Pages

Tuesday, September 30, 2014

WAANDISHI WA HABARI WALIOPATA RUZUKU TMF WAPATIWA MAFUNZO YA AWALI

Baadhi ya waandishi wa habari waliopata ruzuku  ya TMF  ya kuandika habari za vijijini  wakiwa katika mafunzo ya awali katika ukumbi wa TMF Jijini Dar es salaam

Wednesday, September 3, 2014

WACHEZAJI WA TANZANIA PRISONS WALIMLILIA LOVENESS NDIBALEMA



Mume wa marehemu  Loveness Ndibalema, Ngemera Ndibalema akipita kwenye jeneza la mkewe wakati wa kuuaga mwili nyumbani kwake Forest jioni hii.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKARABATI MADARASA

 MSTAHIKI Meya wa jiji .la Mbeya Atanas akizungumza katika hafla ya kuzindua vyumba vya madarasa vinne na jengo la Utawala katika shule ya msingi Hassanga  Uyole jijini hapa  baada kufanyiwa ukarabati na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliogharimu  Sh.31.5milioni.

Tuesday, September 2, 2014

JESHI LA POLISI LAZIMA MAANDAMANO YA WAUMINI ZAIDI YA 500 WA KANISA LA MORAVIAN MBEYA

Mbeya.Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya, limezuia  maandamano ya  waumini zaidi ya 500 wa   Kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi, yaliyotakiwa kufanyika leo,  ya kushinikiza kufanyika mkutano wa dharula wa Sinodi  kwa lengo la kumaliza mgogoro wao uliodumu   kwa mwaka mmoja na nusu.

Kanisa la Moraviani  jimbo lakusini magharaibi  limekuwa na mgogoro uliodumu zaidi ya mwaka mmoja . mara baada kumvua  madaraka  Mwenyekiti wa jimbo  hilo Nosigwe Buya   na  kusimamishwa kazi wachungaji watano waliodaiwa kuhusika kumtetea mwenyekiti huyo.

Akizungumza na  gazeti hili Mwenyekiti wa waumini hao Frank Phiri alisema kuwa leo walipanga kufanya maandamano ya amani kwa lengo la kushinikiza kufanyika kuitishwa mkutano wa Sinodi baada ya kuona viongozi wa kanisa hilo hawafuati maamuzi  na maagizo ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama  Wilaya ya Mbeya.

“ Tulifiata taratibu zote za kuomba kibali cha kufanya maandamano na tayari waumini kutoka  Wilaya zingine walishaingia tangu  lakini cha kushangaza polisiwamtuzuia kufanya hivyo kwa madai kuwa wanahofu vurugu zinaweza kutokea  kitu ambacho tunaamini sisi kuwa siyo  cha ukweli”alisema

Alisema kuwa  juzi siku ya ijumaa waliwasilisha barua ya kuomba kibali  katika ofisi wa mkuu wa polisi wa Wilaya ya Mbeya (OCD ) ambaye alikiri kuipokea na kuwataka warudi jumamosi ambapo walipofika  ofisini kwake walimkuta OCD huyo akiwa na katibu mkuu wa  jimbo hilo.

“Hali  hii inatufanya tukose imani na serikali yetu kwani  kama  viongozi  wa kanisa wameshindwa kufuata maaagizo na maamuzi  ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya  ya kumrudisha  Mwenyekiti katika nafasi yake  na badala yake wanachukua uwamuzi mwingine wa kuwafukuza wachungaji watano  sasa sisi waumini  wanataka tuwe upande gani”alisema 

Alisema kuwa kama waumini wanaamini kuwa  mkutano wa  dharula wa Sinodi  ndiyo unaweza  kumaliza mgogoro huo na kuliweka kanisa  pamoja kama katiba inavyoeleza  ‘lakini hawa wenzetu viongozi hawataki kuitisha Sinodi  wakatgi ndiyo iliyowaweka  madarakani  kufanya hivyo ni kuliua kanisa  kwani mgogoro huu hauwezi kuisha bila ya kuitishwa kwa mkutano huu.”alisema

Akieleza sababu za  kuzuia  maandamano hayo  kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya  Ahmed Msangi alisema kuwa wamefanya hivyo baada ya uchunguzi  wao kubaini kuwa  maandamano hayo yanaweza kuleta machafuko kutokana na mgopgolo ulivyo.

“Kweli tumezuia kufanyika  kwa maandamano hayo kwani kila upande kuna mambo wanataka kufanya mara huyu anataka hili,huyo mwingine anataka hili hivyo tumeona ni vema tuwakatilie wote  ili kuepusha machafuko ambayo yangeweza kutokea”alisema

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KANDORO AJALI YA MBARALIZI

Monday, September 1, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MKUU WA MKOA WA MBEYA KUFUATIA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandoro kuomboleza vifo vya watu 10 vilivyotokea Mbalizi, Mkoani Mbeya tarehe 29 Agosti, 2014 baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace maarufu kama Daladala Na. T 237 BFB kugongana na lori aina ya Tata Na. T 158 CSV.   Katika ajali hiyo, watu saba wengine walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 10 na wengine saba kujeruhiwa katika ajali hii iliyotokea siku chache baada ya ajali nyingine kutokea Mkoani Tabora iliyoua watu 19 na wengine 81 kujeruhiwa”, amesema Rais katika salamu zake.

Rais Kikwete amesema mfululizo wa ajali hizi unaonyesha dhahiri kuendelea kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa umakini miongoni mwa madereva, hivyo jitihada zaidi zinatakiwa kufanywa kusimamia kikamilifu Sheria ya Usalama Barabarani na kufuatiliwa kwa karibu kwa mienendo ya wanaoendesha vyombo vya moto, ili ajali hizi ziweze kupunguzwa na hata kudhibitiwa kabisa katika barabara zetu.

“Naomba upokee  salamu zangu za rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hiyo, na kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa wafiwa wote kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao”Ameongeza.

Rais Kikwete amesema anatambua machungu waliyo nayo wanafamilia, ndugu na jamaa wa watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo, lakini anawaomba wote wawe wavumilivu na wenye subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.

“Ninawaombea kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea katika hali zao za kawaida ili waweze  kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao”, amemalizia kusema Rais Kikwete katika salamu zake. 


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
31 Agosti,2014