Pages

Friday, December 27, 2013

Wabunge muige mfano wa mbunge huyu

 Mbunge wa jimbo la Songwe Wilaya ya Chunya ambaye pia ni Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philip Mulugo akifanya maandalizi ya kuzigawa fedha kiasi cha sh.11.5 kwa ajili ya kuzitoa kama msaada kwa vikundi  23 vidogovidogo vya ujasiliamali (VICOBA) hafla iliyofanyika Mkwajuni  jana  ambapo kila kikundi kimepata  Sh.500,000.
Mwemyekiti  wa VOCOBA jimbo la Songwe  Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Azizi Adam akimwangalia kwa makini mbunge wa jimbo la Songwe Philip Mulugo wakati akizipanga fedha hizo kiasi cha Sh 11.5 milioni kwenye kiti tayari  kuzikabidhi kwa viongozi wa vikundi hivyo

"MULUGO  ahadi umepata"ndiyo kauli mbiu ya mbunge huyo jimboni kwake  akiwa na lengo la kutimiza ahadi kwa wapiga kura wake hapo akiwa ameshika  fedha kiasi cha sh.miloni 11.5 kwa ajili ya kuzikabidhi vikundi vya VICOBA jimboni kwake juzi

"MULUGO  AHADI UMEPATA'"

Wednesday, December 18, 2013

Madiwani Wanne wa Chadema wahojiwa na polisi



MADIWANI   wanne kati  ya  18 chama cha Demkrasia na maendeleo   Chadema na NCCR Mageuzi  katika Jiji la Mbeya  juzi walihojiwa  na   jeshi la polisi Mkoani hapa  kwa tuhuma za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na diwani wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.

Juzi Madiwani 18 wa chama cha Demkrasia na maendeleo   Chadema na NCCR Mageuzi  katika Jiji la Mbeya walipata taarifa  kwa njia ya simu kwa ajili ya   kuhojiwa na jeshi la polisi Mkoani hapa  kwa tuhuma za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na diwani wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.

Mfanyabiashara wa kubadilisha fedha avamiwa na majambazi





MFANYABIASHARA ya kubadilisha fedha  katika mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya Alphonce Mwanjela(36)amevamiwa na kundi la watuwanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kupigwa risasi mguu wa kuliana kuporwa  fedha  zaidi ya milioni 20 zikiwemo shilingi  zakitanzania, Dora za kimarekani,Randi ya Afrika Kusini na kwacha yaZambia.

Akizungumzia tukio hilo kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Barakael
Masaki alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana   majira ya saa 1:45
jioni juzi na  eneo la Sogea makambini Tunduma Wilayani Momba.

Wakulima Wilayani Chunya Walalamikia ushuru mkubwa wa Mazao

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dedatus Kinawiro akizngumza na Wadau na Wakulima wa zao la  Alizeti  kutoka maeneo mbali mbali  Wilayani Mkoani Mbeya  



WAKULIMA  na Wadau wa  za zao la Alzeti Wilaya ya Chunya  Mkoani Mbeya   wamelalamikia  ushuru  mkubwa  wa mazao  unaotozwa na halmashauri ya Wilaya  hiyo kuanzia  shs 3.000  hadi 50;00  kwa madai kuwa unawanyonya Wakulima.



Walitoa malalamiko hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo  katika mafunzo ya  kuvijengea uwezo vikundi vya Wakulima wa zao la Alizeti yaliyoandaliwa na kuendeshwa na taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA)  na  kufanyika  Makongorosi Wilayani  humo.

 Akizungumza kwa niaba ya Wakulima hao Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima  wa Alzeti  kata ya lupa tinga tinga  Israel Mwampondele  alisema kuwa gharama za ushuru huo ni kubwa na kusababisha wakulima wengi kushindwa kulipa kutokana na kuwepo kwa gharama katika uzalishaji wa zao hilo.



“Gharama za  kilimo cha alzeti ni kubwa  kutokana na upatikanaji  hafifu wa pembejeo ikiwa ni pamoja na mbegu na mbolea  wakulima  wengi wamekuwa wakilima zao hilo kwa kiasi kidogo na hivyo  tunapata fedha kidogo ambazo hazikidhi  mahitaji”alisema



Akifafanua  zaidi  Mwampondele alisema kuwa  katika Wilaya hiyo zao la alizeti  na mahindi linatozwa kiasi cha shs.3,000 na  zao la ufuta linatozwa kiasi cha shs.5,000 huku Wilaya nyingine zikitoza ushuru wa mazao kuanzia shs500 hadi 1,000.



"Hata kwenye mageti  ya ushuru hakuna ubao ambao unaainisha vitu ambavyo vinatakiwa kukatiwa ushuru na kwa kiasi kipi cha pesa,wakataji wanakadilia kutoka kichwani na cha ajabu zaidi  hadi  mashudu yanatakiwa kutozwa ushuru "alisema



Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawilo alisema kuwa suala la ushuru  ni la kisheria ambapo  kiwango chake ni asilimia tano (5%) kwa kila ujazo wa gunia moja.



“Sijajua hao  wa Wilaya nyingine wanatumia mfumo gani katika kutoza ushuru huo lakini nitafuatilia halmashauri kuona uhalali wa utozwaji wa ushuru huo kama unazingatia hiyo sheria ya asilimia tano (5%)”alisema



Aidha aliwataka wakulima na wadau hao kuendelea kutoa ushuru wa mazao  hayo kwa kufuata sheria ili kuepuka misuguano  isiyo la lazima ambayo imekuwa ikijitokeza kutokana na kukwepa kulipa ushuru  na kwamba ushuru huo ni kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya hiyo.






 Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dedatus Kinawiro akizngumza na Wadau na Wakulima wa zao la  Alizeti  kutoka maeneo mbali mbali  Wilayani Mkoani Mbeya 


Mkurugenzi wa  taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA) Lucas Malangalila akitoa taarifa ya mradi  kuwawezesha wakulima wa Alizeti  na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna  ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki


WAKULIMA  wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wametakiwa kuongeza kilimo cha zao la  Alzeti  ili kuweza kuendana na mahitaji ya soko na kuweza kujipatia kipato na kuondokana na umasikini.

 
 Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro  katika mafunzo katika  mafunzo ya  kuvijengea uwezo vikundi vya Wakulima wa zao la Alizeti yaliyoandaliwa na kuendeshwa na taasisi ya utetezi wa mazingira na kilimo endelevu (KAEA)  na  kufanyika  Makongorosi Wilayani  humo.


Alisema kuwa kwa sasa  zao la Alizeti ni muhimu kutokana na mafuta yake kuhitaji kwa wingi sokoni lakini katika wilaya ya chunya zao hilo linalimwa kidogo pamoja na kuwepo kwa ardhi kubwa ya kilimo ambayo haitumiki.


Kinawiro alisema kuwa mahitaji ya mafuta ya alizeti ni tani 334,680 kwa  nchi nzima  na uzalishaji ni  tani 132,212 kati ya hizo wilaya ya chunya inazalisha tani 17,212 hivyo kuna fursa kubwa ya kuongeza uzalishaji wa zao la Alzeti.


Aidha alisema  kuwa bado kuna maeneo makubwa  kwa ajili ya shughuli za kilimo ambapo kwa ujumla wilaya hiyo ina  ukubwa wa kilometa za mraba 29219 na kwamba  kilometa 19278 ndilo linafaa kwa kilimo lakini eneo linalolimwa  kwa sasa ni kilometa 2276 pekee.


“Kwa hiyo bado wakulima wa Chunya wanafursa ya kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti lakini hatuitumii kwa ufasaha kwani  mkulima wa chunya analima nusu heka hadi  mbili wakati kuna maeneo makubwa ambayo yanahitaji kulimwa”alisema 


Awali  mratibu wa mafunzo hayo  kutoka   taasisi ya KAEA  Lucas Malangalila alisema  kuwepo kwa  mafunzo   ni matokeo  ya utafiti wa kina wa kuendeleza zao la alizeti uliofanywa na shirika  la maendeleo la uholanzi (SNV Development) ambalo liliona zao hilo kama mkombozi pekee kwa Wananchi wa Chunya  katika kuwaondolea tatizo la umasikini kupitia fursa zilizopo.


Malangalila alisema kuwa  lengo la mafunzo hayo  ni kuwawezesha Wakulima kuangalia  mfumo mwepesi wa  upatikanaji wa  pembejeo ikiwa ni pamoja na kuondokana na tatizo la mbegu zisizo halali na kusababisha wakulima kukosa mazao.



 MMOJA wa washiriki wa mafunzo ya  mradi  kuwawezesha wakulima wa Alizeti  na kuangalia mfumo mwepesi wa upatikanaji wa pembejeo na namna  ya kudhibiti uingizaji wa mbegu feki akiwasilisha kazi za vikundi katika mafunzo hayo yaliyofanyika Makongorosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya

Thursday, December 12, 2013

HABARI KATIKA PICHA

Mhariri wa makala  wa Gazeti la Mwananchi  Florian Ndyesumbilahi  akibadilishana mawazo na  mwakilishi wa gazeti la Uhuru Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa UVCCM  Mkoa wa Iringa Tumain Msowoya  katika  mafunzo ya haki za afya ya uzazi kwa vijana  yaliyoandaliwa na AMREF  na kufanyika katika chuo kikuu cha kilimo  cha Sokoine(SUA)mjini Morogoro 
Afisa wa programu ya sheria na uwajibikaji  wa  vyombo vya habari katika baraza la habari Tanzania (MCT) uwajibikaji Paul Mallimbo aliyebeba kompyuta mpakato (LAPTOP) akisikiliza majadiliano ya washiriki wa   wa mafunzo ya Haki za afya  ya uzazi kwa vijana yaliyoandaliwa naAMREF mjini Morogoro.
washiriki wa   wa mafunzo ya Haki za afya  ya uzazi kwa vijana yaliyoandaliwa naAMREF mjini Morogoro wakifanya kazi za vikundi 

Utoaji wa elimu ya afya kwa vijana ni tatizo kwa familia za kiafrika

 Washiriki na mafunzo ya haki za afya ya uzazi kwa vijana wakifanya kazi za vikundi yaliyoandaliwa na  shirika la AMREF na kufanyika katika  chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Morogoro

 Imeelezwa  kuwa  wazazi na familia za Kiafrika hawana utaratibu wa kutoa elimu ya afya kwa watoto wao walio na umri  kuanzia miaka 10 hadi 16 kwa madai kuwa watakuwa wamechangia  watoto hao  kujiingiza katika  mahusiano ya kimapenzi.

Hayo yamebainika katika kituo cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Morogoro(WAVUMO)waliokuwa wakizungumza na waandishi wa habari waliopo katika mafunzo ya haki  za afya ya uzazi kwa vijana yaliyoandaliwa na shirika la utafiti wa madawa na Tiba (AMREF)  walipotembelea kituo hicho.

Tuesday, December 10, 2013

AMREF yawapiga msasa Waandishi na Wahariri Morogoro








Shirika la utafiti wa madawa na tiba (AMREF) limetoa  mafunzo  ya haki za afya  ya uzazi kwa vijana kwa baadhi ya Waandishi wa habari  na  Wahariri nchini ili kuwajengea uwezo wa    kuandika kwa undani  habari za afya ya uzazi na kuibua changamoto zake katika jamii .

Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika  katika chuo cha kilimo  SUA  na kushirikisha waandishi  22 kutoka katika mikoa ya Njombe,Iringa,Mbeya,Morogoro na   dar es  Salaam ambapo pia waraweza kujifunza uandishi wa  habari za kiuchunguzi na maadili ya uandishi wa habari za afya ya uzazi kwa vijana.