MAMLAKA ya
Mawasiliano Tanzania kanda ya nyanda za juu kusini imeazimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake kwa kukutana na wadau mbali mbali wa mawasiliano Mkoani Mbeya kwa lengo la kubadlishana mawazo na
kuelezea changamoto na mafanikio katika
sekta ya mawasiliano.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo meneja wa TCRA kanda ya nyanda za juu kusini Deogratius
Moyo alisema kuwa watumiaji
wa simu za mikononi wameongezeka kutoka milioni 3.1 hadi kufikia takribani milioni 28.
Moyo alisema
kuwa idadi hiyo inafanya Tanzania kuwa
na Wakazi 59 wenye simu kwa kila wakazi 100 na kwamba utafiti uliofanywa na mamlaka ya mawasiliano
kuna watumiaji wa wavuti wapatao milioni 7.5
ambapo idadi hiyo inaendelea kuongezeka.
Aidha Moyo
amewataka wamiliki na mameneja wa radio na Televisheni
kuhakikisha watangazaji wao wote wanazijua kanuni na sheria za
mawasiliano na utangazaji ili kuepusha upotoshaji kwa jamii.
Alisema kuwa
mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na udhaifu
hafifu wa maudhui kwenye televisheni,ukosefu wa miundombinu kutokana na miji
mingi kujengwa holela na matumizi mabaya ya mitandai ikiwa ni pamoja na simu za
mkononi.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela ameyataka makampuni ya simu
kushirikiana katika uwekaji wa minara ili kuondokana na utitili wa minara na kupunguza gharama za matumizi ya simu kwa Wananchi.
Meela
alisema kuwa utaratibu wa hivi sasa
unaofanywa na hayo makampuni unasababisha
uwepo wa utitiri wa minara,ongezeko la gharama kubwa kwa watumiaji na kuwepo
kwa gharama kubwa katika kuweka minara hiyo.
Alisema kuwa
utitiri wa minara hiyo unachangia kuwepo kwa matumizi ya fedha nyingi ambazo
zingeweza kutumika katika kuwasaidia wananchi kwenye shughuli mbali mbali za
maendeleo.
Brandy
Nelson
0 comments:
Post a Comment