Katibu Mkuu wa Chama cha
mapinduzi Abdalhaman Kinana amepiga marufuku tabia ya kuwalazimisha
Wakulima kutumia mbolea ya Minjingu kutokana na kuwa Wananchi
wahaitaki Mbolea hiyo kwa madai kuwa haiwafai katika kilimo.
Kinana alitoa kauli hiyo jana katika
mkutano wa hadhara alioufanya katika kiwanja cha shule ya msingi ya
Ruanda Nzovwe jijini Mbeya alipokuwa akikamilisha ziara ya kutelembea Wilaya za
Mkoa wa Mbeya kwa lengo la kuangalia changamoto mbali mbali
zinazowakabili Wananchi.
Kinana alisema katika ziara yake
amebaini matatizo manne katika Mkoa wa Mbeya ikiwa ni pamoja na soko la
Mwanjelwa,Mbolea ya Minjingu , barabara na tatizo la kukatika mara kwa
mara kwa umeme na vifaa vinaharibika na kukatisha watu Starehe na
matatizo ya madai ya Walimu.
Alisema kuwa hakuna haja ya
kuendelea kuwalazimisha Wananchi kutumia Mbolea kwani wao ndiyo wanaojua
ni mbolea ipi ambayo inawafaa katika mazao yao ya minjingu hivyo
serikali inapaswa kuweka mbolea inayowafaa wananchi kwenye ruzuku.
“Inakuaje Wakulima ambao
ndiyo wahusika na wapo huku vijijini ndiyo wanajua mbolea inayo faa katika
mazao yao lakini mtu ambaye amekaa Dar es Salaam hafahamu masuala ya kilimo
anawalazimisha wakulima kutumia Mbolea ya minjingu kama wao wanaona inafaa
wabaki nayo wenyewe “alisema
Alisema kuwa hao watu
wanaowalazimisha wakulima kutumia Mbolea ya minjingu wanamadaraka gani
Serikali hadi kufikia maamuzi ambayo hayaendani na matwaka ya
Wananchi”kwani shamba,udongo,mbegu ni ni vya mkulima sasa iweje mtu
mwingine aje kumlazimisha kutumia mbolea ambayo haina manufaa kwa mkulima
huyo”alisema
Aidha katika mkutano huo Kinana
alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kutoa majibu ya
serikali kwa Wananchi kutokana na kukikataa Mbolea ya Minjingu ambapo mkuu huyo
alisema kuwa tayari serikali imetambua mmalalamiko hayo na kuyafanyia
kazi.
Kandoro alisema kuwa kwa sasa
serikali itaingiza Mbolea ya Dap kwenye Ruzuku ili mkulima aweze kuitumia
badala ile ya minjingu na kwamba serikali kushirikiana na wataalam na
viwanda vinavyzalisha mbolea ya minjingu itafanya utafiti wa
kina ili kubaini matatizo ya Mbolea hiyo.
0 comments:
Post a Comment