Kitengo cha Dawati
la jinsia wanawake na watoto cha jeshi
la polisi Mkoa wa Mbeya kimebaini vitendo vya waganga wa kienyeji kuhusika katika kuwashawishi watoto wadogo
kufanya vitedo vya kikatili kwa madai ya
kuwapatia utajiri.
Akizungumza wakati wa
kuadhimisha siku ya 16 za kupambana na ukatili wa kijinsia
Mwenyekiti wa dawati hilo dani ya jeshi
la polisi Mary Gumbo alisema kuwa katika
kuadhimisha siku hizo wamebaini mambo mbali mbali i yanayosababisha watoto
wadogo kujiiingiza katika kufaya ukatili kijinsia.
“Katika siku hii tumefanikiwa kuwatembelea watoto waliopo
katika mahabusu ya Mwanjelwa ikiwa ni
pamoja na kutoa msaada wa unga,sukari na sabuni ambapo tumebaini kuwepo kwa watoto ambao wamefanya matukio mbali
mbali ya kikatili yakiwemo ya ulawiti
huku wengine wakishawishiwa na waganga
wa kienyeji kufanya matukio hayo kwa
madai ya kupatiwa utajiri ”alisema
Alisema kuwa kitendo hicho
kinafanywa na baadhi ya Waganga wa kienyeji kwa malengo ya kujipatia fedha
kwani ni udanganyifu mkubwa na unalenga kuwaharibia watoto wadogo maisha na
hatimaye kuishia mikononi mwa sheria na kufungwa.
“Jamii inapaswa kutambua kuwa watoto wana haki ya kupata elimu na mahitaji
mengine ya kila siku na wanahitaji
msaada mkubwa wa malezi bora kutoka
kwa jamii inayowazunguka na kumuona
mtoto wa mwenzio ni wako hivyo tunahitaji kuwalea vizuri na siyo kuwashawishi
kujiingiza katika kufanya vitendo vya ukatili”alisema
Kwa upande wake Afisa
mfawidhi wa mahabusu ya watoto wadogo
Mwanjelwa mkoani Mbeya Doroth Samky kituo hicho kimekuwa
kikipokea watoto kutoka katika maeneo mbali mbali na kwamba wengi wao wamekuwa
wakikutwa na makosa huku wakiwa hawana wazazi.
Alisema kuwa katika
kuwanusuru watoto kujiingiza katika matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kujihusisha na ukatili,
jamii inapaswa kuelimishwa juu ya masuala ya haki za watoto,unyanyasaji wa kijinsia, ukatili wa watoto na
jinsi ya kuwasaidia watoto kuepukana na kujihusisha na matendo hayo.
0 comments:
Post a Comment