Pages

Monday, December 29, 2014

WAKULIMA 1200 WA MPUNGA WILAYA YA KYELA WAINGIA MKATABA WA KUKOPESHWA MBOLEA

 
 Baadhi  ya Wakulima wa zao la Mpunga  Wilaya ya Kyela wakiwa katika kikao cha pamoja cha kupitia mkataba wa kukopeshwa pembejeo za  kilimo na kampuni ya Mtenda Kyela Rice kwa lengo la kuwawezesha kuongeza uzalishaji wa mpunga ulio na ubora na kuweza kukubalika Sokoni.

Sunday, December 7, 2014

WANAFUNZI WALIOSOMA SANGU WAUNDA UMOJA WA KUSAIDIANA KATIKA SHIDA NA RAHA

 Wanafunzi waliosoma Sangu  wanaoishi jijini Dar es salaam wakiwa katika kikao kilichoafanyika katika hotel ya Land Mark jiji Dar es Salaam wakijadiliana jinsi ya kuendeleza umoja huo na Mkutano mkuu unaotarajia kufanyika katika hotel ya GR jijini Mbeya ambapo wote walioko nje ya mbeya watafika kwa ajili ya kuhudhulia mkutano huo Dec 20,2014.

Thursday, December 4, 2014

MTOTO JUSTA MWASOMOLA (9)AOMBA MSAADA WA KIFEDHA KWA AJILI YA KUPATIWA MATIBABU

 Mtoto Justa Mwassomola (9)akiwa nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya alipofika katika ofisi hiyo kwa ajili ya kuomba msaada wa kifedha kwa ajili kupatiwa matibabu ya kuondoa uvimbe huo
MTOTO Justa   Mwasomola akiwa na baba yake mzazi Ephrahimu Mwasomola




RUNGWE .Mtoto Justa Mwasomola  mwenye umri wa miaka tisa mkazi wa kijiji  cha Masebe wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya  anaomba msaada wa fedha kwa ajii ya kupatiwa matibabu ya uvimbe uliopo juu ya pua nakusababisha kushindwa kuendelea na masomo.

CHADEMA WAKITAKA KITI CHA UMEYA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA



MBEYA.Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema)  amesema kuwa  dhamira iliyopo kwa chama hicho ni kuhakikisha  kinatengeneza historia ya kukalia kiti cha Umeya ndani ya halmashauri  ya jiji la Mbeya.