Pages

Tuesday, April 5, 2016

NAPE Atembelea cha Waandishi za Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania

WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NAPE NNAUYE AKIWA NA BAADHI YA WANAHABARI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA UTALII NA UWEKEZAJI TANZANIA TAJATI ALIPOTEMBELEA MAKAO MAKUU YA CHAMA HICHO JANA ASUBUHI

Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipotembelea Ofisi za TAJATI jana asubuhi

Waziri Nape akionesha eneo la jengo la Ofisi za TAJATI ambalo chama hicho kimewdeka mpango wa kuwa na chumba cha Habari chenye studio kubwa ya kisasa



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye akikabidhiwa kikombe chenye nembo ya Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) kwenye ofisi za chama hicho alipotembelea jana asubuhi

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za TAJATI jana asubuhi(kushoto) ni Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili(kulia) Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe
WAZIRI  wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye amewapongeza wanahabari wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) na kuwataka kukitangaza chama hicho nchi nzima ili kilete tija na manufaa kwa Taifa.

Waziri Nape alisema hayo jana alipozuru ofisi za TAJATI Jijini Mbeya na kusema kuwa fursa ya wanahabari kuandika habari za Utalii na Uwekezaji ni kubwa hivyo ni vyema chama hicho kikasambaa nchi nzima ili fursa hiyo iwafikie wananchi wengi.
‘’Kisambazeni chama chenu nchi nzima, serikali itatoa ushirikiano kwenu, andikeni habari za Utalii na Uwekezaji ili vivutio vya Utalii vitambulike na fursa za uwekezaji zijulikane,’’alisema Waziri Nape.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili alisema kuwa kuanzishwa kwa chama hicho kumelenga kuibua fursa za utalii na uwekezaji zilizopo nchini na kuzitangaza ili vitambulike ndani na nje ya nchi.

Awali Waziri Nape alitembezwa kwenye ofisi za TAJATI na kuelekezwa mikakati ya chama hicho kulifanya jengo hilo kuwa lenye chumba cha Habari na studio ya kisasa itakayowawezesha wanahabari kupata taarifa mbalimbali za Utalii na uwekezaji.


‘’Tumelenga kuwa na chumba cha Habari na Studio ya kisasa itakayowawezesha wanahabari kupata fursa za habari za Utalii na Uwekezaji nchini,’’alisema Christopher Nyenyembe Makamu Mwenyekiti wa TAJATI. 

0 comments: