katika
makundi mawili ambacho kitapitia upya uhakiki wa majina ya watumishi hewa na
kurejea kufanya uhakiki kati ya April 20 hadi 24.
Makalla
aliagiza uhakiki huo kufanyika kati ya tarehe 25 hadi 29 ambapo awali alipata
taarifa ongezeko la watumishi hewa 3 katika halmashauri ya Jiji la Mbeya na
watumishi 7 kutoka halmashauri ya Mbeya.
Alisema
katika uhakiki wa awali Mkoa wa Mbeya na
Songwe uligungulika kuwa na watumishi hewa 94 waliosababisha hasara ya sh milioni
457 na kuwa hadi sasa kuna jumla ya watumishi hewa 10 kati ya watumishi hewa
saba ambapo Halmashauri ya Mbeya ina jumla ya watumishi 23 kutoka watumishi
hewa 16 waliotajwa awali.
Makalla
amewataka wafanyakazi wote kufika mbele ya kamati wakiwa na barua ya mwajiri,
vitambulisho na Payroll ya mwezi Machi 2016 na kuiagiza kamati mara baada ya
kufanya uhakiki watakaobainika na kesi za kujibu waburuzwe mahakamani na
kutakiwa kurejesha fedha zote za serikali.
0 comments:
Post a Comment