Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akipata maelekezo ya jiwe la mpaka wa Tanzania Zambia wa Tunduma kutoka kwa Ofisa wa uhamiaji Japhet Abel mara baada ya kutembelea mpaka huo.
Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akipata maelekezo
ya jiwe la mpaka wa Tanzania Zambia wa Tunduma kutoka kwa Ofisa wa
uhamiaji Japhet Abel mara baada ya kutembelea mpaka huo.
Momba.Zaidi
ya Sh18 bilioni zimekusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)idara ya
forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani
Mbeya katika kipindi cha kuanzia julai 2013 hadi Desemba 2013.
Hayo yalisemwa
na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ya mpaka wa Tunduma Alphonse
Kwikubya mbele ya Naibu Waziri wa Fedha
,Mwigulu Nchemba alipofanya ziara katika mpaka huo kwa lengo la kuangalia
shughuli zinazofanyika katika mpaka .
Alisema kuwa
mapato hayo ni sawa na asilimia 90.34 ambapo
makadilio yalikuwa ni Sh20.8bilioni na kwamba mpaka huo unatoa huduma kwa watu wanaoingia
na kutoka zaidi ya 500 hadi 700 kwa
siku .
Kwikubya
alisema kuwa wengi wa wageni hao
wanatokea nchi za Zambia,Zimbabwe,Botswana,Congo DRC na Afrika Kusini na kwamba
mpaka huo unaurefu wa Kilometa 150 hivyo uthibiti wake unakuwa mgumu kwa
sababu mbali mbali.
Alizitaja
sababu kuu mbili ugumu wa udhibiti wa mpaka huo kuwa ni pamoja na eneo kuwa na
vipenyo vingi haramu na liko wazi sana kupitika kirahisi na wenyeji wa eneo
hilo ambao ni kabila la Wanyamwanga kuwa na mwingiliano mkubwa.
“Wanamwingiliano
mkubwa wa kijamii,kiutamaduni na mila hivyo
kuwahudumia kwa taratibu na sheria za nchi wanaona bughudha kwani wanahisi ni haki yao ya kihistoria hivyo wahalifu wanatumia mwanya
huo kufanya vitendo vyao vya
uhalifu”alisema
Aidha
alieleza changamoto zinazoukabili mpaka huo kuwa ni pamoja na ujenzi holela
katika eneo la mpaka baadhi ya watu wa
tunduma kutokuwa na uzalendo hivyo kuficha kuwezesha wahalifu na wakati
mwingine kupiga vita vyombo vya dola vinaposhughulikia wahalifu kama wavusha
vipodozi visivyoruhusiwa na wafanya
magendo ya sukari.
Alisema
changamoto nyingine kuwa ni pamoja na ukosefu wa umeme mpakani Tunduma ni tatizo
sugu ambalo linaathiri utendaji kazi hasa nyakati za usiku ambapo kituo hufanya
kazi masaa 24.
Momba.Wafanyabiashara wa mamlaka ya mji mdogo Tunduma Wilaya ya
Momba mkoani Mbeya wameishangaa serikali kushindwa kumdhamini mfanyabiashara ambaye ni mwekezaji wa ndani
atakayeweza kutengeneza ajira na badala yake anadhaminiwa mbunge atakayedumu
madarakani kwa miaka mitano.
Waliyasema
hayo jana mbele ya Naibu Waziri wa Fedha
Mwigulu Nchemba katika risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wa chama cha
Wafanyabiashara,viwanda na kilimo(TCCIA) Wilaya ya Momba Simon Kitojo kwenye m kutano uliofanyika katika ukumbi wa
Hoteli ya High Class Tunduma.
“Tunashangaa
tunaposikia mwanasiasa husudani Mbunge ndani ya miaka mitano ya kuchaguliwa
kwake serikali inamdhamini mkopo bila
dhamana yoyote wa zaidi ya Sh300milioni laki ni serikali hiyo hiyo inashindwa
kumdhamini mfanyabiashara ambaye atawekeza
ndani ya nchi kwa muda mrefu zaidi na kuongeza ajira ambayo ndiyo
atitizo na kilio cha serikali yetu cha watu kukosa ajira”alisema Mwenyekiti
huyo
Kitojo
alisema kuwa Serikali kimekuwa kiimba wimbo
wa kutaka kuona Tanzania ina kuwa ni nchi ya viwanda kwa maana ya
kuimarisha sekta ya kilimo na uongezaji wa thamani ya mazao.
”Kwa wimbo
huu hatuoni kama inasema kweli na sisi tunaona kama inaongelea zaidi wawekezaji
wa nje kuliko wa ndani kwa vile wa
tanzania wengi hasa wafanyabiashara wanajulikana nguvu yao na dhamana zao hivyo
hawawezi kuwekeza kwa kiwango kinachotakiwa bila ya serikali kusimama kama
dhamana ya mkopaji kwa kuywa dhama zetu ni za mikopo ya kujikimu tu na sio
kuanzisha miradi mikubwa”alisema
Aidha alisema kuwa kuna changamoto za kimfumo ikiwa
ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara ambpo toka serikalik ilipojitoa kwenye
uchumi hodhi na sekta binafsi kuendesha uchumi huku serikali ikikusanya kodi
pekee hakujawa na elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wake juu ya
kuwaelimisha wafanyabiashara kufanya biashara kwa ufanisi zaidi.
“Tunaiomba serikali ishirikiane na sekta binafsi
kuendesha mafunzo nchi nzima kwa wafanyabiashara kwa lengo la kujua haki
zao,kujitambua,kujua wajibu wake kwa Taifa na hiyo tunaamini itapunguza sana
migongano kati ya serikali na sekta binafsi”alisema
Alisema
kuwa wafanuabiashara wanajiona kama
wameachwa na serikali na wala haitaki kuwahudumia na kwamba wanaonana na
serikali wakati wa kodi na michango mbali mbali pekee.
Momba.Naibu
Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba amesema kuwa eneo ambalo atahakikisha
linafanikiwa katika Wizara hiyo ni ikubana matumizi ikiwa ni pamoja na
kuangalia upya mfumo unaotumika katika sheria ya manunuzi.
Akizungumza
na Wafanyabiashara wa mamlaka ya mji
mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya alisema kuwa alisema kuwa
serikali inabeba mzigo mkubwa kutokana na kuwepo kwa sheria ya manunuzi kwa
kufanya manunuzi ya gharama kubwa badala ya gharama halisi.