Pages

Thursday, September 24, 2015

WAISLAMU WAASWA KUDUMISHA AMANI KWENYE UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akizungumza na waislamu waliojumuika kwenye ibada ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa kumbukumbu ya  Sokoine jijini Mbeya leo asubuhi

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wa dini hiyo wakati wa ibadaa ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo asubuhi

Imamu wa Msikiti wa Isanga Shekhe Ibrahimu Bombo akitoa hotuba ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa Sokoine leo asubuhi

Baadhi ya akina mama wa Kiislamu wakishiriki ibada ya swala ya Idd el Haj kwenye uwanja wa Sokoine

Waumini wa dini ya Kiislamu Mbeya









Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu walioshiriki Ibada ya swala ya Idd El Haj kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine leo asubuhi(Picha zote kwa Hisani ya Mkwinda Blog)

WAUMINI wa dini ya Kiislamu mkoani Mbeya wameungana na waislamu wenzao duniani kwa kushiriki ibada ya swala ya Idd el Haj na kutakiwa kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu.

Wito huo umetolewa leo asubuhi wakati wa ibada hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine na kuhudhuriwa na mamia ya waaislamu kutoka pende zote za Jiji la Mbeya.

Akizungumza mara baada ya ibada hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya aliwataka waislamu na wananchi kwa ujumla kushiriki katika vyema katika uchaguzi mkuu wakiepuka vitendo viovu ambavyo vinaweza kuchochea vurugu inayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Kwa upande wake Imamu wa msikiti wa Isanga Shekhe Ibrahimu Bombo alisema kuwa amani na utulivu uliyopo nchini umetokana na wananchi kufuata taratibu kanuni na sheria za nchi na kuwa si vyema wananchi wakakiuka taratibu zitakazosababisha kuingia katika umwagikaji wa damu.

Akinukuu aya za kitabu cha Koran Tukufu Shekhe Bombo alisema ni haramu damu ya binadamu kumwagika bila sababu za msingi na kuwa yoyote atakayesababisha damu kumwagika ataadhibiwa na Mwenyezi Mungu siku ya kiama.

Alisema kuwa zipo baadhi ya nchi ambazo zimeingia katika migogoro iliyosababisha umwagikaji wa damu kutokana na vita hali ambayo haipaswi kutokea katika nchi ambayo imekuwa kimbilio la wakimbizi kutokana na kuwepo kwa amani na utulivu.

Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Mbeya wameungana na waiislamu wenzao duniani ,kuadhimisha ibada ya Eid El Haj wakiungana na waislamu wengine wanaohudhuria ibada ya Hija huko Mecca Saudi Arabia.

0 comments: