“Ni miaka 50 tangu Tanganyika ipate uhuru wake mwaka 1961, lakini hatujawahi
kutembelewa na kiongozi yeyote yule wa Kitaifa zaidi ya Diwani, na Afisa
Mtendaji wa Kata ambao tumekuwa tukikutana nao katika shughuli za kila siku,
lakini leo kwa mara ya kwanza tumeshuhudia mbunge wa Jimbo la Songwe”
Hivi
ndivyo walivyaoanza kusema baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Some kilichopo katika
kata ya Gua tarafa ya Kwimba wilaya ya Chunya, umbali wa kilomita zaidi ya 210
kutoka Chunya mjini ambapo Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi na Mbunge
wa jimbo hilo, Philipo Mulugo alifanya ziara hivi karibuni katika kijiji hicho.
Aidha kijiji hicho cha Some kina kaya 642 kati ya hizo 352 ni za
watu ambao hawajiwezi na 147 ndiyo wanaojiweza na wananchi hao
wanategemea shughuli za uvuvi , ufugaji na kilimo katika kuendesha
maisha yao.
Uvuvi
Shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Kijiji hicho zinategemea zaidi uvuvi wa
Samaki pamoja na kilimo, hata hivyo idadi ya samaki wanaovuliwa katika Ziwa
rukwa inazidi kupungua jambo ambalo limeanza kuathiri uchumi wa wakazi wa
kijiji hicho.
Mmoja
wa wakazi wa Kijiji hicho, John Mwala anasema kuwa awali mtu mmoja
alikuwa anaweza kuvua samaki zaidi ya 1000 kwa siku lakini kwa sasa wanavua
samaki chini ya 100 hivyo ni dalili tosha kuwa samaki katika ziwa hilo hakuna.
Hata hivyo anasema hadi sasa hawajui chanzo cha kupungua kwa samaki katika ziwa
hilo na kwamba wanasubiri utafiti wa wataalamu ili waweze kujua nini kifanyike
ili hali ya samaki ilejee katika hali ya kawaida.
Kilimo
Anasema wakazi wa Kijiji hicho wanajishughuli kwa kiasi kidogo na kilimo cha
mahindi na mbogamboga kutokana na hali ya ukame pamoja na ukosefu wa pembejeo
za kilimo ikiwemo mbolea na mbegu.
Mwala anasema kuwa kutokana na mazingira yaliyopo katika kijiji hicho
ni vigumu wananchi wake kupata kwa urahisi pembejeo za kilimo na
Mbegu hivyo huwaamua kuegemea kwenye uvuvi ambao pia kwa sasa hauna
tija.
Aidha anasema kipindi cha miaka ya nyuma, wakazi wa kijij hicho walikuwa
wanalima zao la pamba ambalo baadae Serikali ilizuia kilimo
cha zao hilo kutokana na kuibuka kwa funza mwekundu aliyekuwa anashambulia zao
hilo na kwamba hadi sasa hawajalipwa fedha zao za fidia.
Kuhusu Ufugaji anasema kuwa shughuli za ufugajji ni kidogo na kwamba
wafugaji hufuga mifugo yao na kuitunza hakuna biashara inayofanyika ya
mifugo na wakati fulani wafugaji huama na kuenda kuishi sehemu
nyingine.
Huduma za Afya
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Some Euzebius Mbalamwezi anasema kuwa kijiji hicho
kinakabiliwa na changamoto ya ukosaji wa huduma za afya ambapo wanakijiji
hulazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 20 kufuata huduma za afya
katika makao makuu ya kata.
Anasema
ubovu wa miundombinu hususani barabara imekuwa ni kikwazo kwa magari kuweza
kufika katika kijiji hicho hali inayofanya shughuli za kiuchumi na kijamii kuwa
ngumu katika maisha ya kila siku hivyo msaada wa haraka unahitajika katika
kuboresha miundombinu ya barabara ili kijiji kiweze kufikika kwa urahisi na
kusaidia wanawake wajawazito kwenda Hospitali kwa urahisi kupata huduma za
afya.
“Gari zinazoweza kufika huku ni Landcruser Hadtop ambayo hata hivyo
hufika kwa shida sana kutokana na barabara kuwepo kwenye mlima mkubwa
wenye mawe na haijachongwa vizuri na hiyo gari ya uwindaji ambayo
mmekuja nayo nyie ni kwa sababu imetengezwa maalum kwa ajili
ya
mazingira kama haya ya huku kwetu.”anasema
Huduma ya Maji
Mbalamwezi anasema kuwa katika kijiji hicho kuna tatizo la upatikanaji
wa huduma ya maji ambapo wananchi wanalazimika kutumia maji ya ziwa Rukwa na
maji ya visima vilivyochimbwa kienyeji ambayo siyo safi na salama kwa matumizi
ya binadamu.
Elimu
Kuhusu elimu anasema kuwa katika kijiji hicho kuna shule moja ya
msingi Some ambayo pia mazingira ya kutolea elimu hiyo bado siyo
mazuri”kama unavyoona mwenyewe”anasema Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule
hiyo ,Silas Masawe
Anasema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 1987 na kwamba mpaka sasa
ina vyumba vitano vya madarasa ambapo vitatu ni mabanda yaliyojengwa
kwa miti na mabati, mawili yamejengwa kwa matofari ambapo moja wapo
halina madirisha na halijasakafiwa chini.
Mwl Masawe anasema kuwa pamoja na kuwepo kwa mazingira magumu ya
kufundishia maendeleo ya Wanafunzi darasani yanaridhisha pamoja na
kuwepo na changamoto ya kuwepo na idadi kubwa ya mdondoko kutokana na
wanafunzi wengi kuamua kuacha shule na kukimbilia kwenye shughuli za
uvuvi.
Kiuchimi
Kupungua kwa samaki katika ziwa Rukwa hali ya ukusanyaji wa mapato
katika kijiji hicho ni mbaya na hivyo kushindwa kufanya shughuli za
maendeleo kutokana na kukosa fedha za kuendeshea miradi ya maendeleo.
Mtedanji huyo wa kijiji anasema kuwa mapato ya kijiji hicho kwa
asilimia kubwa yanategemea Samaki mbapo kwa sasa samaki hao hakuna na
baadhi ya Wavuvi wameanza kuondoka na kwenda sehemu nyingine kwa ajili
ya kutafuta riziki.
Anasema kuwa kwa sasa kijiji hicho kinakusanya kuanzia shilingi
100,000 hadi 150,000 kwa mwezi fedha ambazo hazitosherezi kufanya
shughuli za miradi ya maendeleo ya kijiji.
Anafafanua kutokana na hali hiyo maisha ya wakazi wa kijiji cha Some
ni magumu kwani kwa sasa wanakula mlo mmoja kwa siku na kwamba kwa
miradi yamendeleo wanategemea serikali na wafadhili mbali mbali kuja
kutoa misaada kwa ajili miradi
“Tunamshukuru huyu muindaji wa poli la Rukwati Danny Mc
kwani
ametusaidia kwa kutupa kiasi cha shs milioni 30 ambazo tumejengea
vyumba vya madarasa viwili katka shule yetu ya Msingi ya Some na
yamekamilika hivyo kuanzia sasa watoto wetu watahama kutoka katika madarasa
ya vibanda na kuhamia kwenye haya madarasa tuliyofadhiliwa.”anasema
Anasema kuwa Wanaiomba Serikali kukikumbuka kijiji hicho kwa
kukitembelea mra kwa mara na kujionea maisha ya wakazi wa kijiji hicho
ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kwa kuwaletea miradi mbali mbali ya
maendeleo kama ilivyo kwa vijiji vingine.
Mbunge
Mbunge wa jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya
ufundi Philipo Mulugo anasema kuwa ameumizwa sana
mazingira ya kijiji hicho ikiwa ni pamoja na ubovu wa barabara,na
ukosefu wa kituo cha kutolea huduma ya Afya
“Nimeumia sana na hali ya barabara katika kijiji hiki cha some poleni
sana nimejionea mimi mwenyewe kwani hata gari imeshindwa kufika huku na
ndiyo maana nikalazimika kutumia hii gari maalum ya uwindaji ili
niweze kufika na kukutana na wananachi wa kijiji cha Some”anasema
Anasema kuwa kutokana na hali mbaya ya barabara anatoa kisi cha
milioni tatu na Mwindaji na mwekezaji wa poli la Rukwati pia anatoa
milioni tatu ambazo kwa pamoja zitatumika kwa jili ya kuchonga
barabara hiyo kwa kuwatumia vijana ambao ni wananchi wa kijiji hicho.
Anasema kuwa fedha hizo siyo kwa ajili ya kumtumia mkanadarasi bali
wakusanywe vijana kutoka katika kijiji hicho ambapo watachonga
barabara hiyo kwa kutumia dhana za kawaida na ndiyo watalipwa fedha
hizo zote milioni sita.
Kwa upande wa Kituo cha kutolea huduma ya Afya mbunge huyo amejitolea
kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa
zahanati ambapo wananchi wataanza kuchangia nguvu zao kwa kufyatua
tofari tayari kwa kuanza ujenzi wa zahanati hiyo mwishoni mwa mwaka
huu 2011.
Amewataka Wananchi wa kijiji cha Some kujitoa na kushiriki kakamilifu
katika kutekeleza miadi ya maendelea na kuithamini michango na
misaada wanayoletewa kwa kuitunza ili kijiji hicho kiwezekuwa na
madiliko kwa kuwa maendeleo kama vijiji vingine.
Aidha amewataka kuanza kulima mazao mchanganyiko ya biasharana chakula
badala ya kutegemea samaki pekee ili kuweza kepukana na njaa ambayo
inaweza ikatokea wakati wowote kutokana na ziw hilo kupungua samaki .
Naibu Waziri wa elimuna mafunzo ya ufundi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Songwe Philip Mulugo akiwa katika kijiji cha Some kata ya Gua Wilaya ya Chunya