Pages

Thursday, September 24, 2015

WAISLAMU WAASWA KUDUMISHA AMANI KWENYE UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akizungumza na waislamu waliojumuika kwenye ibada ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa kumbukumbu ya  Sokoine jijini Mbeya leo asubuhi

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wa dini hiyo wakati wa ibadaa ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo asubuhi

Imamu wa Msikiti wa Isanga Shekhe Ibrahimu Bombo akitoa hotuba ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa Sokoine leo asubuhi

Baadhi ya akina mama wa Kiislamu wakishiriki ibada ya swala ya Idd el Haj kwenye uwanja wa Sokoine

Waumini wa dini ya Kiislamu Mbeya









Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu walioshiriki Ibada ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine leo asubuhi(Picha zote kwa Hisani ya Mkwinda Blog)

WAUMINI wa dini ya Kiislamu mkoani Mbeya wameungana na waislamu wenzao duniani kwa kushiriki ibada ya swala ya Idd el Haj na kutakiwa kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu.

Wito huo umetolewa leo asubuhi wakati wa ibada hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine na kuhudhuriwa na mamia ya waaislamu kutoka pende zote za Jiji la Mbeya.

Akizungumza mara baada ya ibada hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya aliwataka waislamu na wananchi kwa ujumla kushiriki katika vyema katika uchaguzi mkuu wakiepuka vitendo viovu ambavyo vinaweza kuchochea vurugu inayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Kwa upande wake Imamu wa msikiti wa Isanga Shekhe Ibrahimu Bombo alisema kuwa amani na utulivu uliyopo nchini umetokana na wananchi kufuata taratibu kanuni na sheria za nchi na kuwa si vyema wananchi wakakiuka taratibu zitakazosababisha kuingia katika umwagikaji wa damu.

Akinukuu aya za kitabu cha Koran Tukufu Shekhe Bombo alisema ni haramu damu ya binadamu kumwagika bila sababu za msingi na kuwa yoyote atakayesababisha damu kumwagika ataadhibiwa na Mwenyezi Mungu siku ya kiama.

Alisema kuwa zipo baadhi ya nchi ambazo zimeingia katika migogoro iliyosababisha umwagikaji wa damu kutokana na vita hali ambayo haipaswi kutokea katika nchi ambayo imekuwa kimbilio la wakimbizi kutokana na kuwepo kwa amani na utulivu.

Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Mbeya wameungana na waiislamu wenzao duniani ,kuadhimisha ibada ya Eid El Haj wakiungana na waislamu wengine wanaohudhuria ibada ya Hija huko Mecca Saudi Arabia.

Monday, September 21, 2015

MGOMBEA WA CCM ADAIWA KUAHIDIWA UWAZIRI

Katibu wa CCM Mbeya mjini Kerenge akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya mjini Sambwee Shitambala katika mkutano wa kampeni wa Ubunge jimbo la Mbeya mjini kata ya Itezi
Mwenyekiti wa CCM Mbeya mjini Ephrahimu Mwaitenda akizungumza na wakazi wa kata ya Itezi kwenye mkutano wa kampeni za Ubunge jimbo la Mbeya mjini


Meneja Kampeni wa Mbunge wa Mbeya mjini Charles Mwakipesile akizungumza na wakazi wa Jimbo la Mbeya kata ya Itezi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Sambwee Shitambala
Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya mjini Sambwee Shitambala akizungumza na wakazi wa kata ya Itezi kwenye mkutano wa kampeni za Ubunge leo jioni.

Mgombea Udiwani wa kata ya Itezi kwa tiketi ya ACT Bakari Hamisi akiuliza swali kwa mgombea Ubunge wa CCM kwenye mkutano wa kampeni leo jioni

Na Ripota Wetu
WAKAZI wa kata ya Itezi jimbo la Mbeya mjini wamehakikishiwa kuwa mgombea Ubunge wa CCM jimboni humo Sambwee Shitambala akichaguliwa anayo nafasi ya kuwa Waziri kwenye serikali itakayoundwa na Dkt. John Magufuli.
Akizungumza wakati wa kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Meneja wa kampeni wa mgombea huyo Charles Mwakipesile aliwahakikishia wakazi wa Kata hiyo kuwa Shitambala anayo nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa Waziri akichaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Alisema uwezo alionao Shitambala unaendana na hadhi ya Jiji hilo na kuwa ni vyema wakazi wa Jiji hilo wakathamini uwezo wake na kumchagua ili Jiji lipate heshima ya kuwa na Waziri kwenye serikali ya awamu ya tano itakayoundwa na Dkt. Magufuli.
Kwa upande wake Shitambala aliwahakikishia wakazi wa Jiji la Mbeya hasa vijana kuwa uwezekano wa wao kupata ajira bora utaendana na wao kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ndicho pekee chenye sera ya kuboresha maisha ya wananchi wake.
Alisema vijana wanayo nafasi kubwa ya kuwa na ajira bora kupitia sera za mgombea urais wa CCM Dkt. Magufuli ambaye ameahidi kufufua viwanda vilivyokufa.
Shitambala alisema kuwa njia pekee ya vijana kuishi kwa amani na utulivu ni kukichagua CCM ili kuepuka vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani na kuwa yeye atasimamia kuwepo kwa amani na salama na vijana kujishughulisha zaidi na mambo ya maendeleo badala ya vurugu.
Kampeni za uchaguzi mkuu zinaendelea katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya huku wagombea wakiendelea kunadi sera zao kwa wananchi ili kuchaguliwa kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Saturday, September 19, 2015

MBEYA CITY YAPIGISHWA LIGWARIDE NA PRISON YATANDIKWA 1-0

Wachezaji wa timu ya Tanzania Prison wakishangilia goli mara baada ya timu yao kushinda kwa kuifunga timu ya Mbeya City Bao 1-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine leo jioni.


Kikosi cha Mbeya City kilichopigishwa kwata na wajelajela timu ya Prison kwenye uwanja wa Sokoine leo jioni

Kikosi cha Tanzania Prison kilichowapigisha kwata Mbeya City leo jioni.

Kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi akitafakari jambo katika benchi la timu yake katika mchezo wa ligi kuu iliyozikutanisha timu hizo, Mbeya City alipachikwa bao 1-0

Kocha wa Prison Salum Mayanga akiwa katika benchi la Ufundi katika mchezo uliozikutanisha timu hizo leo jioni, ;Prison ilitoka kifua mbele kwa kuichapa Mbeya City Ba0 1-0

Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mechi ya ligi kuu kati ya Mbeya City na Prison, matokeo katika mchezo huo Prison iliichapa , Mbeya City bao 1-0


Sunday, September 13, 2015

NI SIKU YA MWANAHABARI ANNA NKINDA NA MJEDA JULIUS NTIBASANA

Rahaa ya ndoaa Anna Nkinda akiwa amebebwa na mumewe Julius Ntibasana baada ya kufungwa ndoa yao mjini Dodoma 

Bibi harusi Anna Nkinda akiwa katika pozi baada ya kufunga ndoa na mumewe Julisu Ntibasana

Hata ndege huruka pamoja na kufurahia maisha!! nanyi mfurahie maisha ya ndoa yenu Mungu awabariki Anna na Julius


Monday, September 7, 2015

NDEREMO NA VIFIJO SENDOFF YA MWANAHABARI ANNA NKINDA-MBEYA


Mmiliki wa Blogu hii Brandy Nelson akiongozana na wanahabari nwenzie kwa ajili ya kumtunza mwanahabari mwenzao Anna Nkinda kwenye SendOff iliyofanyika katika  ukumbi wa kanisa la Kilutheri Jijini Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita


Tumpambe Dadaetu!!! Tumpambe Maua!!! ndivyo ambavyo wanaoenekana wanahabari Charles Mwakipesile na Brandy Nelson wakati wakimtuza mwanahabari mwenzao Anna Nkinda wakati wa SendOff yake mwishoni mwa wiki




Nao wafanyakazi kutoka Idara ya Habari Maelezo Bw. Mwakilasa na Bibi Mwasandube wakimtunukia zawadi Anna Nkinda wakati wa SendOFF kwenye ukumbi wa kanisa la Kilutheri Jijini Mbeya.
Sherehe iliendelea kunoga

Anaameremetaaaaa!!!!








Bibi harusi mtarajiwa akimlisha keki mmoja wa wapambe wake!!!! ni rahaaa tuuuu!!!!

Asante mama kwa kunilea na kunikuza hadi leo unanikabidhi kwa wengine!!! ndivyo anavyoonekana kusema Anna Nkinda wakati akimkabidhi mama yake Keki