Pages

Wednesday, February 26, 2014

Habari katika picha

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akishuka kutoka juu ya Tenki la maji lenye ujazo wa lita 500,000  katika mradi wa maji safi na mazingira katika kijiji cha Igurusi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya

 Kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Mbarali Dk.Sebastian Siwale akimuonyesha mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro chumba cha upasuaji kwa wakina mama wajawazito katika kituo cha afya cha madibira Wilayani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Miyobweni Wilaya ya Mbarali kuhusu kushiriki katika kuchangia shughuli za maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiangalia tenki la maji katika shule ya sekondari Madibira  Wilaya ya Mbarali lililojengwa kwa lengo la kuhifadhi maji .

Monday, February 10, 2014

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATOA ZAWADI YA PROJECTOR KWA WATEJA WAKE

Meneja masoko wa  kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kanda ya nyanda za juu kusini Jonathan Masenya akimkabidhi zawadi ya Projektor Meneja wa Meneja masoko wa  kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kanda ya nyanda za juu kusini Jonathan Masenya Jenifer Ambilikile baada ya baa hiyo kupata ushindi wa kukua kwa asilimia 25(PROJECT USHINDI) ambapo baa hiyo ilipata ilizawadiwa  seti ya Projetor ,Viti 48 na meza 12.



Meneja masoko wa  kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kanda ya nyanda za juu kusini Jonathan Masenya akiwa kwenye maandalizi ya kutoa zawadi  ya Projector  kwa baa ya Mama mwaji iliyopo katika viwanja wa maonyesho ya nane nane jijini Mbeya

Thursday, February 6, 2014

TAKUKURU yawafikisha mahakamani watumishi wanne wa halmashauri ya mbarali

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Mbeya imewafikisha katika mahakama ya hakimu mkazi  Wilaya ya Mbarali  watendaji  wanne wa halmashauri ya Wilaya  hiyo kwa makosa  tisa likiwemo la kutoa malipo hewa  kwa  Watumishi.
 
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya  Gwaya Sumaye aliwataja washitakiwa hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa mganga mkuu wa Wilaya ya Mbarali Dk Somoka Mwakapala ambaye amehamishiwa Wilaya ya  Handeni Mkoani Tanga.

Wafanyabiashara Tunduma waishangaa serikali

Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akiwa mpaka wa Tanzania na Zambia Tunduma Wilaya ya Momba akikagua mpaka huo hivi karibuni
Wafanyabiashara  wa mamlaka ya mji mdogo Tunduma Wilaya ya Momba mkoani Mbeya wameishangaa serikali kushindwa kumdhamini  mfanyabiashara ambaye ni mwekezaji wa ndani atakayeweza kutengeneza ajira na badala yake anadhaminiwa mbunge atakayedumu madarakani kwa miaka mitano.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika moja ya miradi ya maendeleo katika kijiji cha Mshewe halmshauri ya Wilaya ya Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amebaini madudu katika halmashauri  ya Wilaya ya Mbeya baada ya  Sh 208 milioni kutolewa  kwenye kikundi kisicho halali (kikundi  hewa)  na kati ya hizo Sh21milioni zikiwa zimetumika  katika kijiji cha Imezu  kata ya Itewe  Wilayani humo.
 
Kandoro alibaini hayo juzi alipotembelea kijiji hicho ambapo kuna ujenzi wa mradi   wa mfereji wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ulioibuliwa na wananchi  unaotarajia kugharimu kiasi cha Sh 208 milioni hadi kukamilika kwake.

Habari katika picha

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa baraka FM Charles Mwaipopo wa kwanza kushoto na mwandishi wa gazeti la  jambo leo Moses Ng`wati  wa katikati wakipokea maelekezo kutoka kwa Mwandishi wa mkongwe Ulimboka Mwakilili baada ya kukutana katika maeneo ya Posta jijini Mbeya .

Wednesday, February 5, 2014

HABARI KATIKA PICHA

 Mwandishi wa habari wa TBC 1 Hosea Cheyo akiwa kazini katika skimu ya  umwagiliaji katika kijiji cha mshewe Wilaya ya Mbeya vijijini.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akisikiliza maelezo kuhusu shamba la mfano lililopandwa bila kulimwa kwa lengo kutunza mazingira(kilimo hifadhi) kwa kuzuia mmomyoko katika kikijiji cha mshewe  kutoka kwa mkulima Philimon Mwajegele.

Tuesday, February 4, 2014

Ziara ya Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba

 Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akipata maelekezo ya jiwe la mpaka wa Tanzania Zambia wa Tunduma kutoka kwa Ofisa wa uhamiaji Japhet Abel mara baada ya kutembelea mpaka huo.
 Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akipata maelekezo ya jiwe la mpaka wa Tanzania Zambia wa Tunduma kutoka kwa Ofisa wa uhamiaji Japhet Abel mara baada ya kutembelea mpaka huo.




Momba.Zaidi ya Sh18 bilioni zimekusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)idara ya forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya katika kipindi cha kuanzia julai 2013 hadi Desemba 2013.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ya mpaka wa Tunduma Alphonse Kwikubya  mbele ya Naibu Waziri wa Fedha ,Mwigulu Nchemba alipofanya ziara katika mpaka huo kwa lengo la kuangalia shughuli zinazofanyika katika mpaka .

Alisema kuwa mapato hayo ni sawa na asilimia 90.34 ambapo  makadilio yalikuwa ni Sh20.8bilioni na kwamba  mpaka huo unatoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka zaidi ya   500 hadi 700 kwa siku .

Kwikubya alisema  kuwa wengi wa wageni hao wanatokea nchi za Zambia,Zimbabwe,Botswana,Congo DRC na Afrika Kusini   na kwamba  mpaka huo unaurefu wa Kilometa 150 hivyo uthibiti wake unakuwa mgumu kwa sababu mbali mbali.

Alizitaja sababu kuu mbili ugumu wa udhibiti wa mpaka huo kuwa ni pamoja na eneo kuwa na vipenyo vingi haramu na liko wazi sana kupitika kirahisi na wenyeji wa eneo hilo ambao ni kabila la Wanyamwanga kuwa na mwingiliano  mkubwa.

“Wanamwingiliano mkubwa  wa kijamii,kiutamaduni na mila hivyo kuwahudumia kwa taratibu na sheria za nchi wanaona bughudha  kwani wanahisi ni haki yao  ya kihistoria hivyo wahalifu wanatumia mwanya huo kufanya vitendo vyao  vya uhalifu”alisema

Aidha alieleza changamoto zinazoukabili mpaka huo kuwa ni pamoja na ujenzi holela katika  eneo la mpaka baadhi ya watu wa tunduma kutokuwa na uzalendo hivyo kuficha kuwezesha wahalifu na wakati mwingine kupiga vita vyombo vya dola vinaposhughulikia wahalifu kama wavusha vipodozi  visivyoruhusiwa na wafanya magendo ya sukari.

Alisema changamoto nyingine kuwa ni pamoja na ukosefu wa umeme mpakani Tunduma ni tatizo sugu ambalo linaathiri utendaji kazi hasa nyakati za usiku ambapo kituo hufanya kazi masaa 24.


Momba.Wafanyabiashara  wa mamlaka ya mji mdogo Tunduma Wilaya ya Momba mkoani Mbeya wameishangaa serikali kushindwa kumdhamini  mfanyabiashara ambaye ni mwekezaji wa ndani atakayeweza kutengeneza ajira na badala yake anadhaminiwa mbunge atakayedumu madarakani kwa miaka mitano.
 
Waliyasema hayo jana mbele ya  Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba katika risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara,viwanda na kilimo(TCCIA) Wilaya ya Momba Simon Kitojo  kwenye m kutano uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya High Class Tunduma.

“Tunashangaa tunaposikia mwanasiasa husudani Mbunge ndani ya miaka mitano ya kuchaguliwa kwake  serikali inamdhamini mkopo bila dhamana yoyote wa zaidi ya Sh300milioni laki ni serikali hiyo hiyo inashindwa kumdhamini mfanyabiashara ambaye atawekeza  ndani ya nchi kwa muda mrefu zaidi na kuongeza ajira ambayo ndiyo atitizo na kilio cha serikali yetu cha watu kukosa ajira”alisema Mwenyekiti huyo

Kitojo alisema kuwa Serikali kimekuwa kiimba wimbo  wa kutaka kuona Tanzania ina kuwa ni nchi ya viwanda kwa maana ya kuimarisha sekta ya kilimo na uongezaji wa thamani ya mazao.

”Kwa wimbo huu hatuoni kama inasema kweli na sisi tunaona kama inaongelea zaidi wawekezaji wa nje kuliko  wa ndani kwa vile wa tanzania wengi hasa wafanyabiashara wanajulikana nguvu yao na dhamana zao hivyo hawawezi kuwekeza kwa kiwango kinachotakiwa bila ya serikali kusimama kama dhamana ya mkopaji kwa kuywa dhama zetu ni za mikopo ya kujikimu tu na sio kuanzisha miradi mikubwa”alisema

Aidha  alisema kuwa kuna changamoto za kimfumo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara ambpo toka serikalik ilipojitoa kwenye uchumi hodhi na sekta binafsi kuendesha uchumi huku serikali ikikusanya kodi pekee hakujawa na elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wake juu ya kuwaelimisha wafanyabiashara kufanya biashara kwa ufanisi zaidi.

“Tunaiomba  serikali ishirikiane na sekta binafsi kuendesha mafunzo nchi nzima kwa wafanyabiashara kwa lengo la kujua haki zao,kujitambua,kujua wajibu wake kwa Taifa na hiyo tunaamini itapunguza sana migongano kati ya serikali na sekta binafsi”alisema 

Alisema kuwa  wafanuabiashara wanajiona kama wameachwa na serikali na wala haitaki kuwahudumia na kwamba wanaonana na serikali wakati wa kodi na michango mbali mbali pekee.

 
Momba.Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba amesema kuwa eneo ambalo atahakikisha linafanikiwa katika Wizara hiyo ni ikubana matumizi ikiwa ni pamoja na kuangalia upya mfumo unaotumika katika sheria ya manunuzi.

Akizungumza na Wafanyabiashara wa  mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya alisema kuwa alisema kuwa serikali inabeba mzigo mkubwa kutokana na kuwepo kwa sheria ya manunuzi kwa kufanya manunuzi ya gharama kubwa badala ya gharama halisi.