Pages

Thursday, June 19, 2014

BASI LA NEWFORCE LAUA WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI IGURUSI MBEYA

Mbeya.Watu  wawili wamekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa baada ya  kugongwa  na basi  la kampuni ya Newforce  kuligonga gali lingine aina ya Fuso na kuacha njia na kuwagonha watembea kwa mguu  katika kijiji cha Igurusi Wilaya ya Mbarali  Mkoani Mbeya .

 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi aliwataja waliokufa katika  ajali hiyo kuwa ni pamoja na Theresia Hingi (65) na Mary Kizito (26)  wote wakazi wa igurusi  ambapo walifariki papo hapo.


Alisema  kuwa  kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12:00 jioni  katika kijiji cha Igurusi barabara ya Mbeya Njombe  na kuhusisha basi la kampuni ya Newforce lenye namba za usajili T. 952 CGU aina ya Scania.

Msangi  kuwa basi hilo  lilikuwa likitokea jijini Dar  es  salaam kuja Mbeya  lilipofika katika eneo la Igurusi liligonga gari linginel enye namba za usajili T. 954 AMH aina ya Fuso  lililokuwa likiendeshwa  na  Tupa Anyosisye(32) mkazi wa Kiwira tukuyu  na kasha kuacha njia na kuwagonga watembea kwa mguu.

Alisema kuwa katika ajali hiyo watu wengine wanne wamejeruhiwa  kati yao ni abiria mwanaume mmoja na wanawake watatu  watembea kwa miguu ambao majina yao hayajafahamika na kwamba walikimbizwa katika hospitali ya mission Chimala.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni mwendo kasi wa basi la Newforce na kwamba dereva wa basi hilo alikimbia mara baada  ya ajali na jeshi la polisi linaendelea kumsaka kwa ajili ya kufikishwa mbele ya sheria.

Wakati huo huo Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Suzane Mhendwa (45) mkazi wa kijiji cha uhamila Wilayani Mbarali ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani baada ya kutokea kwa mzozo baiana yake na mtuhumiwa nyumbani kwao.

Msangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea  jana usiku majira ya saa 1:00 katika kitongoji cha CCM Wilaya ya Mbarali ambapo marehemu alikuwa na mzozo na mtu anayedaiwa kuwa ni ndugu yake na nipo alipochomwa kisu na kufa papo hapo  na kwamba chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa na mtuhumiwa  anatafutwa


0 comments: