Pages

Friday, June 20, 2014

MWANAFUNZI AUA MWANAFUNZI MWENZIE KWA KUMPIGA NA JIWE KICHWANI

Mbeya. Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule Sekondari NzondaHaki ya jijini Mbeya na mkazi wa Nzovwe jijini hapa, amefariki dunia baada ya kupigwa na jiwe kichwani.



Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakaeli Masaki alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Joshua Buku (19) na kwamba ilidaiwa kuwa alipgwa jiwe kichwani na kijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Joshua Sadi (17) mzaki wa Simike wote wa jijini Mbeya.

Thursday, June 19, 2014

BASI LA NEWFORCE LAUA WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI IGURUSI MBEYA

Mbeya.Watu  wawili wamekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa baada ya  kugongwa  na basi  la kampuni ya Newforce  kuligonga gali lingine aina ya Fuso na kuacha njia na kuwagonha watembea kwa mguu  katika kijiji cha Igurusi Wilaya ya Mbarali  Mkoani Mbeya .

 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi aliwataja waliokufa katika  ajali hiyo kuwa ni pamoja na Theresia Hingi (65) na Mary Kizito (26)  wote wakazi wa igurusi  ambapo walifariki papo hapo.

JAMMBAZI LAUAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI NA POLISI TUNDUMA MBEYA



 Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akionyesha Bunduki  aiana ya ShortGun iliyokamatwa  kwenye tukio la majibizano ya risasi baina ya majambazi na askari polisi katika eneo la Msikitini Mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya na kusababisha kifo cha jambazi mmoja .

Thursday, June 12, 2014

AUA MKE WAKE KWA KUMCHOMA KISU SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI

Mbeya .Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti Mkoani hapa akiwemo Mwanamke mmoja mkazi wa  kijiji cha Isangati Mbeya vijijini  aliyekufa baada ya  kumchomwa  kisu  na mume wake  huku akiwa amelala.

Akizungumzia  matukio hayo kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Madawa Jaston (29)na kwamba tukio  hilo  lilitokea jana majira saa  5:00 asubuhi kijijini hapo.

WAKALA WA VIPIMO MKOA WA MBEYA WAFANYA MKUTANO NA WADAU WA VIPIMO

 Kaimu meneja wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya Deogratius Hussein akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi Kaimu katimu tawala Mkoa wa Mbeya Leonard Magacha katika ukumbi wa Goden City Hotel
 Wadau wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya wakiendelea na mkutano katika ukumbi wa Goden City Hotel
Kaimu katibu tawala Mkoa wa Mbeya (RAS)Leonard Magacha akitoa hotuiba yake katika mkutano wa wadau wa wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya.


Mbeya.Wakala wa vipimo (WMA)ametakiwa kujiimarisha  kwakufanya ukaguzi wa  mara kwa mara katika maeneo ya masoko ili kuweza  kutatua tatizo la Lumbesa linalosababisha wananchi na wakulima kudhurumiwa mazao yao.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu katibu tawala  Mkoa wa Mbeya Leonard  Magacha katika mkutano wa pamoja wa wadau wa  wakala wa vipimo uliofanyika katika ukumbi  Mbeya  Gorden City  jijini hapa.

RIFT YA KWANZA MKOANI MBEYA YAZINDULIWA KATIKA JENGO LA CHAMA CHA WALIMU

Mmoja wa Walimu akiimbia shairi katika siku ya uzinduzi wa Rift ya Kwanza katika Mkoa wa Mbeya kwenye jengo  la ghorofa sita mali ya  chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoani Mbeya na ndiyo jengo lefu kuliko yote katika jiji la Mbeya 
 Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza  katika uzinduzi wa Rift ya kwanza  Mkoani Mbeya katika jengo la  Ghorofa sita mali ya chama cha Walimu Mkoa wa Mbeya

Wednesday, June 11, 2014

HABARI KATIKA PICHA ZA TUKIO LA KIKAO CHA KWANZA CHA KAMATI YA MAANDALIZI YA HARUSI YA JOHN MTUMURI (mchina wa soweto)

Bwana Harusi Mtarajiwa  John Mtumuri akikabidhi fedha kwa mtunza hazina  Akibearali Mbuta wa kamati ya maandalizi ya harusi yake inayotarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu,

Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya harusi hiyo wakiwa kwenye kikao cha kwanza

Wajumbe wa kamati ya maandalizi wakipata chakula katiika kikao cha kwanza

Mtunza hazina na Bwana harusi wakiwa katika mchakato kupokea ahadio za wajumbe wa kamati hiyo

 Mjumbe wa kamati ya maadalizi ya harusi hiyo Lugano Mwangobola akichukua chakula
Nyuma aliyeshika kipaza sauti  ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Adam Mwakatumbula akipokea ahadi kutoka kwa wajumbe

 Bwana harusi mtarajiwa John Mtumuri akijadiliana jambo na Mtunza hazina wa kamati hiyo Akberali kwenye kikao cha kwanza cha maandalizi ya harusi yake.
 Mjumbe wa kamati Samwel Access computor akitoa ahadi yake mbele ya Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Adam Mwakatumbula
 Wajumbe wakichukua chakula kilichoandaliwa kwa jali ya kikao cha kwanza
 Wajumbe wa kamati ya maandalizi wakiwa kwenye kikao
Viongozi wa kamati wakijadiliana na jambo
 Wajumbe wa kamati wakiendelea na kikao
 Mmoja wa Wajumbe wa kamati hiyo Yona Mwakalasya (Nafuu Phone) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kamati hayupo pichani.

Wakina mama wa Soweto hawakuwa nyuma katika kumuunga mkono John Mtumuri katika kikao cha kwanza cha kamati ya maandalizi ya harusi yake

Wakina mama wakiwa wamevalia sare katika kikao cha kwanza cha kamati ya maandalizi ya harusi ya John Mtumuri

Sunday, June 8, 2014