"MULUGO AHADI UMEPATA'" |
Friday, December 27, 2013
Wabunge muige mfano wa mbunge huyu
Mbunge wa jimbo la Songwe Wilaya ya Chunya ambaye pia ni Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philip Mulugo akifanya maandalizi ya kuzigawa fedha kiasi cha sh.11.5 kwa ajili ya kuzitoa kama msaada kwa vikundi 23 vidogovidogo vya ujasiliamali (VICOBA) hafla iliyofanyika Mkwajuni jana ambapo kila kikundi kimepata Sh.500,000.
Wednesday, December 18, 2013
Madiwani Wanne wa Chadema wahojiwa na polisi
MADIWANI
wanne kati ya 18 chama cha Demkrasia na maendeleo
Chadema na NCCR Mageuzi katika Jiji la Mbeya juzi walihojiwa na jeshi la polisi Mkoani hapa
kwa tuhuma za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi na diwani wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.
Juzi
Madiwani 18 wa chama cha Demkrasia na maendeleo Chadema na NCCR
Mageuzi katika Jiji la Mbeya walipata taarifa kwa njia ya simu kwa
ajili ya kuhojiwa na jeshi la polisi Mkoani hapa kwa tuhuma
za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na diwani
wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.
Mfanyabiashara wa kubadilisha fedha avamiwa na majambazi
MFANYABIASHARA ya kubadilisha fedha katika mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya Alphonce Mwanjela(36)amevamiwa na kundi la watuwanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kupigwa risasi mguu wa kuliana kuporwa fedha zaidi ya milioni 20 zikiwemo shilingi zakitanzania, Dora za kimarekani,Randi ya Afrika Kusini na kwacha yaZambia.
Akizungumzia tukio hilo kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Barakael
Masaki alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 1:45
jioni juzi na eneo la Sogea makambini Tunduma Wilayani Momba.
Akizungumzia tukio hilo kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Barakael
Masaki alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 1:45
jioni juzi na eneo la Sogea makambini Tunduma Wilayani Momba.
Wakulima Wilayani Chunya Walalamikia ushuru mkubwa wa Mazao
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dedatus Kinawiro akizngumza na Wadau na Wakulima wa zao la Alizeti kutoka maeneo mbali mbali Wilayani Mkoani Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dedatus Kinawiro akizngumza na Wadau na Wakulima wa zao la Alizeti kutoka maeneo mbali mbali Wilayani Mkoani Mbeya
Mkurugenzi wa taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA) Lucas Malangalila akitoa taarifa ya mradi kuwawezesha wakulima wa Alizeti na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki
WAKULIMA wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kuongeza kilimo cha zao la Alzeti ili kuweza kuendana na mahitaji ya soko na kuweza kujipatia kipato na kuondokana na umasikini.
MMOJA wa washiriki wa mafunzo ya mradi kuwawezesha wakulima wa Alizeti na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki akiwasilisha kazi za vikundi katika mafunzo hayo yaliyofanyika Makongorosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
WAKULIMA na Wadau wa
za zao la Alzeti Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
wamelalamikia ushuru mkubwa wa mazao
unaotozwa na halmashauri ya Wilaya hiyo kuanzia shs 3.000
hadi 50;00 kwa madai kuwa unawanyonya Wakulima.
Walitoa malalamiko hayo mbele ya
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo katika mafunzo ya
kuvijengea uwezo vikundi vya Wakulima wa zao la Alizeti yaliyoandaliwa na
kuendeshwa na taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA)
na kufanyika Makongorosi Wilayani humo.
Akizungumza kwa niaba ya
Wakulima hao Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa Alzeti kata ya
lupa tinga tinga Israel Mwampondele alisema kuwa gharama za ushuru
huo ni kubwa na kusababisha wakulima wengi kushindwa kulipa kutokana na kuwepo
kwa gharama katika uzalishaji wa zao hilo.
“Gharama za kilimo cha alzeti
ni kubwa kutokana na upatikanaji hafifu wa pembejeo ikiwa ni pamoja
na mbegu na mbolea wakulima wengi wamekuwa wakilima zao hilo kwa
kiasi kidogo na hivyo tunapata fedha kidogo ambazo hazikidhi
mahitaji”alisema
Akifafanua zaidi
Mwampondele alisema kuwa katika Wilaya hiyo zao la alizeti na
mahindi linatozwa kiasi cha shs.3,000 na zao la ufuta linatozwa kiasi cha
shs.5,000 huku Wilaya nyingine zikitoza ushuru wa mazao kuanzia shs500 hadi 1,000.
"Hata kwenye mageti ya
ushuru hakuna ubao ambao unaainisha vitu ambavyo vinatakiwa kukatiwa ushuru na
kwa kiasi kipi cha pesa,wakataji wanakadilia kutoka kichwani na cha ajabu
zaidi hadi mashudu yanatakiwa kutozwa ushuru "alisema
Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa
Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo alisema kuwa suala la ushuru ni la
kisheria ambapo kiwango chake ni asilimia tano (5%) kwa kila ujazo wa
gunia moja.
“Sijajua hao wa Wilaya
nyingine wanatumia mfumo gani katika kutoza ushuru huo lakini nitafuatilia
halmashauri kuona uhalali wa utozwaji wa ushuru huo kama unazingatia hiyo
sheria ya asilimia tano (5%)”alisema
Aidha aliwataka wakulima na wadau
hao kuendelea kutoa ushuru wa mazao hayo kwa kufuata sheria ili kuepuka
misuguano isiyo la lazima ambayo imekuwa ikijitokeza kutokana na kukwepa
kulipa ushuru na kwamba ushuru huo ni kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya
hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dedatus Kinawiro akizngumza na Wadau na Wakulima wa zao la Alizeti kutoka maeneo mbali mbali Wilayani Mkoani Mbeya
Mkurugenzi wa taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA) Lucas Malangalila akitoa taarifa ya mradi kuwawezesha wakulima wa Alizeti na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki
WAKULIMA wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kuongeza kilimo cha zao la Alzeti ili kuweza kuendana na mahitaji ya soko na kuweza kujipatia kipato na kuondokana na umasikini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa
Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro katika mafunzo katika mafunzo
ya kuvijengea uwezo vikundi vya Wakulima wa zao la Alizeti yaliyoandaliwa
na kuendeshwa na taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu
(KAEA) na kufanyika Makongorosi Wilayani humo.
Alisema kuwa kwa sasa zao la
Alizeti ni muhimu kutokana na mafuta yake kuhitaji kwa wingi sokoni lakini
katika wilaya ya chunya zao hilo linalimwa kidogo pamoja na kuwepo kwa ardhi
kubwa ya kilimo ambayo haitumiki.
Kinawiro alisema kuwa mahitaji ya
mafuta ya alizeti ni tani 334,680 kwa nchi nzima na uzalishaji
ni tani 132,212 kati ya hizo wilaya ya chunya inazalisha tani 17,212
hivyo kuna fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa zao la Alzeti.
Aidha alisema kuwa bado kuna
maeneo makubwa kwa ajili ya shughuli za kilimo ambapo kwa ujumla wilaya
hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 29219 na kwamba kilometa 19278
ndilo linafaa kwa kilimo lakini eneo linalolimwa kwa sasa ni kilometa
2276 pekee.
“Kwa hiyo bado wakulima wa Chunya
wanafursa ya kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti lakini hatuitumii kwa
ufasaha kwani mkulima wa chunya analima nusu heka hadi mbili wakati
kuna maeneo makubwa ambayo yanahitaji kulimwa”alisema
Awali mratibu wa mafunzo
hayo kutoka taasisi ya KAEA Lucas Malangalila
alisema kuwepo kwa mafunzo ni matokeo ya utafiti
wa kina wa kuendeleza zao la alizeti uliofanywa na shirika la maendeleo
la uholanzi (SNV Development) ambalo liliona zao hilo kama mkombozi pekee kwa
Wananchi wa Chunya katika kuwaondolea tatizo la umasikini kupitia fursa
zilizopo.
Malangalila alisema kuwa lengo
la mafunzo hayo ni kuwawezesha Wakulima kuangalia mfumo mwepesi wa
upatikanaji wa pembejeo ikiwa ni pamoja na kuondokana na tatizo la
mbegu zisizo halali na kusababisha wakulima kukosa mazao.
MMOJA wa washiriki wa mafunzo ya mradi kuwawezesha wakulima wa Alizeti na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki akiwasilisha kazi za vikundi katika mafunzo hayo yaliyofanyika Makongorosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya
Saturday, December 14, 2013
Thursday, December 12, 2013
HABARI KATIKA PICHA
Utoaji wa elimu ya afya kwa vijana ni tatizo kwa familia za kiafrika
Washiriki na mafunzo ya haki za afya ya uzazi kwa vijana wakifanya kazi za vikundi yaliyoandaliwa na shirika la AMREF na kufanyika katika chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Morogoro
Imeelezwa
kuwa wazazi na familia za
Kiafrika hawana utaratibu wa kutoa elimu ya afya kwa watoto wao walio na
umri kuanzia miaka 10 hadi 16 kwa madai
kuwa watakuwa wamechangia watoto hao kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.
Hayo yamebainika katika kituo cha watu wanaoishi na
virusi vya Ukimwi Morogoro(WAVUMO)waliokuwa wakizungumza na waandishi wa habari
waliopo katika mafunzo ya haki za afya
ya uzazi kwa vijana yaliyoandaliwa na shirika la utafiti wa madawa na Tiba
(AMREF) walipotembelea kituo hicho.
Tuesday, December 10, 2013
AMREF yawapiga msasa Waandishi na Wahariri Morogoro
Shirika la
utafiti wa madawa na tiba (AMREF) limetoa
mafunzo ya haki za afya ya uzazi kwa vijana kwa baadhi ya Waandishi
wa habari na Wahariri nchini ili kuwajengea uwezo wa kuandika kwa undani habari za afya ya uzazi na kuibua changamoto
zake katika jamii .
Mafunzo hayo
ya siku tatu yanafanyika katika chuo cha
kilimo SUA na kushirikisha waandishi 22 kutoka katika mikoa ya Njombe,Iringa,Mbeya,Morogoro
na dar es Salaam
ambapo pia waraweza kujifunza uandishi wa
habari za kiuchunguzi na maadili ya uandishi wa habari za afya ya uzazi
kwa vijana.
Subscribe to:
Posts (Atom)