Pages

Tuesday, February 4, 2014

Ziara ya Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba

 Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akipata maelekezo ya jiwe la mpaka wa Tanzania Zambia wa Tunduma kutoka kwa Ofisa wa uhamiaji Japhet Abel mara baada ya kutembelea mpaka huo.
 Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akipata maelekezo ya jiwe la mpaka wa Tanzania Zambia wa Tunduma kutoka kwa Ofisa wa uhamiaji Japhet Abel mara baada ya kutembelea mpaka huo.




Momba.Zaidi ya Sh18 bilioni zimekusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)idara ya forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya katika kipindi cha kuanzia julai 2013 hadi Desemba 2013.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ya mpaka wa Tunduma Alphonse Kwikubya  mbele ya Naibu Waziri wa Fedha ,Mwigulu Nchemba alipofanya ziara katika mpaka huo kwa lengo la kuangalia shughuli zinazofanyika katika mpaka .

Alisema kuwa mapato hayo ni sawa na asilimia 90.34 ambapo  makadilio yalikuwa ni Sh20.8bilioni na kwamba  mpaka huo unatoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka zaidi ya   500 hadi 700 kwa siku .

Kwikubya alisema  kuwa wengi wa wageni hao wanatokea nchi za Zambia,Zimbabwe,Botswana,Congo DRC na Afrika Kusini   na kwamba  mpaka huo unaurefu wa Kilometa 150 hivyo uthibiti wake unakuwa mgumu kwa sababu mbali mbali.

Alizitaja sababu kuu mbili ugumu wa udhibiti wa mpaka huo kuwa ni pamoja na eneo kuwa na vipenyo vingi haramu na liko wazi sana kupitika kirahisi na wenyeji wa eneo hilo ambao ni kabila la Wanyamwanga kuwa na mwingiliano  mkubwa.

“Wanamwingiliano mkubwa  wa kijamii,kiutamaduni na mila hivyo kuwahudumia kwa taratibu na sheria za nchi wanaona bughudha  kwani wanahisi ni haki yao  ya kihistoria hivyo wahalifu wanatumia mwanya huo kufanya vitendo vyao  vya uhalifu”alisema

Aidha alieleza changamoto zinazoukabili mpaka huo kuwa ni pamoja na ujenzi holela katika  eneo la mpaka baadhi ya watu wa tunduma kutokuwa na uzalendo hivyo kuficha kuwezesha wahalifu na wakati mwingine kupiga vita vyombo vya dola vinaposhughulikia wahalifu kama wavusha vipodozi  visivyoruhusiwa na wafanya magendo ya sukari.

Alisema changamoto nyingine kuwa ni pamoja na ukosefu wa umeme mpakani Tunduma ni tatizo sugu ambalo linaathiri utendaji kazi hasa nyakati za usiku ambapo kituo hufanya kazi masaa 24.


Momba.Wafanyabiashara  wa mamlaka ya mji mdogo Tunduma Wilaya ya Momba mkoani Mbeya wameishangaa serikali kushindwa kumdhamini  mfanyabiashara ambaye ni mwekezaji wa ndani atakayeweza kutengeneza ajira na badala yake anadhaminiwa mbunge atakayedumu madarakani kwa miaka mitano.
 
Waliyasema hayo jana mbele ya  Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba katika risala yao iliyosomwa na Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara,viwanda na kilimo(TCCIA) Wilaya ya Momba Simon Kitojo  kwenye m kutano uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya High Class Tunduma.

“Tunashangaa tunaposikia mwanasiasa husudani Mbunge ndani ya miaka mitano ya kuchaguliwa kwake  serikali inamdhamini mkopo bila dhamana yoyote wa zaidi ya Sh300milioni laki ni serikali hiyo hiyo inashindwa kumdhamini mfanyabiashara ambaye atawekeza  ndani ya nchi kwa muda mrefu zaidi na kuongeza ajira ambayo ndiyo atitizo na kilio cha serikali yetu cha watu kukosa ajira”alisema Mwenyekiti huyo

Kitojo alisema kuwa Serikali kimekuwa kiimba wimbo  wa kutaka kuona Tanzania ina kuwa ni nchi ya viwanda kwa maana ya kuimarisha sekta ya kilimo na uongezaji wa thamani ya mazao.

”Kwa wimbo huu hatuoni kama inasema kweli na sisi tunaona kama inaongelea zaidi wawekezaji wa nje kuliko  wa ndani kwa vile wa tanzania wengi hasa wafanyabiashara wanajulikana nguvu yao na dhamana zao hivyo hawawezi kuwekeza kwa kiwango kinachotakiwa bila ya serikali kusimama kama dhamana ya mkopaji kwa kuywa dhama zetu ni za mikopo ya kujikimu tu na sio kuanzisha miradi mikubwa”alisema

Aidha  alisema kuwa kuna changamoto za kimfumo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara ambpo toka serikalik ilipojitoa kwenye uchumi hodhi na sekta binafsi kuendesha uchumi huku serikali ikikusanya kodi pekee hakujawa na elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wake juu ya kuwaelimisha wafanyabiashara kufanya biashara kwa ufanisi zaidi.

“Tunaiomba  serikali ishirikiane na sekta binafsi kuendesha mafunzo nchi nzima kwa wafanyabiashara kwa lengo la kujua haki zao,kujitambua,kujua wajibu wake kwa Taifa na hiyo tunaamini itapunguza sana migongano kati ya serikali na sekta binafsi”alisema 

Alisema kuwa  wafanuabiashara wanajiona kama wameachwa na serikali na wala haitaki kuwahudumia na kwamba wanaonana na serikali wakati wa kodi na michango mbali mbali pekee.

 
Momba.Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba amesema kuwa eneo ambalo atahakikisha linafanikiwa katika Wizara hiyo ni ikubana matumizi ikiwa ni pamoja na kuangalia upya mfumo unaotumika katika sheria ya manunuzi.

Akizungumza na Wafanyabiashara wa  mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya alisema kuwa alisema kuwa serikali inabeba mzigo mkubwa kutokana na kuwepo kwa sheria ya manunuzi kwa kufanya manunuzi ya gharama kubwa badala ya gharama halisi.


Mwigulu alisema kuwa manunuzi yanakwamisha maendeleo ya nchi kwani asilimia 70 ya bajeti ya serikali ni manunuzi “utakuta serikali inaendesha  bajeti za aina tatu na watendaji wasio waaminifu  kwenye halmashauri  wanagawana zabuni kwa ajili ya masilahi yao binafsi”alisema 

“Ukikuta jengo la kanisa au msikiti  ni imara na la bei nafuu limejengwa kwa mfumo wa kawaida lakini asilimia kubwa ya majengo yanayojengwa na serikali kwa mfumo wa zabuni ni mabovu na yametumia gharama kubwa”alisema 

Alisema kuwa katika kuhakikisha hayo yote yanakwisha atawasilisha mapendekezo  katika kipengele cha usimamizi wa fedha na kwamba  hatua zinazochukuliwa dhidi ya wabadhilifu wa fedha za serikali katika halmashauri za Wilaya na jiji za kuwahamisha ni lazima zifanyiwe marekebisho.

“Mfumo wa kuwahamisha watendaji wasio waadilifu  unachangia kuwepo kwa kiburi kwani kuhama haijawahi  kuwa adhabu  ya mtu aliyefanya makosa eti wanasema haki za binadamu je hizi haki zipo kwa watu wenye makosa pekee hapana hatuwezi kuvumilia hili lazima marekebisho yafanyike katika kuchukua hatua za hawa watu”alisema 

Aidha kuhusu mashine za EFD Mwigulu amewataka wafanyabiashara hao kubadilika na kutumia mashine hizo kwa ajili ya manufaa yao na ya Serikali kwa ajili ya kusaidia mahitaji muhimu ya kijamii kutekelezeka badala ya kuyageuza kisiasa.

“Mambo ambayo yananikera ni pamoja na urasimu kwani kitu kinapotokea badala ya kufanya utekelezaji  tunakimbilia kuunda tume tunachelewa kutekeleza  na kuwa nyuma kimaendeleo  kwani wanasiasa wa sasa wanajali masilahi yao binafsi,vijana wenzagu tubadilike niungwana na uzalendo kutumia  muda kutafakari  mara baada ya jambo kutokea ndipo tuchukue hatua”alisema 

Alisema kuwa Taifa kuwa tegemezi ni jambo la aibu na huduma za kijamii bado siyo ya kuridhisha na mtiririko wa fedha za maendeleo hauna kiwango cha kuridhisha “sasa mapato yatatoka wapi kwani haya yote yanategemea mapato ya ndani ili tuweze kusonga mbele katika maendeleo”alisema

0 comments: