Pages

Monday, November 25, 2013

HABARI KATIKA PICHA

Askari polisi kutoka Dawati la  jinsia Wanawake na Watoto kutoka  jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya   wameadhimidha siku 16 za kupambana na ukatili wa kijinsia  kwa kutoa msaada wa unga,sukari na sabu  kwenye mahabusu ya watoto Wadogo iliyopo Mwanjelwa jijini mbeya .kulia aliyevaa sweta la kijivu ni Ofisa mfawidhi wa kituo hicho  Bibi Doroth Samky akitoa mkono wa shukrani kwa askari polisi  kutoka katika dawati hilo Biam Msele. 

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya  Bibi Magreth Malenga akiwa katika moja ya shamba darasa la zao Mpunga uliopandwa kwa mbegu za kisasa na kutumia mbolea mradi unaotekelezwa na kituo cha utafiti wa kilimo Uyole  katika kijiji cha Makwale Wilayani  Kyela

Mkazi na mkulima wa kijiji mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoani  Mbeya Joseph Mwazembe akipandikiza miche ya kahawa katika shamba lake baada ya kuathiliwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

0 comments: