Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Dk.Michael Kadeghe
Serikali Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya
imejipanga kuwachukulia hatua kali za
kisheria makampuni yatakayobainika yanunua
kahawa mbichi (CHERRY)kutoka kwa wakulima.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya
Mbozi Dk.Michael Kadeghe alipokuwa akizungumza na Wakulima na Wadau wa zao
la kahawa kwenye katika kituo cha
utafiti wa kahawa (TACRI)cha Mbimba Wilayani Mbozi.
Dr. Kadeghe
alisema kuwa ununuzi wa kahawa mbichi unamyonya mkulima na kusababisha kuwepo kwa matukio ya uhalifu mashambani kwa
Wahalifu kuingia shambani na
chuma kahawa mbichi na kwenda kuuza kwenye makampuni hayo.
Aidha alisema kuwa ununuzi wa kahawa mbichi yanaathiri
uchumi wa Wilaya ya Mbozi kwani zaidi
ya asilimia 80 ya mapato ya Halmashauri hiyo yanetegemea zao la Kahawa.
Alisema
kuwa kilimo cha kahawa ni muhimu katika wilaya hiyo kwani uchumi wa Wananchi
unategemea zao hilo ambapo kila msimu wa kahawa
halmashauri hiyo inakusanya shilingi 2.5 Bilioni.
“Utaratibu umeandaliwa wa jinsi ya kuwakamata
tutakaowabaini wananunua kahawa mbichi kwani kamati ya ulinzi na usalama ya
Wilaya imejipanga na kuweka mikakati yake ya kuhakikisha tabia hii ya
baadhi ya makampuni na watu wanataka kujinufaisha kupitia mkulima
inakomeshwa”alisema
Aidha alisema kuwa serikali Wilaya pia
imeandaa utaratibu wa kugawa bure miche ya kahawa kwa Wakulima ili
kuwawezesha wakulima hasa vijana kuweza kuongeza uzalishaji wa zao
la kahawa na kuweza kuondokana katika umasikini.
“Vijana wengi hawana shughuli za
kufanya hivyo tumeamua kama Wilaya kuhakikisha hakuna vijana wanaoshinda
vijiweni kwa kuwagawia bure miche ya kahawa na kuwapa ruzuku ya
pembejeo ili waweze kujihusisha na kilimo cha zao la kahawa”alisema
Akizungumza
kwa ya Wakulima Mtemi Miya alisema kuwa ubora wa kahawa
katika Mkoa wa Mbeya sio wa kuridhisha kwani kahawa nyingi bado iko kwenye
madaraja ya chini kwani msimu mwaka 2012,2012 karibu asilimia 96.4 ya
kahawa yote ilikuwa katika daraja la tisa.
Alisema kuwa
hali hiyo inachangia kushusha kipato cha Wakulima kwani kwa
sasa kahawa hununuliwa na kulipwa kwa madaraja hivyo wanaiomba
serikali kuwasaidia Wakulima
katika kuhakikisha wanazalisha kahawa yenye ubora unaotakiwa sokoni na kuweza kukuza kipato cha
mkulima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment