Pages

Monday, June 20, 2016

MAKALLA AWAPA SOMO LA KILIMO NA UFUGAJI WATAFITI WA UYOLE








 



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa somo kwa taasisi za utafiti wa kilimo, mifugo wa chuo cha kilimo Uyole akiwataka kuwekeza zaidi kwenye  utafiti ili kutoa wataalaam bora wa kilimo na ufugaji.
Makalla amesema ili kujitosheleza kwa chakula na mazao ya mifugo nchini wataalamu bora wa utafiti wanahitajika ikiwa ni pamoja na kuwa na malighafi ya Viwanda.
Amesema Rais Dkt John Pombe Magufuli anataka nchi iwe na viwanda vidogo, viwanda vya Kati na vikubwa na kwamba viwanda hivyo vitategemea zaidi malighafi za ndani ambazo zitatokana na kilimo cha kitaalamu sanjari na upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo.
Amefafanua kuwa nchi yoyote inayowekeza kwenye utafiti huondokana na matatizo ya kukosekana kwa mbegu bora za mazao ya kilimo na mifugo na hivyo jambo pekee la taasisi za Uyole kutumia teknolojia ya kisasa kwa usindikaji wa mazao ili kuyaongezea thamani.

Kadhalika Makalla amewataka maofisa kilimo,vikundi vya wakulima na wafugaji kutembelea chuo cha Utafiti Uyole ili kujifunza mambo mbalimbali ya kilimo na ufugaji ili kuzalisha kwa tija.

Saturday, June 18, 2016

MAKALLA ASHIRIKI UJENZI WA KITEPUTEPU RUNGWE



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipita kwenye eneo la kivuko cha Kibundungulu kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambacho kinajengwa

Mkazi wa kijiji cha Kibundungulu akipita ndani ya mto Mbaka kutokana na kivuko cha eneo hilo kuvunjika baada ya kutokea mafuriko wakati wa masika

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akishiriki kukoroga zege kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha Kibundungulu wilayani Rungwe

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akizungumza na wakazi wa eneo la mto Mbaka ambako kinajengwa kivuko

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kivuko katika mto Mbaka wilayani Rungwe

Kilio cha wakazi wa kitongoji cha Kibundungulu kilichopo katika kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe waliokuwa wakipata tabu kuvuka kwenye kiteputepu sasa kumalizwa mwezi ujao.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ambaye amewatembelea wananchi wa kitongoji hicho na kushiriki ujenzi wa kivuko hicho jana amesema kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kimemuwezesha Mkandarasi kukamilisha kivuko hicho kwa muda wa wiki mbili.
Amesema kwa mujibu wa mkandarasi kivuko hicho kitakamilika Julai 8 na wananchi wa kijiji hicho wataanza kupata huduma muhimu za kijamii kwa kutumia kivuko hicho.
Awali wananchi wa maeneo hayo walikuwa wakipita ndani ya mto kutokana na kivuko hicho kusombwa na maji wakati wa masika na kwamba kivuko hicho kitakuwa ni cha muda huku kukiwa na mkakati wa kujenga daraja la kudumu.
Aidha Makalla amewasihi wananchi kuacha kuvuka kwa kutumia waya na kuwa kukamilika kwa kivuko hicho kitasaidia wananchi kuondokana na tatizo la kuvuka kwenye mto wenye maji mengi jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.

Sunday, June 5, 2016

MWAMPONDELE ASHINDA KATIBU UCHUMI NA FEDHA CCM MKOA WA MBEYA

James Mwampondele (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Uchumi na Fedha wa CCM mkoa wa Mbeya.



Mwandishi wa habari na mwkilishi wa gazeti la Chama (UHURU) mkoa wa Mbeya Solomon Mwansele akimpongeza kwa kwa kuchaguliwa kuwa  Katibu Uchumi na Fedha mkoa wa Mbeya James Mwampondele






MJASIRIAMALI na mwekezaji Jijini Mbeya James Mwampondele(50) ameshinda nafasi ya Katibu Uchumi na Fedha ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoani Mbeya kwa kupata jumla ya kura 36 kati ya kura 65 za wajumbe wote wa uchaguzi huo.
Mwampondele aliwabwaga wapinzani wake aliochuana nao  vikali katika uchaguzi huo ambao ni  Steven Mwakajumilo aliyepata kura 25  na Mshereheshaji mashuhuri Jijini Mbeya Charles Mwakipesile aliyepata kura 4.
Wagombea Mwakajumilo na Mwakipesile waliwahi kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu kuwania nafasi ya Ubunge na kushindwa kwenye mchujo wa ndani wa CCM ambapo Mwakipesile aliwania Jimbo la Mbeya mjini na Mwakajumilo aliwania jimbo la Busokelo.
Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya aliyekuwa  Katibu Uchumi na Fedha wa mkoa wa Mbeya Hans Mwakisyala kufariki dunia kabla ya kumaliza muda wake uliotarajiwa kumalizika Julai mwaka huu.
Mwakisyala alipokea kijiti kutoka kwa Kenneth Ndingo aliyedumu katika nafasi hiyo kwa jumla ya miaka 15 hadi mwaka 2014 alipoamua  kupumzika.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo Mwampondele aliwashukuru wanachama wa CCM kwa kumuunga mkono na kuahidi kuendeleza mazuri ya mtangulizi wake  ambapo pia aliomba ushirikiano wa hali na mali kwa viongozi wa chama.
‘’Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu, pili nawashukuru wana CCM wote pamoja na viongozi wangu bila kuwasahau wagombea wenzangu, naahidi kushirikiana nanyi kwa hali na mali katika kusimamia sera na ilani za chama chetu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi,’’alisema Mwampondele.

Thursday, June 2, 2016

MADIWANI MAKETE, WANGING'OMBE KUPATA MAFUNZO YA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA


Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Njombe Richard Moshi(kulia) akimshukuru Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima mara baada kufunga mafunzo ya uzinduzi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma kwa Halmashauri za Mkoa wa Njombe.

Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt.Peter Kilima akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za umma

Mwezeshaji kutoka mradi wa Mifumo ya Uimarishaji Sekta za Umma Bunto Mbozi akiwasilisha mada kwenye kikao kilichowahusisha Wakurugenzi, wakuu wa idara, wenyeviti na viongozi wa halmashauri 6 za mkoa wa Njombe

Kiongozi wa uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma Dkt. Peter Kilima akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe Richard Moshi taarifa ya uteuzi wa Halmashauri mbili za Makete na Wanging'ombe kwa ajili ya kushiriki mafunzo ya awamu ya kwanza kwa Madiwani wa Halmashauri hizo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Richard Moshi akitanganza Halmashauri mbili za mwanzo zilizochaguliwa kushiriki mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma kwa madiwani.

Mkurugenzi Msaidizi, Uismamizi Rasilimali watu Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mmbaga akitoa nasaha mara baada ya kufungwa kwa uzinduzi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma mjini Njombe.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma wakiwa kwenye kazi za vikundi

Kiongozi wa Timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari 

Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Miriam Mmbaga akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo kwa watendaji an watumishi wa idara halmashauri za wilaya mkoa wa Njombe.

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Assumpter Mshama akizungumza kwenye kikao kilichozishirikisha Halmashauri 6 za Mkoa wa Njombe

Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima akihakiki taarifa zake kabla ya kutangazwa kwa Halmashauri mbili za Makete na Wanging'ombe kushiriki mafunzo kwa madiwani juu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma.


HALMASHAURI 2 za Makete na Wanging’ombe mkoani Njombe zimechaguliwa kuingia katika awamu ya kwanza ya  mafunzo ya Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).
Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Shirika la Msaada la Kimataifa la Marekani USAID yatawahusisha Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi pamoja na wakuu wa Wilaya.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa Halmashauri hizo Kiongozi wa timu ya Uzinduzi Dkt Peter Kilima alisema Halmashauri hizo zimechaguliwa kuwa za mwanzo kushiriki mafunzo hayo kutokana na changamoto walizonazo.
‘’Vigezo vya uhitaji vimewapa nafasi ya kwanza kushiriki mafunzo haya kwa Madiwani ingawa halmashauri zote za Mkoa wa Njombe zitapata mafunzo hayo kwa awamu ya pili’’
Alisema mafunzo hayo yanatarajia kuanza Jumatatu ijayo mjini Njombe na kutolewa na wataalamu wa mafunzo kutokea mjini Dodoma.
Akizungumzia kuteuliwa kwa Halmashauri ya Makete,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Egnato Mtawa alisema anaamini changamoto zilizopo zimetoa kipaumbele kwao kuwa wa mwanzo kupata mafunzo hayo.
‘’Changamoto za Wilaya yetu zimetupa kipaumbele kuteuliwa wa mwanzo kupata mafunzo kwa Madiwani,tuna changamoto za jiografia na Miundo mbinu, tunaamini hatimaye changamoto tulizonazo zitapatiwa ufumbuzi’’ alisema Mtawa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Assumpter Mshama alisema mafunzo hayo kwa Madiwani yataongeza weledi wa utendaji kazi kwa watumishi  kutokana na Halmashauri hiyo kuwa mpya.
Awali akizungumza mara baada ya kufungwa kwa uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi, Usimamizi wa Rasilimali watu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Miriam Mmbaga alisema kukosekana kwa maadili kwa watumishi wa umma ndiko kunakosababisha Halmashauri nyingi zipate hati zenye mashaka.
Alifafanua kuwa maadili yanayoelezwa ni yale yale yaliyopo katika imani za dini kwa kuwa vitabu vya dini zote zinapinga vitendo viovu ikiwemo rushwa.
‘’Dini zote zinapinga rushwa, maadili ya utumishi wa umma ni yale yale yaliyopo kwenye vitabu vya Uislamu na Ukristo,’’ alisisitiza.

Wednesday, June 1, 2016

USAID YAZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA KWA MIKOA 13

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Njombe Anatory Choya(wa nne kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Njombe na watendaji viongozi wa mradi wa Uimarishaji Mifumo hya Sekta za Umma jana.

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Njombe Anatory Choya akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Edwin Mwanzinga kabla ya uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma mjini Njombe jana.

Watendaji na viongozi wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma wakati wa uzinduzi wa mradi huo mjini Njombe jana.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njonbe Anatory Choya(kulia) akiteta jambo na Kiongozi wa Uzinduzi wa mradi wa Mifumo ya Uimarishaji Sekta za Umma kwenye ukumbi wa Kyando mjini Njombe jana.

Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa rasimali watu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mariam Mmbaga akitoa ufafanuzi juu ya utendaji bora wa watendaji wa Halmashauri unavyoweza kusaidia kuboresha huduma kwa umma.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anatory Choya akitamka neno la Uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma mjini Njombe jana.

Kiongozi wa Uazinduzi wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma Dkt. Peter Kilima akielezea azma ya mradi huo kwa Halmashauri 93 na mikoa 13 nchini.


SHIRIKA la msaada la Marekani USAID limekuja na muarobaini utakaoweza kuzisaidia Halmashauri za miji, Manispaa na Majiji kuepukana na hati chafu kwa kuanzisha mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya Sekta za Umma PS3.
Mradi huo wa wenye gharama ya Dola milioni 62 utaanza  kutekelezwa kwenye halmashauri 93  za miko 13 ya Njombe,Iringa,Morogoro,Mbeya,Lindi,Mtwara, Rukwa, Dodoma,Kigoma,Kagera, Mwanza,Shinyanga na Mara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo mkoani Njombe Kiongozi wa timu ya Uzinduzi wa mradi huo Dkt. Peter Kilima alisema kuwa mradi huo utazisaidia Halmashauri kujenga dhana shirikishi katika uimarisha mifumo ya sekta za utendaji kwa umma.
Alisema mradi huo wa miaka mitano umeanza Julai 2015 ambao utaendelea hadi Julai 2020 ambapo matarajio kila halmashauri katika halmashauri 93 zitafikiwa na mradi huo.
Dkt. Kilima alisema mifumo ya utekelezaji ipo katika sehemu 5 za Rasilimali watu,Rasilimali fedha,Mfumo wa TEHAMA na Tafiti Tendaji ambapo kwa sasa imeshazinduliwa katika mikoa 7 ya Iringa,Shinyanga,Dodoma,Mwanza,Mbeya, Mtwara na Rukwa.
Alisema mradi huo umbao umeandaliwa kwa kushirikiana na serikali ya Marekani na Tanzania unatekelezwa na mashirika saba yakiwemo ya Kitaifa na Kimataifa ambayo ni Abt Associates Inc ambaye ndiye mtekelezaji mkuu pamoja na watekelezaji wasaidizi.
‘’Mradi huo utaimarisha mfumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri, utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa’’alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali watu,Ofisi ya Rais TAMISEMI, Miriam Mmbaga alisema mradi huu utatoa msaada wa kitaaluma katika ,kuimarisha mifumo iliyopo kwenye utawala wenye lengo la ushirikishwaji katika kuboresha utoaji huduma kwa jamii.