Pages

Sunday, May 25, 2014

PSPF YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA WA THAMANI YA SH 10 MILIONI KWA WAHANGA WA MAFURIKO KYELA

 Mkuu wa Wilaya Kyela Mkoani Mbeya  Magreth Malenga akipokea msaada wa mafuta ya kula kutoka kwa  Afisa wa fedha wa mfuko wa pesheni kwa watuishi wa Umma (PSPF)Idd Sekondo  wakati wa kukabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko Wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya Kyela Mkoani Mbeya  Magreth Malenga akipokea gunia la mchele  kutoka kwa  Afisa  mfawidhi  Mkoa wa Mbeya  wa   mfuko wa pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF)Said Kipindura  wakati wa kukabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko Wilayani humo.

 Afisa  mfawidhi wa  Mkoa wa Mbeya  wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF)Said Kipindura  akiwa amebeba ndoo za mafuta ya kula akizipeleka  stoo wakati wa kukabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko Wilayani





Zaidi ya Sh4.5bilioni  zinahitajika kwa ajili ya kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara na shule yaliyoharibiwa na mvua na kusababisha kutokea kwa mafuriko katika Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Malenga  mara baada ya  kupokea  msaada wa chakula kutoka mfuko wa pensheni kwa watumushi wa Umma(PSPF)wenye  thamani ya Sh10milioni kwa ajili ya wahanga wa mafuriko.


Alisema kuwa kutokana na mafuriko hayo barabara za halmashauri ya Wilaya zimeharibiwa vibaya ikiwa ni pamoja na zile zilizopo chini ya wakala wa barabara Tanzania (Tanroad)ambapo matengenezo ya haraka yanahitajika kwa ajili ya kurudisha mawasiliano kama ilivyo awali.

Mkuu huyo alisema kuwa kutokana na uharibifu huo  zaidi ya Sh2.3bilioni ambapo kwa upande wa shule za msingi nane na moja ya Sekondari  zinahitajika zinahitajika  Sh2.3bilioni kwa ajili ya matengenezo  na kurudisha katika kazi yake ya awali.

“Kutokana na mafuriko hayo kuna changamoto nyingi ambazo tunakabiliwa nazo katika masuala ya elimu kwani hata maabara ya baadhi ya shule zetu zimeharibiwa vibaya na hivyo kusababisha wanafunzi wa kidato cha nne kushindwa kufanya mazoezi ya vitendo katika mtihani wao wa mwisho kwa baadhi ya shule”alisema

Alisema  kuwa  jumla ya kaya 3983  zenye watu 18,976 ziliathiliwa na mafuriko hayo na kwamba  kaya 235 zenye idadi ya  watu 1087 ndiyo zimefikiwa  ambapo mifugo zaidi ya 3000 ilisombwa na maji.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Afisa mfawidhi  wa PSPF Mkoa wa Mbeya Said Kipindura alisema kuwa mfuko huo umetoa  kilo 4800 za mchele,maharagwe kilo 2000 na mafuta ya kula lita 600 ambavyo vyote vinathamani ya Sh10milioni.

Kipindula  alisema kuwa  mfuko huo unatambua kuwa unawajibu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidiana na serikali katika   kuisaidia jamii mara inapokuwa imekumbwa na maafa.


 

0 comments: