Pages

Thursday, June 19, 2014

JAMMBAZI LAUAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI NA POLISI TUNDUMA MBEYA



 Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akionyesha Bunduki  aiana ya ShortGun iliyokamatwa  kwenye tukio la majibizano ya risasi baina ya majambazi na askari polisi katika eneo la Msikitini Mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya na kusababisha kifo cha jambazi mmoja .



 Baadhi  ya wandishi wa habari Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye chumba cha mikutano katika ofisi ya kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya


MBEYA.Mtu mmoja anayesadikika kuwa ni jambazi  ameuwawa katika tukio la kurushiana  risasi na askario polisi  na  kupigwa risasi  ubavu katika  eneo la msikitini mji mdongo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.

Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya  Ahmed Msangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea  leo majira ya saa 11 Alfajili  baada ya marehemu huyo akiwa na mwenzake kurushiana risasi na askari polisi mara baada ya kujaribu kuwasimamisha.
Alisema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa Walinzi wa usiku katika eneo hilo kuwatilia shaka watu hao  kuwa wanania ya kufanya uhalifu  wa kutumia silaha  na ndipo  askari waliokuwa doria walifika katika eneo hilo  na kufanya msako mkali.

“Kutokana na taarifa hizo msako  mkali ulianza   wa kuwatafuta  watuhumiwa  na ilipofika majira ya saa 11:00 alfajili ya leo  walikutana na watu wawili waliowatilia shaka kutokana na jinsi walivyovaa  kulingana maelekezo  yaliyotolewa na  walinzi “alisema 

Msangi alisema kuwa  kati ya watu hao mmoja alikuwa amevaa  jaketi kubwa  jeusi na  mwingine akiwa amebeba mfuko mkubwa , wakati  polisi wakijaribu kuwasimamisha  watu hao walianza kukimbia na mmoja aliyekuwa amevaa jaketi alipofika umbali wa mita 20 alitoa silaha bunduki na kuanza kufyatua risasi ovyo uelekero wa askari.

“Baada ya kuona hivyo askari walijibu na katika majibizano hayo ya kurushiana  risasi  jamabazi mwenye silaha alipigwa risasi ubavuni na kufariki dunia  papo hapo na kufanikiwa kukamata bunduki moja aiana  ya AK – 47 yenye  namba 592058 ikiwa na risasi 25  kwenye magazine yenye  uwezo wa kubeba risasi 30”alisema 

Alisema kuwa  mtuhumiwa mmoja aliyekuwaamaebeba mfuko  mkubwa alifanikiwa kukimbia  na kwamba  baada ya upekuzi marehemu alikutwa na kitambulisho cha mpiga kura chenye jina la Joseph Thadei  Kapinga   mzaliwa  Songea  Ruvuma  lakini  ni mkazi wa Mafiga Morogoro.

Alisema kuwa katika tukio  hakuna madhara yoyote yaliyotokewa kwa wanananchi na ashkari polisi  na kwamba upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa aliyerkimbia pamoja na mtandao wao wa ujambazi.



0 comments: