Pages

Sunday, May 25, 2014

HABARI KATIKA PICHA ZA MATUKIO YA MISS MBEYA VIJIJINI

  Ofisa uhusiano wa nje wa kampuni ya bia(TBL) Abubakar Mansoli akimkabidhi mshindi wa mashindano ya urembo ya Miss Mbeya vijijini Atukuzwe Fabian zawadi ya seti  Kopyuta yenye thamani Sh800,000 baada ya kunyakua Taji hilo katika ukumbi wa Royal  Tughimbe Mbalizi Mbeya vijijini.Picha na brandy Nelson
 Mshindi wa  kwanza  wa Miss Mbeya vijijini aliyekaa akiwa  katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Pendo Nelson na watatu  Neema Tadei


 Washiriki wa shindano la uremb la Miss Mbeya vijijini wakitoa burudani mbele ya wageni waalikwa katika ukumbi wa Royal Tughimbe Mbalizi Mbeya vijijini.

 Kikundi cha burudani  kutoka Mbalizi  kikionyesha show kali kama mfano wa kikundi cha THT

 Warembo wakionyesha show
 Jaji msaidizi wa mashindano ya  kumsaka  Miss Mbeya vijijini  Mary Gumbo akizungumza katika mashindano hayo


. Mkazi wa kijiji cha  Mbalizi Atukuzwe Fabiani  jana aliibuka mshindi wa Miss Mbeyavijijini baada ya kubwaga warembo wenzie 12 katika  mashindano yaliyofanyika  katika ukumbi wa Royal Tughimbe  na kujinyakulia zawadi ya seti Kompyuta yenye thamani  ya  ya Sh 800,000.

Akitangaza matokeo ya mashindano hayo  jaji mkuu wa mashindano hayo Maulid Lyoba ambaye ni afisa mauzo wa kampuni ya bia ya TBL  alisema kuwa  nafasi ya pili imechukuliwa na Pendo  Nelson ambaye alizawadiwa  meza ya kioo (Dressing table).



Lyoba alimtaja mshindi wa  tatu katika mashindano hayo kuwa ni Neema Tadei ambaye alikabidhiwa zawadi ya seti ya  radio  yenye thamani ya Sh250,000.


Akizungumzia ushindi huo mrembo huyo  Miss Mbeyavijijini  alisema kuwa atatumia nafasi hiyo katika kuhamasisha jamii kuwasaidia watotoambao wameshindwa kuendelea na shule na wale wa mitaani.

"Nashukuru nimeshinda nafasi hii na ninaahidi sitobweteka nitaitumia vizuri kwa kuhakikisha nashiriki katika shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuihamasisha serikali kuongeza vitanda katika wodi za wakina mama wajawazito na watoto na wakina mama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali"alisema

Kwa upande wake Ofisa uhusiano wa nje wa kampuni ya bia(TBL) Abubakar Mansoli alisema kuwa pamoja na zawadi walizokabidhiwa  mshindi wa kwanza hadi wa  watatu,watashiriki mashindano ya kumsaka mrembo wa Mkoa wa Mbeya (MissMbeya 2014).
Alisema kuwa warembo hao wataungana na wenzao kutoka jiji la Mbeya (Miss city Center) ambao tayari wameshapatiakana ambapo mashindano ya Mkoa yanatarajiwa kufanyika mwe Juni mwaka huu.

0 comments: