Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika moja ya mikutano yake katika ziara ya siku tatu Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya |
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aikataa
taarifa ya matumizi ya fedha zaidi ya Sh 174 milioni za miradi miwili ya bwawa la maji katika kijiji cha Iyula na Msia
Wilayani Mbozi na kutoa wiki moja kwa
halmashauri ya Wilaya kutoa maelezo ya sahihi ya miradi hiyo.
Katika fedha hizo,
Sh 134 milioni zimetumika katika mradi wa bwawa la maji
katika kijiji cha Iyula huku fedha zilizopokelewa kutoka serikalini zikiwa Sh 250 milioni na nyingine ni Sh40milioni za mradi wa bwawa la maji la kijiji
cha Msia ambapo fedha hizo zimetumika huku mradi ukiwa bado haujaaanza
kutekelezwa.