Katibu Mkuu wa Chama
cha Mapinduzi (CCM)Abdulhamani
Kinana ametubu mbele ya Umma kuwa
chama hicho hakina sababu ya kukwepa lawama kwa kuwa muda mrefu kimechangia
Wananchi kupata mateso na kudhulumiwa kutokana na kushindwa kuwasimamia
watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakifanya
mambo ovyo ovyo na kusababisha chama na serikali yake kuendelea
kuchukiwa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi
ya Luanda Nzovwe jijini Mbeya huku mamia
ya watu waliodhuhuria mkutano huo wakimshangilia alisema kuwa kuna mambo mengi
ambayo CCM imefanya vibaya ikiwa ni pamoja na kuyambia macho vitendo vya ovyo
ovyo vinav yowaumiza Wananchi.
“Katika hili Wananchi naomba msiwalaumu hawa viongozi wa CCM
walioko huku kwenu mtulaumu sisi tuliopo mbinguni ambao kwa mara nyingine
tumeshiriki katika kuwadhurumu na
kuwanyanyasa nyie kwa ajili ya masilahi ya watu binafsi”alisema
Alisema kuwa kuna mashamba
na Viwanda ambavyo vimebinafsishwa na kuuzwa kwa bei ndogo
na wawekezaji wa viwanda hivyo wamekuwa wakiwanyanyasa Wananchi huku
wale wa kwenye mashamba
wakishindwa kuendeleza mashamba
hayo na kuamua kuwakodishia
Wananchi kwa gharama kubwa lakini chama hicho kimekikaa kimya bila kuchukua hatua yoyote.
“Mimi ninashangaa tunajisifia kuwa tumefanikiwa kujenga
barabara lakini hakuna tunachokifanya
kwa hawa wananchi wewe ikiwa ni pamoja na kutoa ahadi za ajira kwa vijana huku ni kuwaongopea hawa vijana wetu kwani tutawapeleka wapi kama
viwanda vingi vilivyobinafsishwa vimekufa na havifanyi kazi”alisema
Kinana ambaye
asilimia kubwa ya hotuba yake katika mkutano huo alitumia kuichambua CCM na kueleza ukweli na uwazi alisema kuwa
hakuna haja ya viongozi wa
CCM na Wanachama wake kuimba nyimbo za
Iena iena CCM Namba moja wakati
hakuna kinachofanyika katika kuwasaidia Wananchi kutatua matatizo yao.
“Harafu
mnalalamika kuwa wananchi hawaji kwenye mikutano waje kusikiliza nini
utumbo? Wananchi hawawezi kuja kuja kusikiliza ujinga mnaosema na
nyie kama viongozi mnatakiwa kuwajibika kwa wananchi na kufahamu
nini mnatakiwa kufanya kwa wananchi sio kukaa na kubweteka tu”alisema Kinana
Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Nape Nauye
amesema kuwa katibu Mkuu Abdulhaman
Kinana ni kiongozi wa mfano wa kuigwa
kutokana na utaratibu wake wa kuzunguka
nchi nzima na kusikiliza kero za Wananchi.
Alisema kuwa Katibu huyo tangu ameingia madarakani amekuwa
akikiongoza chama hicho kwa kukaa na Wananchi wa ngazi ya chini na kusikiliza
kero zao na kufuatilia utekelezaji wa Iran ya chama cha mapinduzi.
“Nakupongeza Katibu mkuu kwa kazi kubwa unayoifanya kwani
ume weza hata kukaa chini na mabarozi wa nyumba kumi na kuwasikiliza kero zao
na kubadilishana mawazo hiki
unachokifanya ni mfano na ndiyo CCM ya
hayati baba wa Taifa Mwl Julius
Kambarage Nyerere”alisema
Naye Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Godfrey
Zambi alisema kuwa hapo nyuma chama
kilitaka ku[poteza mwelekeo kwa wananchi kutokana na kutojitokeza mbele ya
Wananchi na kusikiliza kero zao.
Alisema kuwa kwa sasa chama hicho kimeamua kurudi na kuanza
kusikiliza kero za Wananchi na kuyasemea
mambo ambayo yanayowasumbua na
wamekuwa wakikosa mahala pa kuyapeleka na kupatiwa ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment