Pages

Wednesday, December 18, 2013

Wakulima Wilayani Chunya Walalamikia ushuru mkubwa wa Mazao

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dedatus Kinawiro akizngumza na Wadau na Wakulima wa zao la  Alizeti  kutoka maeneo mbali mbali  Wilayani Mkoani Mbeya  



WAKULIMA  na Wadau wa  za zao la Alzeti Wilaya ya Chunya  Mkoani Mbeya   wamelalamikia  ushuru  mkubwa  wa mazao  unaotozwa na halmashauri ya Wilaya  hiyo kuanzia  shs 3.000  hadi 50;00  kwa madai kuwa unawanyonya Wakulima.



Walitoa malalamiko hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo  katika mafunzo ya  kuvijengea uwezo vikundi vya Wakulima wa zao la Alizeti yaliyoandaliwa na kuendeshwa na taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA)  na  kufanyika  Makongorosi Wilayani  humo.

 Akizungumza kwa niaba ya Wakulima hao Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima  wa Alzeti  kata ya lupa tinga tinga  Israel Mwampondele  alisema kuwa gharama za ushuru huo ni kubwa na kusababisha wakulima wengi kushindwa kulipa kutokana na kuwepo kwa gharama katika uzalishaji wa zao hilo.



“Gharama za  kilimo cha alzeti ni kubwa  kutokana na upatikanaji  hafifu wa pembejeo ikiwa ni pamoja na mbegu na mbolea  wakulima  wengi wamekuwa wakilima zao hilo kwa kiasi kidogo na hivyo  tunapata fedha kidogo ambazo hazikidhi  mahitaji”alisema



Akifafanua  zaidi  Mwampondele alisema kuwa  katika Wilaya hiyo zao la alizeti  na mahindi linatozwa kiasi cha shs.3,000 na  zao la ufuta linatozwa kiasi cha shs.5,000 huku Wilaya nyingine zikitoza ushuru wa mazao kuanzia shs500 hadi 1,000.



"Hata kwenye mageti  ya ushuru hakuna ubao ambao unaainisha vitu ambavyo vinatakiwa kukatiwa ushuru na kwa kiasi kipi cha pesa,wakataji wanakadilia kutoka kichwani na cha ajabu zaidi  hadi  mashudu yanatakiwa kutozwa ushuru "alisema



Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo alisema kuwa suala la ushuru  ni la kisheria ambapo  kiwango chake ni asilimia tano (5%) kwa kila ujazo wa gunia moja.



“Sijajua hao  wa Wilaya nyingine wanatumia mfumo gani katika kutoza ushuru huo lakini nitafuatilia halmashauri kuona uhalali wa utozwaji wa ushuru huo kama unazingatia hiyo sheria ya asilimia tano (5%)”alisema



Aidha aliwataka wakulima na wadau hao kuendelea kutoa ushuru wa mazao  hayo kwa kufuata sheria ili kuepuka misuguano  isiyo la lazima ambayo imekuwa ikijitokeza kutokana na kukwepa kulipa ushuru  na kwamba ushuru huo ni kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya hiyo.






 Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dedatus Kinawiro akizngumza na Wadau na Wakulima wa zao la  Alizeti  kutoka maeneo mbali mbali  Wilayani Mkoani Mbeya 


Mkurugenzi wa  taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA) Lucas Malangalila akitoa taarifa ya mradi  kuwawezesha wakulima wa Alizeti  na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna  ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki


WAKULIMA  wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kuongeza kilimo cha zao la  Alzeti  ili kuweza kuendana na mahitaji ya soko na kuweza kujipatia kipato na kuondokana na umasikini.

 
 Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro  katika mafunzo katika  mafunzo ya  kuvijengea uwezo vikundi vya Wakulima wa zao la Alizeti yaliyoandaliwa na kuendeshwa na taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA)  na  kufanyika  Makongorosi Wilayani  humo.


Alisema kuwa kwa sasa  zao la Alizeti ni muhimu kutokana na mafuta yake kuhitaji kwa wingi sokoni lakini katika wilaya ya chunya zao hilo linalimwa kidogo pamoja na kuwepo kwa ardhi kubwa ya kilimo ambayo haitumiki.


Kinawiro alisema kuwa mahitaji ya mafuta ya alizeti ni tani 334,680 kwa  nchi nzima  na uzalishaji ni  tani 132,212 kati ya hizo wilaya ya chunya inazalisha tani 17,212 hivyo kuna fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa zao la Alzeti.


Aidha alisema  kuwa bado kuna maeneo makubwa  kwa ajili ya shughuli za kilimo ambapo kwa ujumla wilaya hiyo ina  ukubwa wa kilometa za mraba 29219 na kwamba  kilometa 19278 ndilo linafaa kwa kilimo lakini eneo linalolimwa  kwa sasa ni kilometa 2276 pekee.


“Kwa hiyo bado wakulima wa Chunya wanafursa ya kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti lakini hatuitumii kwa ufasaha kwani  mkulima wa chunya analima nusu heka hadi  mbili wakati kuna maeneo makubwa ambayo yanahitaji kulimwa”alisema 


Awali  mratibu wa mafunzo hayo  kutoka   taasisi ya KAEA  Lucas Malangalila alisema  kuwepo kwa  mafunzo   ni matokeo  ya utafiti wa kina wa kuendeleza zao la alizeti uliofanywa na shirika  la maendeleo la uholanzi (SNV Development) ambalo liliona zao hilo kama mkombozi pekee kwa Wananchi wa Chunya  katika kuwaondolea tatizo la umasikini kupitia fursa zilizopo.


Malangalila alisema kuwa  lengo la mafunzo hayo  ni kuwawezesha Wakulima kuangalia  mfumo mwepesi wa  upatikanaji wa  pembejeo ikiwa ni pamoja na kuondokana na tatizo la mbegu zisizo halali na kusababisha wakulima kukosa mazao.



 MMOJA wa washiriki wa mafunzo ya  mradi  kuwawezesha wakulima wa Alizeti  na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna  ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki akiwasilisha kazi za vikundi katika mafunzo hayo yaliyofanyika Makongorosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya

0 comments: